Sunday, June 18, 2017

YESU ALISEMA NINI KUHUSU ROHO MTAKATIFU NA MAREHEMU MUHAMMAD?

Image may contain: sky, cloud, ocean, nature, text and outdoor
1. Roho Mtakatifu atakuja kwa Jina lake.
2. Roho Mtakatifu anajua yote.
3. Roho Mtakatifu atakaa ndani yetu.
4. Roho Mtakatifu anamtukuza Yesu.
Neno la Mungu linasema kuwa, Roho Mtakatifu alikuja kwa Jina la Yesu.
1. ROHO MTAKATIFU ALIKUJA KWA JINA LA YESU:
UTHIBITISHO: - Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
MUHAMMAD ALIPEWA UTUME NA MKEWE:
Kiitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
2. ROHO MTAKATIFU ANAJUA YOTE NA ATATUFUNDISHA KUHUSU YESU KRISTO:
Anafundisha yooote ambayo Yesu aliwaambia mitume wake.- Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
MUHAMMAD HAKUJUA YOTE BALI ALIKIRI KUWA YEYE NI KIROJA.
Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
3. ROHO MTAKATIFU ALIKAA NDANI YA WANAFUNZI WA YESU
Yohana 14:17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
MUHAMMAD HAKUWEPO WAKATI WA YESU NA HAKUWA NA UWEZO WA KUKAA NDANI YETU KAMA ROHO MTAKATIFU.
4. ROHO MTAKATIFU ANAMTUKUZA YESU KRISTO:
Yohana 16:14 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
MUHAMMAD HAKUMTUKUZA YESU BALI ALLAH, HIVYO HAWEZI KUWA ROHO MTAKATIFU BALI ALIMKUFURU ROHO MTAKATIFU.
Walio mkufuru Roho Mtakatifu wote wataingia Jehannam.
5. YESU ANAWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE
Yohana 20 aya ya 21 na 22 inasema: 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
AYA HAPO JUU IPO WAZI kabisa kuwa YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE NA HAKUWAPA MUHAMMAD AMBAYE alikuwa bado HAJAZALIWA.
Nimevunja hoja dhaifu za Wakufuru Roho Mtakatifu kwa kutumia aya thabiti za Biblia Takatifu.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW