Wednesday, July 19, 2017

MUHAMMAD NA ALLAH WANADAI KUWA NYOTA HUINUKA NA KUKIMBIA

Image may contain: night, sky and text


Ndugu zanguni:
Ninapo sema kuwa, hii dini ni ya kutengeneza na ilitengenzwa na mtu asie na elimu hata ya chekechea mnafikiri natania?
Nyota ni nini?
Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisayansi imegunduliwa ya kwamba ni magimba makubwa sana katika anga la nje yanayong'aa kwa sababu yanatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za mnururisho kutokana na myeyungano ya kinyukilia ndani yake. Lakini ziko mbali sana na kwa hiyo tunaziona kama nukta ndogo za nuru. Kwa jumla nyota zinaonekana kwenye anga kwa mpangilio usiobadilika, na kila nyota huwa na mahali pake pasipobadilika kati ya nyota nyingine, hata kama nyota kwa jumla zinazunguka angani juu yetu kila siku.
Muhammad anadai kuwa, eti kuna nyota tano tu na zinainuka na kukimbia na kushindana na Mwezi na Jua.
Nabii [Muhammad] alijibu: ‘Ali, kuna nyota tano: Jupiter (al-birjis), Saturn (zuhal), Zebaki (utarid), Mars (Bahram), na Venus (al-zuhrah). Nyota hizi tano huinuka na kukimbia kama jua na mwezi na hushindana nazo pamoja. Nyota nyingine zote zimening’inizwa toka mbinguni kama taa zilivyoning’inizwa toka kwenye misikiti…" al-Tabari juzuu ya 1 uk.235-236.
Hivi mtu mwenye akili anaweza amini huu uongo na ukosefu wa elimu?
Eti, nyota zinaning'inia kama taa za kwenye Misikiti.
Nyota nyingi ni magimba kama jua letu maana masi kubwa ya gesi na utegili kwenye hali ya joto kali, ya sentigredi elfu kadhaa. Zinaonekana ndogo kwa sababu ya umbali wao.
Kornreich wanasema kuwa kuna angalau Nyota Trilioni 10 [10 trillion galaxies in the universe]. Unapo zidisha na [the Milky Way's] inakaribia nyota Bilioni 100 [estimated 100 billion stars results in a large number indeed]
1,000,000,000,000,000,000,000,000 stars, or a "1" yenye sifuri 24 mbele yake. Lakini Muhammad na Allah wanadai kuwa eti kuna nyota tano tu. https://www.space.com/26078-how-many-stars-are-there.html
Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kundi la namna hiyo huitwa galaksi. Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wa jua letu, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Tunaona sehemu za nyota zake angani zikionekana kama kanda la kung'aa linalojulikana kwa jina "njia nyeupe".
Maisha ya nyota:
Fizikia na astronomia zimegundua ya kwamba nyota hazidumu milele bali zina mwanzo na pia mwisho. Kutokana na tabia hii wataalamu mara nyingi huongea juu ya "maisha", "kuzaliwa" na "kufa" kwa nyota ingawa si viumbehai.
Je, tumwamini Allah na Muhammad wasio jua hata elimu ya nyota au tuamini elimu tulio nayo leo hii? Yaani binadamu wana akili zaidi ya Allah kuhusu elimu ya nyota kunamfanya Allah awe bandia na wa kutengenezwa tu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW