Warumi 10:17 16 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. 17 Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Kumbuka kipaumbele cha Yesu hapa kwa wanafunzi wake kilikua ni kiwango cha Imani ila kwa upande mwingine kipaumbele cha shetani ni kiwango cha hofu uliyonayo.Ni mambo yanayoenda sambamba lakini hayafanani.
WOGA UNAMPA SHETANI NAFASI YA KUFANYA KAZI ZAKE NDANI YAKO KWA UHURU WA KUKUTAWALA NA KUKUFANYIA ANACHOTAKA.
VUNJA VIFUNGO VYA HOFU
Tambua kuwa hofu huleta vifungo.Pindi roho ya hofu inapoweka mizizi moyoni mwako unakuwa mtumwa na mfungwa wa hofu.Hii ni kanuni halisi ambayo inaonekana kabisa kwenye kitabu cha Waebrania
Waebrania 2:14-15 14 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 15 Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
No comments:
Post a Comment