Hali ya kutambua/ kutambulika yatoka kwa Mwasisi-Mtambuzi
Ulimwengu uliobuniwa unatambulika. Kilimanjaro ya theluji au ngorongoro ya kijani yatambulika kwa macho. Ijapokuwa tunautambua ulimwengu lakini wenyewe haujitambui. Mata (matter) na nguvu (energy), mwamba na umeme, kompyuta na roboti havijitambui. Havina utambuzi wa nafsi. Haviwezi kutambua nafsini kwa kufikiri, kusikiliza, kukumbuka, kuongea, kuhisi, kuhiari, na hapo hapo kung’amua walichokitambua. Mwanadamu anatoa wapi utambuzi huo? Kama gesi iliyojilipukia (“big bang”) ilizua wanadamu wenye utambuzi, iweje chanzo kisichojitambua (mlipuko) kitofautiane na zao lake linalojitambua (mtu)? Hakika, wanadamu wenye ufahamu wametoka kwa Muumba mwenye-ufahamu. Mtu anamtambua Muumba na Muumba anamtambua mtu—wawili wanafahamiana hata kama wachukua muda kujuana. Mungu ndiye "akiisha kuwawekea walimwengu nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu." (Matendo 17:26b,27)

MAANGUKO KAMILI
La ajabu, miaka 100 kabla Babeli haijafikia kilele cha ukuu wake, nabii Isaya alishatabiria kuangushwa kwake kwa maneno thabiti sana. Katika kifungu kilichopewa kichwa cha habari 'Mzigo wa Babeli' ni hivi alivyosema.
"...Siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu...Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao...Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa... Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. Lakini huko watalala
hayawani wakali wa nyikani "(Isaya 13:6,17,19-21)
hayawani wakali wa nyikani "(Isaya 13:6,17,19-21)
Hatima ya Babeli inaeleweka: wavamizi watakuwa Wamedi (taifa mashariki ya Babeli); jiji litakuwa maganjo, lisilokaliwa na mtu wala mnyama pori. Tukumbuke utabiri huu ulitolewa miaka 100 kabla ya Babeli kukua kufikia nguvu na utukufu wake.
Nabii mwingine, Yeremia, akiandika miaka 100 baadaye, wakati
Nebukadreza alipokuwa akikaribia kuivamia Yerusalemu, aliongeza mtazamo juu ya anguko la Babeli.
Nebukadreza alipokuwa akikaribia kuivamia Yerusalemu, aliongeza mtazamo juu ya anguko la Babeli.
"BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli upepo uharibuo... Babeli umeanguka na kuangamia ghafla... Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi... Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo pasipo mtu kukaa huko... kuta pana za Babeli zitabomelewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa... Ee BWANA, umenena habari za mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele..."
Na mwishowe nabii anaamriwa kufunga jiwe kwenye gombo la unabii ule na kulitupia ndani ya mto Frati, aseme, "Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena..." (Yeremia:51:1,8,28,37,58,62-64) uwiano kati ya unabii wa Isaya, ulioandikwa miaka 100 kabla ya mamlaka ya Babeli kushamiri, na ule wa Yeremia, ulioandikwa wakati dola na jiji vilipokuwa
katika kilele cha utukufu wake ni mtimilifu. Kwa watu wa siku zile itakuwa ilionekana kama ilivyo kwetu leo tuambiwe miji mikubwa kama London, New York au Sydney itaangamizwa ibakie magofu milele. Katika enzi hii ya silaha za nyuklia, jambo hilo linawezekana; lakini manabii wa Israeli walitamka hayo zaidi
ya miaka 2500 iliyopita wakati hakuna ambaye angeweza kuota kwamba uharibifu kamili namna hiyo ungewezekana.

Historia inaonyesha jinsi ambavyo unabii huo wa maanguko ya Babeli ulivyotimizwa hatua kwa hatua. Wavunjaji wa Kwanza walikuwa Wamedi na Wajemi katika karne ya sita (K.K). Kuanzia wakati huo umwamba wa Babeli ulianza kufifia. Baadaye walikuja Wayunani chini ya Aleksanda Mkuu, wakifuatiwa na Warumi; baada yao makabila kadhaa yapendayo vita kama Wapathi, Waarabu na Watarta.
Kwa karne nyingi mahali halisi pa jiji la Kale la Babeli palikuwa mahame, yaliyoepukwa - wasafiri wasemavyo - na wahamaji wanaotangatanga. Ni hivi karibuni tu wataalamu wa kihistoria wachimbuao chini ( Archaeologists), walipochunguza eneo hilo katika nusu ya kwanza ya karne ya 19, na kugundua mabaki ya kuta kubwa, mahekalu ya nguvu na malango, na masanamu makubwa yaliyoonyesha ulimwengu ulioshikwa na butwaa jinsi ukuu wa Babeli ulivyokuwa enzi zake.
Kwa hiyo historia inatuonyesha jinsi Babeli 'Utukufu wa falme,'
ulivyoangushwa na kuachwa, kama manabii wa Israeli walivyotabiri ingekuwa.
ulivyoangushwa na kuachwa, kama manabii wa Israeli walivyotabiri ingekuwa.
Sasa tunageukia mfano wa pili unaotofautiana, unaotuonyesha pia uhakika wa unabii wa Biblia katika:-
====USIKOSE SEHEMU YA SITA ==== HATIMA YA MISRI
Misri iliwahi pia kuwa dola yenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati.
Misri iliwahi pia kuwa dola yenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment