Friday, July 14, 2017

NANI KAMPA UTUME NA UNABII MTUME MUHAMMAD? SEHEMU YA KWANZA

Image may contain: 3 people, people on stage and text


Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu.
Twazidi pia kukushukuru kwa ajili yakuyafuata mafundisho haya ya Biblia Takatifu.
Twaamini mada ile ile lakini ya tatu kuhusu imani ya kiislamu itakusaidia ukiwa mkristo wa kweli kutoishiriki mihadhara ya ubishi kati ya waislamu na wakristo.
Sababu ya pili, ni kwako ndugu na dada ambaye ungali bado katika upotevu wa uislamu bila yako kujuwa ukweli kwa wazi.
Katika zile sababu zaidi ya 25 zinazotudhihirishia uongo na upotevu wa dini ya uislamu tumetamani kuchimbua «Utume na unabii wa nabii Muhammad s.a.w»
Tunazo sababu zaidi ya mia (100) kuwauliza Waislamu na kitabu chao Qura'n swali tulilolitaja hapo juu na maswali mengine kuhusu UISLAMU na Qura'n! na moja ya hayo maswali ni sababu kitabu chao yaani Qur’ani kinatutaka sisi wakristo kusilimu, lakini kabla tusilimu nakuingia dini ya uislamu ni sherti tumjuwe vyema vilivyo huyu nabii sababu Yesu Kristo anatuonya kwamba manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi yamkini hata wachaguliwa wa Mungu. Mathayo 7 :15-20.
Kwa hivi ni sherti Muhammad atumbukizwe ndani ya Biblia iliyokitangulia kitabu alichopewa ijapokuwa baadaye tutajuwa alikipewa na nani ? na akizama ndani ya Biblia hatuna budi kumfwata na kumtumikia Allah subhanahu wa tahalah! Lakini ikimtema kando huyo si nabii na mtume wa Yehova Mungu.
Ukweli ambao hatuwezi kuupinga ni kwamba Biblia Takatifu ambayo waislamu pia huitumia kwakuichezea-chezea na isitoshe pia kwakuitumia kuwapiga wakristo waliopofushwa wakidhani kwamba waislamu wanaiamini, hiyo Biblia imekuwapo duniani zaidi ya miaka 2000 kabla ya Qur’ani tukufu kuwepo.
Biblia Takatifu inasema hivi:
Kutoaka 20:1-3
«Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.»
Hapa Mungu alitutahazarisha mapema kumpitia mtumishi wake nabii Musa ya kwamba tuepuke kuwa na miungu mingine ila yeye pekee ambaye jina lake ni Yehova!
Haya maneno sawa na Mathayo 7:15-20 Mungu aliyasema kabla ya Muhammad kuwepo, kabla ya Qur’ani kuwepo na kabla kuwepo kwa wanaume 4 walioiandika Qur’ani tukufu ambao ni:Seidinah Umar, Osman, Abubakar na Ali.
Inamaanisha nini?
Ni kwamba kama Mungu mwenyezi anavyokuwa na watumishi kama vile mitume na manabii, vilevile miungu nayo yaweza kuwa namitume na manabii wake.
Kwa mujibu wa Mathayo 7:15-20, Yesu Kristo anatupatia alama yakuwatambuwa manabii wa uongo akisema katika mstari wa 16 hivi « Mtawatambua kwa matunda yao »
Basi natujaribu kuliangalia andiko lingine jinsi gani twaweza kuwatambua,
1Yohana 4:1-3, 15
«Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.»
15 «Kila akiriye ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.»
Hiki ni kipimo tunachokitumia kuwapima mitume na manabii!
Mathayo 7:15-20
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.»
Hebu niseme hivi kulingana na tahazari ambayo Mungu ametupatia katika maandiko hayo mawili hapo juu:
‘Muhammad namlinganisha na mti, sasa matunda yake yakiwa mazuri sina ubishi nitamfuata, lakini yakiwa ni matunda kinyume na hayo nitamhesabu kama nabi iwa uongo’.
Je, katika Qurani Allah wa waislamu na Muhammad anasemaje?
Qr. 112 au surat Al-Ikhlas’
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.
Hakuzaa wala hakuzaliwa.
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.
Qr. 19 au surat Maryam 35
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanau, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
Huyu ni mungu tofauti na Mungu wa mbinguni ambaye jina lake ni Yehova! na tukilinganisha na yale maandiko ya Mathayo na waraka wa kwanza wa Yohana ukweli uko wazi kama huyu hatokani na Mungu na kwamba huyu ni Anti-Kristo! Kwani Biblia inasemaje ?
1Yohane 2:22-26,
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.
Na hii ndiyo ahadi aliyoyuahidia, yaani, uzima wa milele.
Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.
Wakolosai 1:13-15,
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Yohane 3:16-17,
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Kwa maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Kwahivi sisi wakristo tunazo sababu zaidi ya 100 kwanini hatumtambui mtume Muhammad, dini yake na mungu wake ambazo Mungu akituwezesha tutaziweka wazi moja kwa moja.
Ila hatuwezi kutosema hii moja ambayo ni hii:
Katika kitabu cha Qura’n tukufu kuanza na surat Al-Faatihah hadi surat Al-Nasmaandishi yake yanampinga Yehova Mungu wa israel.
CHIMBUKO NA UKOO WA UTUME NA UNABII WA MUHAMMAD
Kwanza kabisa, sote twajuwa kama kila mtoto huenda na kabila, lugha na mil aya babaake ila si ya mamaake. Hilo halina shaka hata kidogo!
Ibrahimu babaake Isaka na Ismail kabla aitwe na Mungu alikuwa ni mwarabu wa ki kurdi na baadaye Mungu aliyeviumba vyote akambadilisha na uzao wake wote baadaye ukawa ni waebrania.
Mwanzo 12:1-3
«Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.»
Lakini Muhammad, Qur’ani na wafuasi wake huzidi kuhakikisha kuwa Muhammad ni wa ukoo wa Ibrahimu wakati Ibrahimu si mwarabu tena!
Katika kitabu cha «maisha ya mtume Muhammad sw», twahakikishiwa kwamba Muhammad ni mwarabu wa kabila la Makureshi.
KUPEWA UTUME
Nilipokuwa nikichunguza kitabu cha historia ya Muhammad, kwa umri wake wa miaka 12 alikwenda na Abu Talib baba yake mdogo huko Shamu (Syria) kwa safari ya biashara, njiani wakakutana na mwanamume nabii wa kikristo ambaye jina lake alikuwa ni Bahirah naye akatowa unabii kuhusu Muhammad kwa maneno haya:
« Ewe Abu Talib;
Mtunze vema mtoto huyu kwa maana naona alama za umaarufu kwa mtoto huyu katika siku zake za usoni naye atapata kazi ya kumtumikia Mungu.»
Ni katika kitabu cha Maisha ya mtume Muhammad, ukurasa namba 4. Swali ni hili, lini nabii wa kikristo akatabiri uislam? Jibu ni hapana sababu neno la unabii kutoka kwa Mungu haliwezi kamwe kutabiri imani kinyume na Mungu na Kristo mwana wake wa pekee!
Mithali 8:7-9
«Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea Yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.»
2Petro 1:20-21
« Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.»
Tito 1:2
« katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu»
Kumbe ni wazi kwamba nabii huyu alikuwa na ujumbe muhimu kwamba siku moja Muhammad angalimtumikia Kristo Yesu na Ukristo lakini kwa bahati mbaya shetani akaubadilisha mwelekeo wa huyu maskini baadaye kama tutakavyoona katika wito wake.
Pangoni la Jabal Hira kaskazini mwa Mekka ndiko Muhammad alikuwa akienda kuabudu siku zote lakini alikuwa akimwabudu nani? Nakuomba tusome huu wito wake wa utume hapo chini.
USIKOSE SEHEMU YA PILI

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW