SEHEMU YA KWANZA
Watu wengi wamesema kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na mke wake mwenye umri mdogo zaidi, A’isha, binti wa Abu Bakr, alipokuwa na miaka karibu 53 na [A’isha] alikuwa na miaka tisa. Baadhi ya Waislam wanakataa maneno haya. Kama mtu atadai kuwa Muhammad na A’isha walijamiiana wakati A’isha alipokuwa na umri wa miaka tisa, na walifanya makosa, jambo hili litakuwa ni kashfa kubwa sana kwa Muhammad. Kwa upande mwingine, kama ilikuwa kweli, jambo hili litaonyesha sura tofauti kabisa ya Muhammad itakayo washtua watu wengi. Kwa hiyo basi, madai haya dhidi ya Muhammad ni ya kweli au uongo?
Andiko hili litaanza kwa kutoa ushahidi wa A’isha kuwa na miaka tisa wakati ndoa yake ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba, kisha litatoa vipingamizi 11 dhidi ya jambo hili, na mwishoni, litauliza itakuwa vipi endapo kila wazo lilikuwa sahihi.
Jambo hili ni la muhimu kwa desturi iliyotumika sehemu nyingi sana lakini ambayo imepuuzwa sana siku za leo: mabibi arusi watoto kwenye nchi za Kiislam waliotokana na mfano wa Muhammad.
Huko Iran, hadi kufikia Juni 2002 iliruhusiwa kisheria kwa msichana wa miaka 9 kuolewa kwa ruhusa ya wazazi. Voices Behind the Veil (Sauti Ttokea Nyuma ya Mtando) uk.136-137.
Huko Ivory Coast kitabu hiki pia kinatuambia kuhusu msichana wa miaka 12 ambaye alikuwa anaondoka nyumbani asubuhi kwa masaa mengi kabla ya kurudi nyumbani. Baada ya baba yake kumfunga, alimuunguza kwa kipande cha chuma, alimfungia kwa muda wa siku tatu bila chakula, hatimaye almwoza kwa mwanaume wa miaka 40. Hakuwahi kumpeleka shule kwa sababu alisema kuwa jambo hilo litawaondoa kwenye desturi zao, (mabinti) wataanza kuuliza maswali, na kutokupenda kuolewa mpaka wafikishe umri wa maka 19 au 20.
Wataliban walizishawishi familia zao kuoza mabinti wao wakiwa na umri mdogo hata miaka nane. Voices Behind the Veil uk.110.
Gazeti la Dallas Morning News 9/28/03 uk.1,10S lilikuwa na habari ya kusikitisha kuhusu tabu ya wasichana wa Kiislam wa Nigeria ambao waliolewa wakiwa na umri mdogo sana, walipata ujauzito na walipopata uchungu wa uzazi miili yao midogo ilikuwa bado haijawa tayari. Kwa kiasi kikubwa habari hii ilikuwa mbaya, kimsingi wengi wa wasichana hao walihitaji kuzaa kwa upasuaji (C-section) lakini hawakuweza kupata huduma hiyo. Wengi wao walinusurika, lakini hawakuweza kupata watoto tena kwa sababu ya kuharibiwa kwa miji ya mimba.

Ili kuelewa asili ya mamlaka ya mfano wa Muhammad, ni muhimu tufahamu jambo moja kuhusu Hadithi za Kiislam. Hadithi zina nafasi ya juu sana katika madhehebu ya Suni kuliko mapokeo yalivyo na nafasi kwenye makanisa ya Katoliki na Orthodox. Waislam wa madhehebu ya Suni wanaamini kuwa mikusanyiko sita ya Hadithi ndiyo yenye mamlaka kubwa zaidi kwenye Uislam baada ya Kurani. Sehemu iliyobaki ya andiko hili inaonyesha kuwa dai hili ni la kweli kabisa, kwa mujibu wa vyanzo vingi vya awali vya Kiislam vyenye kuunga mkono. Pamoja na nukuu hizi toka kwenye Hadithi sita zinazoaminika ni nukuu toka kwa wana historia wa zamani wa Kiislam wanaoheshimika sana ibn Ishaq na al-Tabari.
1. Sahih al-Bukhari 810-870 BK, 256 BH
1a. "Alisimulia baba wa Hisham: Khadija alkufa miaka mitatu kabla ya Nabii kuondoka Madina. Alikaa huko miaka miwili au zaidi kisha akamuoa ‘Aisha alipokuwa msichana mwenye umri wa miaka sita, na Muhammad aliikamilisha ndoa yao kwa tendo la unyumba wakati ‘Aisha alipokuwa na umri wa miaka tisa." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 43 na.236, uk.153.

1b. Habari hizo zipo pia kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 43 na.234, uk.152.
1c. "Alisimulia ‘Urwa: Nabii aliandika (mkataba wa ndoa) na ‘Aisha wakati msichana alipokuwa na umri wa miaka sita na aliikamilisha ndoa yake nay eye kwa tendo la unyumba wakati akiwa na miaka tisa na ‘Aisha aliendelea kuwa naye kwa miaka tisa (yaani mpaka kifo cha Nabii). Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 sura ya 60 na.88, uk.65.
1d. Alisimulia ‘Aisha: Nabii alikuwa akinisitiri kwa Rida (vazi lenye kukinga sehemu ya juu ya mwili) yake nilipokuwa nawaangalia Waethiopia waliokuwa wanacheza kwenye ua wa nyuma wa msikiti. (Niliendelea kuangalia) hadi nilipotosheka. Hivyo unaweza kuelewa ni jinsi gani binti mdogo (ambaye hajafikia umri wa kuvunja ungo) ambaye ana hamu ya kufurahia burudani alivyofanyiwa mambo ya namna hii. Bukhari juzuu ya7 kitabu cha 62 sura ya 115 na.163, uk.119.
1e. "Alisimulia ‘Aisha: (mke wa Nabii) sikumbuki kama wazazi wangu waliamini dini yoyote ile isipokuwa dini ya kweli (yaani Uislam), na (sikumbuki) siku yoyote iliyopita bila sisi kutembelewa na Mtume wa Allah asubuhi na jioni." Bukharijuzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 4 na.245, uk.158. Kwa hiyo, ‘Aisha ama hakuwa mkubwa ama hakuwa amezaliwa kabisa wakati wazazi wake walipo badili dini na kuwa Waislam. Jambo hili linaendana na yeye kuwa mtoto wakati ndoa yake na Muhammad ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba.
2. Sahih Muslim 817-875 BK, 261 BH
Mkusanyiko huu unachukuliwa kuwa wa pili wenye kuaminika zaidi miongoni mwa Hadithi.
Mkusanyiko huu unachukuliwa kuwa wa pili wenye kuaminika zaidi miongoni mwa Hadithi.
2a. "(3309) A’isha (Allah na apendezwe naye) aliripoti: Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka sita, na niliingizwa nyumbani mwake nikiwa na miaka tisa. (A’isha) Aliendelea kusema: Tulikwenda Madina na nilishikwa na homa kwa muda wa mwezi mmoja, na nywele zangu zilianguka hadi kwenye ndewe (masikioni). Umm Ruman (mama yangu) alikuja kwangu na wakati huo nilikuwa kwenye bembea pamoja na wenzangu ninaocheza nao. Mama aliniita kwa sauti na nilikwenda kwake na sikujua kwa nini aliniita. Alinishika mkono na kunipeleka mlangoni, na nilikuwa ninasema: Ha, ha (kana kwamba nilikuwa natweta kwa mshangao), mpaka msukosuko wa moyo ulipomalizika. Alinipeleka kwenye nyumba ambako walikuwa wamekusanyika wanawake wa the Ansar. Walinibariki na kunitakia bahati njema na kusema: Uwe na sehemu katika mambo mazuri. Mama alinikabidhi kwao. Waliniosha kichwa changu na kuniremba na hapakuwa na kitu kilichonitisha. Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) alikuja pale asubuhi, na nilikabidhiwa kwake." Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 sura ya 548 na.3309, uk.715-716.
2b. "(3310) A’isha (Allah na apendezwe naye) aliripoti: Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka sita, na niliingizwa kwenye nyumba yake nilipokuwa na miaka tisa."
(3311) A’isha (Allah na apendezwe naye) aliripoti kuwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alimuoa alipokuwa na miaka saba, na alipelekwa kwenye nyumba yake (Mtume) kama bibi arusi alipokuwa na miaka tisa, na hapa midoli (wanasesere) yalikuwa pamoja naye: na (Nabii Mtakatifu) alipokufa ‘Aisha alikuwa na miaka kumi na nane." Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 sura ya 548 na.3310, 3311, uk.716.

2c. "(5981) A’isha aliripoti kuwa alizoea kuchezea midoli mbele ya Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) na wenzake aliokuwa akicheza nao walipokuja (nyumbani) kwake waliondoka kwa sababu walimwonea aibu Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake), lakini Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) aliwatuma kwake (A’isha).
2d. (5982) Hadithi hii imesimuliwa kwa mamlaka ya Hisham ikiwa na mlolongo ule ule wa waenezaji huku ikiwa na utofauti kidogo wa maneno." Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 29 sura ya 1005 na.5981-5982, uk.1299.
3. Sunan Abu Dawud 817-888/9 BK, 275 BH
3a. "(2116) A’isha alisema: Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka saba. Msimuliaji Sulaiman alisema: Au miaks sita. Mtume alifanya nami tendo la unyumba nilipokuwa na miaka tisa." Sunan Abu Dawudjuzuu ya 2 kitabu cha 5 sura ya 700 na.2116, uk.569.

3b. "(4913) A’isha alisema: Nilizoea kuchzea midoli. Nyakati zingine Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) aliniingilia wakati wasichana walikuwa pamoja nami. Alipoingia (ndani ya nyumba) walitoka nje, na alipotoka nje waliingia ndani."Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1769 na.4913, uk.1373.
Angalia kwa ungalifu. Hii haimaanishi kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na A’isha wakati wenzake aliokuwa akicheza nao wakiangalia. Badala yake inamaanisha kuwa wenzake walicheza naye, na walienda nje wakati Muhammad alipokuja, na walirudi baada ya Muhammad kuondoka.
3c. "(4915) A’isha alisema: Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka saba au sita. Tulipokuja Madina, baadhi ya wanawake walikuja. Kwa mujibu wa maelezo ya Bishr: Umm Ruman alikuja kwangu nilipokuwa nabembea. Walinichukua, walinitayarisha na kunipamba. Baada ya hapo nilipelekwa kwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake), na alinichukua na kuanza kuishi nami kinyumba nilipokuwa na miaka tisa. (Umm) alinivutia mlangoni na niliangua kicheko.
Abu Dawud alisema: Hii ndio kusema: Nilipata siku za mwezi, na nililetwa kwenye nyumba, na kulikuwa na wanawake kadhaa wa Ansari (Wasaidizi) ndani yake. Walisema: Kwa bahati nzuri na baraka. Masimulizi ya baadhi yao yamejumuishwa na mengine. Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4915, uk.1374.

3d. (5916) [kosa la uchapaji, namba sahihi ni 4916]. Masimulizi yaliyotajwa hapo juu yalienezwa pia na Abu Usamah kwa namna kama hii hii kupitia mlolongo wa wasimulizi tofauti. Maelezo haya yanasema: ‘Kwa bahati nzuri.’ (Umm Ruman) alinikabidhi kwao. Waliniosha kichwa changu na kunivisha upya. Hakuna mtu aliyekuja kwangu mara moja isipokuwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) mchana wa kabla ya saa sita. Hivyo walinikabidhi kwake. Sunan Abu Dawudjuzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4916, uk.1374.
3e. (4917) A’isha alisema: Tulipokuja Madina, wanawake walikuja kwangu wakati nilipokuwa nacheza kwenye bembea, na nywele zangu zilifika kwenye masikio. Waliniletea, wakaniandaa na kunipamba. Kisha wakanipeleka kwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) na alinichukua na kuishi nami kinyumba, nilipokuwa na umri wa miaka tisa. Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4917, uk.1374.
3f. (4918) Masimulizi yaliyoelezwa hapo juu yalienezwa pia na Hisham b. ‘Urwah kupitia kwenye mlolongo wa asimlizi tofauti. Maelezo haya yanasema pia: Nilikuwa nabembea na nilikuwa na marafiki zangu. Walinichukua na kunipeleka kwenye nyumba; kulikuwa na wanawake kadhaa wa Ansar (Wasaidizi). Walisema: Kwa bahati njema na baraka. Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4918, uk.1374.
3g. (4919) A’isha alisema: Tulifika Madina na kuishi na Banu al-Harith b. al-Khazraj. Alisema: Naapa kwa Allah, nilikuwa nabembea kati ya mitende miwili. Kisha mama yangu alikuja, na aliniambia nishuke chini; na nywele zangu zilifika kwenye masikio. Kisha muenezaji anasmulia masimulizi yaliyobaki." Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4915-4919, uk.1374.
Hitimisho kuhusu Abu Dawud: nukuu na nukuu zinazopinga nukuu 7 zinathibitisha kuwa A’isha alikuwa na miaka tisa.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
No comments:
Post a Comment