Wednesday, June 7, 2017

WARUHUSU MALAIKA WA VITA

Image may contain: text
Katika jina lenye nguvu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi. Ninaruhusu Malaika wa vita kutoka Ufalme wa Mungu ninawaamuru enyi wote kukaa kwenye nafasi zenu dhidi ya shetani na mapepo yote, sambaeni kila mahali sasa, mjieneze katika Anga, Nchi na Bahari, muangamize nguvu zote za giza katika Anga, Nchi na Bahari, muangamize nguvu za giza katika anga za nchi kavu na baharini mpige shetani bila kukoma, haribuni mipango yote waliyoifanya dhidi yangu. Ninawamuru enyi malaika na Bwana mnizunguke kama wigo sasa. Mnizunguke mimi katika jina la Yesu Kristo-Amen.
Mathayo 26: 53 “Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?”
Luka2: 13 “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,”
Mwanzo 32: 1 “1 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu. Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.”
Zaburi 148: 2 “Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.”
Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,”
"Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi. Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado." Daniel 10: 12
USICHOKE KUOMBA KILA SIKU.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW