Friday, July 21, 2017

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: cloud, sky and text


Kilichoanza huanzishwa na Muanzilishi
Kila kitu ulimwenguni kina mwanzo ulioanzishwa. Aya hii ipo hapa kwa kuwa mwandishi alimwaga wino juu ya ukurasa huu. Nani aliye hai ambaye hakupokea uhai toka kwa wazazi? Ni mama yupi anayepasisha kwa wanawe uhai ambao hakuupokea kutoka kwa waliomtangulia? Mwanzoni mwa mapokezano hayo ya uhai yupo nani kama si Yeye Aliye na uzima, uzima usio wa kupewa au kuazimwa? Pasipo Mwenye-kitabu hakuna kitabu cha kuazimwa. Tuna uhai wa kuazimwa kwa kuwa yupo Mwenye uhai aliyetuazima. Yeye daima "hapatikani na mauti" (1Tim 6:16); na "ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu" (Matendo 17:28)
Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vyote. Maelezo yake kuhusu chanzo cha uovu; taarifa yake isiyo na kasoro kuhusu mahusiano ya Mungu na taifa la Israel; ujumbe wake unaopenya kupitia kwa manabii wao; 'habari njema' yake iliyohubiriwa na Yesu Kristo na mitume wake; na juu ya yote uchambuzi wake sahihi uhusuo mapungufu ya silka ya mwanadamu ukilinganishwa na utakatifu, kweli na rehema ya Mungu, iliyodhihirishwa zaidi hasa katika Mwanawe - haya yote ni mambo ya kipekee yasiopatikana katika kitabu kingine chochote duniani. Haya yalimfanya Henry Rogers, miaka 100 iliyopita kusema: "Biblia sio namna ya kitabu ambacho mwanadamu angekuwa ameandika kama angeweza, au angeweza kuandika angeweza". Kwa maneno mengine, Mungu anahitajika katika kuelezea uwepo wake.
Katika kazi hii fupi tutaangalia mojawapo ya mambo yake ya ajabu: unabii wake. Kihalisi, unabii sio kuelezea tu mambo ya mbeleni. Nabii alikuwa ni mtu 'aliyesema kwa niaba' ya mwingine, msemaji; na unabii ulikuwa ni ujembe alioutoa nabii kwa niaba ya Mungu. Lakini kwa kuwa unabii wa Biblia unao pia 'utabiri' mwingi wa mambo yajayo, kwa lengo hili tu tutazingatia maana hiyo hapa.
==== USIKOSE SEHEMU YA PILI====
NANI MWENYE MAMLAKA YA UNABII?
Lakini kwanza inabidi tukubaliane juu ya swali moja la muhimu: Biblia inadai kwamba mamlaka ya unabii inatoka kwa Mungu tu na ni uthibitisho wa uweza wake?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW