Watu wa imani nyingine wamekuwa wakiwashutumu Wakristo na hata kuwaita makafiri kwa vile eti wanakula nyama ya Nguruwe, kwa madai kuwa eti imekatazwa katika maandiko matakatifu yaani Tourati na ikiwemo Quran.
Leo nataka kuanika wazi ili kama unakula mdudu huyu umle kwa amani bila kuhukumiwa au kushutumiwa na mtu.
Mafundisho ya Agano jipya kuhusu vyakula (Nguruwe).
Biblia inasema mafundisho yoyote yanayokataza mtu kula vitu Fulani ni mafundisho ya Mashetani (1Timotheo 4;1-5).
Ndio maana waganga wa kienyeji mtu anapokwenda kuaguliwa hukatazwa kula baadhi ya vitu Mungu sio Mganga wa kienyeji. Na wanaomwamini hawana sheria ya kuwazuia nini cha kula au kutokula.
Biblia inasema hakuna kitu najisi kwa mtu asiye najisi lakini kitu Fulani ni najisi kwake yeye aliye najisi (Rumi14;14).
Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula bali katika moyo safi (Mathayo 5;8).
Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)
Paulo mtume alifundisha kuwa chakula ni kwa tumbo tu na si mambo ya rohoni.
Paulo mtume alifundisha kuwa chakula ni kwa tumbo tu na si mambo ya rohoni.
(1Koritho 6;13).Hoja ya Pepo waliotolewa na Yesu kuwaingia nguruwe je ina maana gani?
Jambo lingine ambalo wanaharakati wa kiislamu hulishikia bango kuwa Nguruwe hawafai ni lile tendo la Pepo waliotolewa kwa mtu aliyeteseka kama kichaa kuomba ruhusa kuwaingia Nguruwe (Marko 5;12-13).
Kwa mujibu wa wachangiaji wa maoni ya kibiblia kama Mathew Henry commentary na wengineo hujaribu kutoa ufafanuzi huu kuhusia na na swala hili.
Nchi ya Wagerasi ilikuwa inakaliwa na Wayahudi wengi walioasi na kufuata mambo ya mataifa, swala la kufuga Nguruwe lisingeweza kufanywa na Wayahudi wa kawaida kwani kwao walikatazwa kula wanyama hao kwa mujibu wa sheria ya Musa.
Hivyo tendo la Yesu kuruhusu pepo kuingia Nguruwe kama walivyojiombea wenyewe lilikuwa ni sehemu ya hukumu kwao kwa kuishi kinyume cha sheria ya Musa, Jambo hili linathibitishwa na maombi ya mapepo “asiwapeleke nje ya nchi ile” maana yake kutokana na uasi uliokuwepo katika nchi ile mapepo bado yalikuwa na kazi katika mji ule, na hivyo waliomba wasihukumiwe kabla ya wakati wala wasifungwe kwani Kristo alikuwa na mamlaka hiyo.
Aidha inaonekana Tendo lile lilifanyika kwa kusudi la kuwafanya wachungaji wa Nguruwe kuingia mjini na kutoa taarifa kwa haraka watu wamtukuze Mungu na kama sehemu ya kutoa Hesabu ya mifugo kupotea hivyo kutokuwa na Kesi. Jambo hili liliwafanya Wagerasi waogope na kumsihi Yesu aondoke mipakani mwao.
Katika eneo hili pia tunaona jinsi thamani ya mwanadamu ilivyo bora nguruwe walikuwa wapata 2000 kwa sasa kilo ya nyama ya Nguruwe ni kati ya 6000/- kwa wastani chukua 6000 zidisha mara 100 yaani kilo za nguruwe mmoja mara 2000 idadi ya nguruwe woote utapata gharama ya 120,000,000/ yaani Bilioni moja na milioniishirini. Hasara waliyoipata wagerasi hailinganishwi na roho moja ya mtu anayepokea wokovu hivyo Kristo alitaka kuonyesha ni jinsi gani Roho ya Mtu ina thamani.
Jambo lingine ni kuonyesha wingi wa pepo ambao walijitaja kuwa ni jeshi legion kwa kawaida kikosi cha askari wa kirumi kilichoitwa legion kilibeba askari 6000 au zaidi.
Jambo lingine ni kuonyesha wingi wa pepo ambao walijitaja kuwa ni jeshi legion kwa kawaida kikosi cha askari wa kirumi kilichoitwa legion kilibeba askari 6000 au zaidi.
Pepo hao walikuwa ni wengi na isingeliwezekana watu kujua Mtu huyu anateswa na pepo wengi kiasi gani kama Masihi hangeuliza Maswali na pia kuruhusu Pepo hao kuingia Nguruwe, hii ilisaidia wanafunzi na jamii kujua ni wingi wa mapepo kiasi gani wakati mwingine hutesa watu.bKwa bahati nzuri pia Nguruwe hao walikufa baharini, hii haimaanishi kuwa Nguruwe woote wana mapepo.
Tendo la Masihi hapo halina uhusiano na kula au kutokula Nguruwe bali thamani ya mtu na mateso yanayotokana na Mshetani ambayo waislamu ni rafiki zao.
Kwa kuhitimisha nawaalika watu wote duniani msiwe na wasiwasi wa kula kiti moto na wanyama wengineo mnaojisikia kuwala Karibuni.
Shalom.
No comments:
Post a Comment