Saturday, July 15, 2017

MITUME 12 WA ISA BIN MARYAM NI AKINA NANI?


Image may contain: 8 people, people smiling, text

KAMA ISA BIN MARYAM ALIKUWA YESU, TUAMBIENI MAJINA YA MITUME WAKE KUMI NA WAWILI

NDIO MAANA ISA BIN MARYAM HAWEZI KUWA YESU KRISTO

Biblia na Ukristo ulio kuwepo miaka 600 kabla ya Uislam, Muhammad, na Quran inasema hivi:
Mitume halisi kumi na wawili wameoredheshwa katika Mathayo 10:2-4, “Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya;

Neno “mtume” lamaanisha mwanafunzi au mfuasi. Neno “mtume” la maanisha “mtu aliyetumwa nche.” Huku Yesu akiwa ulimwenguni, wafuasi wake kumi na wawili waliitwa mitume. Mitume kumi na wawili walimfuata Yesu Kristo, wakajifunza kutoka kwake, na wakaelimishwa naye.
Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo; Simoni mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti.”

Bibilia pia yaorodhesha hao mitume kumi na wawili katika Mariko 3:16-19 na Luka 6:13-16. Linganisho la fahamu hizi tatu laonyesha tofauti chache katika majina. Inaonekana Thadayo pia aliitwa “Yuda, mwana wa Yakobo” (Luka 6:16) na Lebayo (Mathayo 10:3). Simoni mfarisayo pia aliitwa Simoni Mkananayo (Mariko 3:18). Yuda Iskariote ambaye alimsaliti Yesu, nafasi yake ilichukuliwa na Mathiya (angalia Matendo Ya Mitume 1:20-26). Walimu wengine wa Bibilia wanamwona Mathiya kama mtume ambaye “hastahili” na wanaamini kuwa Paulo alikuwa chaguo la Mungu kumpadilisha na Yuda Iskariote kama mtume wa kumi na mibili.

Sasa basi, tunawaomba Waislam watuletee majina 12 ya Mitume wa Isa Bin Maryam ili tukubalia kuwa Isa Bin Maryam ni Yesu Kristo..

Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW