Friday, July 14, 2017

QURAN YATHIBITISHA KUWA, YESU NI ZAIDI YA MUHAMMAD


Image may contain: one or more people, people sitting, meme and text



KINACHOMFANYA YESU ASIWE SAWA NA MUHAMMADI, NI HII AYA YA QURAN 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
فاطر (22) Faatir
Wala hawalingani walio hai na maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
Hapo 👆 Tunaambiwa hawalingani walio hai na Maiti,
YESU YEYE YUPO HAI 👇
Ufunuo 1:17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
MUHAMMADI KAFA 👇
( قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ )
الطور (31) At-Tur
Sema: ngojeni na mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongojea (sifi mimi peke yangu, nanyi mtakufa vilevile)
YESU YEYE AMEWEZA KUWASIKILIZISHA SAUTI WALIO MAKABURINI 👇
Yohana 11:38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
MUHAMMAD YEYE AMEAMBIWA KUWA HAWEZI KUWASIKILIZISHA SAUTI WALIOMO MAKABURINI 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
35:22
............. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
Cha ajabu LEO waislamu wamekuwa mahodari wa kuwasomea maiti maneno ya kuwaambia
Abdallah tukiondoka hapa Watakuja malaika nao watakuuliza
"Mola wako nani?" SEMA! "mola wangu ni Allah"
"Nabii wako ni nani?" sema, "Nabii wangu ni Muhammadi "
Sasa ikiwa tu kipenzi cha Allah ameambiwa hana uwezo wa kuwasikilizisha waliomo makaburini, ninyi huo uwezo wa kumzidi mtume wenu mmeutoa wapi?
Imeletwa kwenu na: Abel Suleiman Shiliwa

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW