Friday, July 14, 2017

KWANINI TUNAKULA NGURUWE? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: one or more people and outdoor


Kiti moto mdudu mwenye mjadala mkali duniani.
Biblia inasema hivi katika Wakolosai 2 : 16 ‘Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;’ Kwa tafasiri nyepesi biblia inasema usimuache mtu yeyote akuhukumu ‘do not let anyone judge you’ kwa habari ya nunakula nini unakunywa nini, au kama huandami mwezi au kushika sabato mtu asikuhukumu, maana yake ni kuwa mafundisho yoyote duniani ya imani yoyote yanayokataza ule nini usile nini ni mafundisho ya Mashetani, sisi wakristo hatuna miiko, ukienda kwa wapunga pepo wanganga watakupangia ule nini usile nini haya ni mafundisho ya mashetani ona 1Timotheo 4 1-5 Biblia inasema :-
1. Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2. kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3. wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 4. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5. kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.’
Ndugu zangu unaweza kuona maandiko haya yako wazi kabisa kwamba kumzuia mtu ajiepushe na chakula fulani ni mafundisho ya roho zidanganyazo yaani mapepo na mashetani biblia iko wazi kuwa kila kiumbe kilichoumbwa na Mungu ni kizuri kama ukikipkea kwa shukurani kwa vile vimeatakaswa na neno la Mungu !
Wakati najenga Msingi huu napenda pia nikufahamishe vema somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo :-
Ufahamu kuhusu Nyakati saba za Maongozi ya Mungu.
Mafundisho ya Quran kuhusu Nyama ya Nguruwe.
Mafundisho ya Agano jipya kuhusu kula Nguruwe.
Ufahamu kuhusu nyakati saba za maongozi ya Mungu.
Moja ya sababu zinazopelekeabaadhi ya watu kupinga aina Fulani ya vyakula ikiwemo nyama ya nguruwe ni kuto kuyajua maandiko na kutofahamu juu ya nyakati saba za Maongozi ya Mungu ambapo Mungu aliongoza kwa Sheria tofauti tofauti, ikumbukwe kuwa Mungu ndie mtunga sheria na huweza kupanga au kupangua sheria “Amendments” kulingana na nyakati Yeye mwenyewe, kama apendavyo, Kama bunge linavyoweza kupitisha sheria na hatimaye kuibadili wakati Fulani kama wapendavyo ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, Mungu ameiongoza Dunia hii kwa nyakati tofauti tofauti zipatazo saba, maeneo sita kati yake yametimizwa na eneo la saba litakuwa ni wakati ujao
Nyakati za Maongozi ya Mungu kibiblia Zimegawanyika katika Maeneo makuu saba yafuatayo
Innocence Period-Hiki ni kipindi cha uumbaji mpaka anguko la Adamu(mwanadamu)
Concience Period-Hiki ni kipindi cha dhamiri mpaka gharika
Human Government Period-Hiki ni kipindi cha kujitawala mpaka wakati wa Ibrahimu
Promise au Patriach Period-Hiki ni kipindi cha mababa mpaka wakati wa Musa.
Dispensation of Law- hiki ni kipindi cha sheria ya Musa.
Dispensation of Grace-Hiki ni kipindi cha neema au wakati wa Mataifa.
Escatological times-Kipindi cha mambo yajayo (Dhiki kuu, hukumu ya mataifa, utawala wa miaka 1000,vita ya gogu na magogu, ziwa la moto, Mbingu mpya na nchi mpya.)
Katika vipindi hivi vyoote Mungu aliweka sheria mbalimbali za kuongoza vipindi hivyo,Mtu asipofahamu vizuri anaweza kuchanganya mambo katika vipindi hivyo Mungu aliweka au kubadili sheria zake kulingana na nyakati hizo na makusudi yake aliyoyakusudia kwa wakati huo.
Mfano sheria kuhusu Vyakula;-
Kipindi cha uumbaji mpaka anguko la Adamu (Innocence Period).
Sheria ilikuwa moja tu wasile tunda la ujuzi wa mema na mabaya tu wakati huu mwanadamu hakula nyama (Mwanzo 2;16-17,1;28-30) Mungu aliweka sheria hii moja kwa sababu Adamu na Eva walikuwa Peke yao na Mungu aliwapa vitu vyote hebu jaribu kuwaza kama Mungu angesema Usizini, usiibe hizo sheria pale Bustanini zingemuhusu nani wakati Adam yuko peke yake na mkewe
Kipindi cha dhamiri Anguko mpaka wakati wa gharika Gharika (Concience period.)
Wakati huu Mungu aliamuru wale vitu vyoote isipokuwa Damu tu (Mwanzo 9;1-4).Baada ya gharika Mungu alimruhusu Nabii Nuhu na wanawe kula kila kitu yaani vitu vyote isipokuwa Damu tu yaani lazima damu ya mnyama imwagike unapotaka kumla, soma biblia yako Mwanzo 9: 1-4 waliruhusiwa kula kila kitu yaani vyote akiwemo Yule mdudu Nguruwe!
Wakati wa sheria ya Musa (Mungu aliamuru wale baadhi ya vitu na baadhi vilikatazwa).
hii ilikuwa ni kwa sababu za kiafya na kutafuta utii wa Israel, baadhi ya vitu vilivyokatazwa ni pamoja na Ngamia, Sungura, Nguruwe, Kambale, Taa, Pweza, Ngisi, n.k. Mungu aliwakataza WAYAHUDI peke yao wasile baadhi ya wanyama na samaki wote wasio na Magamba na wanyama wasio na kwato zilizopasuliwa kati, au wenye kwato zilizopasuliwa kati lakini hawacheui soma (Walawi 11;1-47).
Wakati wa Neema,
Wakati huu Mungu aliamuru kuliwa kwa vitu vyoote isipokuwa damu ambayo kibiblia imekatazwa milele. ( Luka 17;10,1Koritho 10;25-27,Kolosai 2;16,1Timotheo 4;1-5). Wakati wa neema ndio wakati huu wa agano jipya wakati huu tunaruhusiwa kula kila kitu bila kujali wala kuulizauliza soma maandiko yale juu.
Tatizo kubwa la waislamu ni kutokujua nyakati hizi za maongozi ya Mungu na Sheria alizoweka, wanachanganya mambo.
Aidha katika namna ya kushangaza waislamu wanaona Nguruwe tu kuwa ni haramu, huku wamesahau kuwa Mungu alikataza hata ngamia ambao mara nyingi huchinjwa na waislamu wakati wa iddi alhaji. wavuvi wengi wa pwani ni waislamu mara nyingi huvua taa, pweza na ngisi, Mtu anayeamua kuishika sheria na ashike yoote na asiyedumu katika yoote amelaaniwa (Galatia 3;10). Wanyama wengi miongoni mwa waliokatazwa wanahitilafu za kiafya kama wasipoandaliwa vema mfano Nguruwe ana tegu wengi katika nyama yake pia huharibika kwa Haraka nyama yake inapokaa zaidi ya wakati hivyo kutokana na mazingira ya jangwani walikokuwa wanasafiri Israel isingelikuwa vema kuruhusiwa kutumia aina hizi za nyama. Mungu aliwapa sheria hii Wayahudi peke yao wakiwa chini ya nabii Musa. Baada ya kuyaelewa haya sasa hebu tuangalie Mafundisho ya Quran kuhusu Nguruwe!
=====> USIKOSE SEHEMU YA TATU..........
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW