"Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee." Mithali 22:6
Mwenendo wenu ni fundisho kubwa kabisa mbele ya mtoto wenu. Njia ipasayo kumlea mtoto ni kuketi na mtoto na kumshauri maadili mema ya maisha (Kumbukumbu la Torati 6:7). Ni kumwelekeza kwenye mambo matakatifu, kabla hajaharibiwa na walimwengu.
Bibilia iko na mengi ya kusema kuhusu njia tunayoweza kuwalea watoto wetu wawe wanaume na wanawake wa Mungu. Kitu cha kwanza tunastahili kufanya ni kuwafunza ukweli kuhusu neno la Mungu.
Pamoja na kumpenda Mungu na kuwa mfano mwema kwa kujitoa sisi wenyewe kwa amri zake, tunastahili kuzitii amri za Kumbukumbu 6:7-9 kuhusu kuwafunza watoto wetu kufanya hivyo. Ufahamu huu unasisitiza jambo linaloendelea wa maelekezo hayo.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment