Friday, July 14, 2017

UMESHA MSAMEHE?


Image may contain: 2 people, text

Mpendwa:
(Mathayo 18:21-22"Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.)
Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mungu Mkuu anakwambia samehe saba mara sabini kwa siku. Cha ajabu watu wa siku hizi wamesha lisahau hili Neno la uzima tena lenye nguvu sana. Kama wewe ni Mkristo halisi, basi utakubaliana nami kuwa, NGUVU YA MSAMAHA ni kubwa kuliko HUKUMU unazo zitoa kwa wale walio kukosea au kosa. Haijalishi wamefanya nini, wewe kazi yako ni kusamehe kama ulivyo samehewa na Yesu.
Isaya 43:25 "Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Umeona hapo kwenye Isaya? Yesu anafuta makosa yako si kwaajili yako bali kwa ajili yake yeye. Kwakuwa yeye ni Mtakatifu na mwenye huruma. Wewe huwezi fanya lolote lile liweze kukupa msamaha, ni kwa mapenzi yake tu, ndio maana umesamehewa. Lakini leo umeshahu na kuanza kuhumu yule aliye tenda dhambi, au yule aliye zini. Je, wewe hukuwai zini?
Waefeso 4:26-27' Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.
Wengi wetu tunalala na vinyongo ndani yetu, huku tukijiita ni Wakristo, tena tulio Okoka. Neno linakwambia, "JUA LISICHWE" huku ukiwa na kinyongo ana au uchungu ndani yako. Huko ni kutenda dhambi. Ukifa na uchingu kwenye moyo wako, basi Jehannam inaweza kuwa yako.
Mathayo 6:12"Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Basi usichoke kuwasamehe deni wadaiwa wako kama mabvyo Yesu ametusamehe.
Luka 17:4 "Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Umesha pewa formula ya kusamehe. Je, upo tayari kumsamehe yule aliye kukosea?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW