Sunday, July 23, 2017

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: one or more people, ocean, text and outdoor
Wanadamu wote wanamuwazia Mungu. Waumini, wasioamini, au wanaodai hawajui kuwa Mungu yupo huwa wanachukua msimamo wao baada ya kuingiwa na kupambana na wazo lenyewe.
Lakini, wazo linatua kichwani likitokea wapi?
Aidha wazo limetoka ndani ya mtu au nje. Tujuavyo, chanzo huwa kikuu kupita matokeo yake (Mjapani ni mkuu kuliko Toyota). Kwa kuwa “Mungu” wa vichwani mwao hufikiriwa kuwa mkuu (katika wema, uweza na busara) kuliko yeyote wanayemjua (kuliko baba au mama), basi dhana ya uwepo wa Mungu ni akisi ya uhalisia uliopo nje ya vichwa vyao. Dhana haikuibuka vichwani mwao kama uyoga. Kutoka nje, Mungu ameweka, "milele ndani ya mioyo" yao. Ndiyo maana, pamoja na mahangaiko ya kitambo na wakati uliopo, kwa kujua au kutokujua, watu wote huangaikia umilele, hatima yao baada ya maisha yao duniani (Mhubiri 3:11; Matendo 17:26,27).
BIBLIA INATABIRI YAJAYO?
Tunaweza tu kuchunguza historia na uzoefu wetu kutambua kwamba wanadamu kwa jinsi walivyo, hawawezi kujua hata kidogo ya mbeleni. Kwa nini?
Hatuwezi hata kujua litakalotupata usiku wa leo, au kesho tukienda kazini, achilia mbali mwaka kesho; au litakaloipata dunia katika miaka 100, hata tusiposemea miaka 2000! Watu wangekuwa na utambuzi kidogo tu wa mambo yajayo, maamuzi mengi yangebadilika kiasi gani! Ajali nyingi kiasi gani zingeepukwa! Maafa mengi kiasi gani yasingeliachiwa yatokee. Vita vingi kiasi gani visingeanzishwa! Uzoefu katika maisha yetu wenyewe, na wa historia ya mwanadamu unatuonyesha kuwa mwanadamu hana ufahamu wowote wa hakika wa litakalotokea.
Lakini chukulia kwamba mambo yajayo yameelezewa, sio mara moja, bali mara nyingi. Na kwa nyakati zote katika kitabu hicho hicho, Biblia na sio katika kingine chochote duniani! Halipaswi hilo kutufanya tukae chini na kuzingatia? Ndio maana tunasema kwamba unabii wa Biblia ni wa maana sana, na unapaswa kuchunguzwa kwa makini, kwa kuwa mambo mengi mno
yanautegemea. Ni kiashiria ya kwamba upo katika dunia uweza mkuu na nguvu impitayo mwanadamu.
"NDIO, LAKINI..."
Wale wasioamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu, hawapendi kabisa unabii wake. Unapokubali imetabiri kisahihi mambo kabla ya kutokea utakuwa umeanza kukubali uwepo wa Mungu... Kwa hiyo wanajaribu kuielezea mbali.
"Unabii," wanasema, " haukuwa hasa utabiri wa mambo. Uliandikwa baada ya matukio 'unayoyabashiri.'
Sasa hii hoja inaweza kuwa na nguvu kama unaweza kuthibitisha kuwa yale yaliyoandikwa katika Biblia, na hasa yale ya Agano la Kale kwamba yaliandikwa baada ya matukio yanayodaiwa kutokea. Lazima tuseme hapa wazi kwamba hawana uthibitisho wa moja kwa moja juu ya hili; hitimisho lao ni
matokeo tu ya kutafsiri mambo kujiridhisha wapendavyo. Ukweli ni kwamba, utafiti wote uliofanywa katika miaka 100 iliyopita unaonyesha kwamba yaliyoandikwa katika Biblia ni halisi; ni ya nyakati zinazodaiwa kuandikwa.
Lakini kuna njia ya mkato katika jambo hili inayoweza kutusaidia katika lengo letu. Hakuna anayeweza kubisha kudai kwamba maandiko ya Agano la Kale hayakuwepo miaka 200 kabla ya kuzaliwa Kristo, kwa kuwa yalitafsiriwa katika Kiyunani wakati huo, na huwezi kutafsiri kitu kisichokuwepo!
Ubishi mwingine ni kusema, "Ndio, unabii huu wa Biblia ni utabiri wa kijanja wa kisiasa wa watu waliokuwa wakichunguza matukio enzi zao na kuona mwelekeo wa matokeo yake."
Utabiri wa kijanja kisiasa! Uliotolewa karne nyingi kabla ya Kristo na unaoendelea kuwa kweli miaka 2000 hadi leo! Hao manabii walikuwa wachawi wa namna gani kuweza kufanikisha hilo bao? Kusema hivyo ni kuonyesha tu yasivyowezekana maelezo yake.
Lakini jibu la hakika kwa ubishi huu kama ilivyo kwa ubishi mwingine wowote, ni kusoma sehemu ya unabii wenyewe. Kwa hiyo tunaanza na:-
==== USIKOSE SEHEMU YA NNE ==== UNABII KUHUSU BABELI
Katika enzi ya manabii wa Israeli (Kama 850-560 K.K) kuliinukia dola mbili kuu katika maeneo yanayoizunguka mito ya Frati na Tigrisi, katika Iraki ya sasa. Ya kwanza ilikuwa dola ya Ashuru iliyokuwa na makao makuu Ninawi. Kwa karne mbili, Waashuru walivamia ardhi ya mataifa waliowazunguka:
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW