Friday, July 14, 2017

TOA KWANZA BORITI KWENYE JICHO LAKO, KISHA UTATOA KIBANZI KWENYE JICHO LA MWENZAKO.

Image may contain: text


Mathayo 7: 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Wakristo watajifunza kutokana na ukosoaji ujengao.
Imeandikwa katika Mithali 9:8-9 " Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; mkaripie mwenye hekima naye atakupenda. mwelimishe mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwenye haki naye atazidi kuwa na elimu."
Nimeweka hili somo kuwakumbusha kuwa, unapo mnyooshea mwenzako kidole kimoja, kuna vidole vingine vitatu vinakunyooshea wewe mwenyewe. Je, umesha jiuliza ni kwanini?
Unaposema, fulani ni mzinifu na mtenda dhambi na apigwe mawe, hata wewe ulisha wai zini lakini haukupigwa mawe.
Tuanze kujichunguza wenyewe, je, sisi sio watenda dhambi kama wale?
Kama wewe ulisha wai mwangalia mdada au mvulana kwa matamanio, BASI WEWE NI MZINZI NA MZINIFU.
Kama wewe ulisha iba hata Penseli au chukua karatasi ofisini kwako, wewe ni MWIZI.
Kama wewe ulisha danganya kwa kuomba kazi au ili upate kitu fulani, wewe ni MUONGO.
Kama wewe ulisha mchukia mtu na kukasirika vibaya, basi wewe ni MUUWAJI. N.K
Je, unaweza nusurika na hukumu ya Mungu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW