Friday, July 14, 2017

MAKKA NI MJI WA KIPAGANI WENYE MIUNGU NA MASANAMU 360


Image may contain: one or more people and text

Umeishawahi kujiuliza Makka ilikuwaje kabla Muhammad hajazaliwa?
Yaelekea ilikuwa sehemu ya kuvutia, kwani ilikuwa ni kituo cha biashara, mahali penye kusanyiko la tamaduni mbalimbali. Palikuwa na wafanya biashara wenye dini mbalimbali. Watu wa kabila la Kureshi wa Makka walimwabudu Hubal, Al-ilah na mabinti watatu wa Al- ilah. Mwamba mweusi kutoka mbinguni uliheshimiwa sana uliwekwa kwenye kona ya kaaba.
Kaaba ilikuwa ni kitovu cha kuabudia miungu/sanamu 360 kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 43 sura ya 33 na.658 uk. 396 na juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 47 na.583 uk. 406.
Ensaiklopidia ya Uislam (iliyohaririwa na Eliade) uk.303 na kuendelea inasema, watu, kabla ya Uislam, waliomba mara 5 wakielekeza nyuso zao Makka na kufunga nusu siku kwa muda wa mwezi mzima. Wakureshi walifunga siku ya 10 ya Myharram/Muharam. Hii nayo Muhammad aliagiza ifanyike, lakini baadaye ikawa hiari. (Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 25 na.172 uk.109), pia Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 24 na.31 uk. 25.
Waarabu kabla ya Uislam walifanya hija (Umrah) Maka. Fiqh us-Sunnah juzuu ya 5 uk.122, na Bukhari juzuu ya 2 kitabu 26 sura ya 33 na.635 uk.371-372 zinasema walidhani kutokufanya 'Umrah ikijuwa ni moja ya dhambi kubwa sana duniani. Walipofika Makka waliifunika kaaba kwa nguo ya Fiqh juzuu ya 5 uk.131, na walikuwa na mwezi mtakatifu uliohitaji kujitenga na vita kabla ya kuja kwa Uislam (Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 sura ya 96 na.482 uk.273.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW