Sunday, June 18, 2017

MUNGU ROHO MTAKATIFU ANAISHI NDANI YETU

Image may contain: one or more people and text
Ezekieli 36:27 “nami nitatia roho yangu ndani yenu na kuwaendesha katika sheria zangu nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda” maneno haya anayasema MUNGU kupitia kinywa cha nabii Ezekieli.
Ni Mungu aangaliae yote Zaburi 139:7 inasema “niende wapi njiepushe na Roho yako, Niende wapi niukimbie uso wako”
Ni maombi yangu Zaburi 51:11-12 inayosema “usinitenge na uso wako wala Roho Mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wokovu wako ,unitegemeze kwa Roho ya wepesi wako” yatimie kwako.
Katika Kumbukumbu la Torati anasema hivi Kumbukumbu la Torati 4:6 anasema “sikiza ee izraeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja” MUNGU ni mmoja anaposema nitatia roho yangu ndani yenu (yetu) maana yake Mungu kuja kukaa ndani yetu kupitia ROHO MTAKATIFU,
Biblia katika ule Waraka kwanza wa Yohana 4:8-9 anasema “kwa maana wako watatu washuhudiao[mbinguni Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu na hawa watatu ni umoja 9 kisha wako watatu washuhudiao duniani] Roho, na maji, na damu; na hawa hupatana kwa habari moja.tukipokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwanawe. Mungu mmoja aliye ziumba mbingu na nchi yeye Mungu na Roho Mtakatifu na Neno (Yesu) mbinguni ni umoja na duniani wako watatu wanaopatana kwa habari mmoja.
Watatu duniani Biblia inasema ni Roho Mtakatifu (Mungu pamoja nasi), Maji, na Damu. Kwa habari ya maji Biblia inasema hivi “Ezekieli 36:25 nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote” anaeleza habari ya utakaso. Damu ya YESU ndio ukombozi na upatanisho wetu ili tumwone Mungu.
ROHO MTAKATIFU ndiye aliyekuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake; Luka Mtakatifu anasema Luka 1:35 “Malaika kajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu MWANA WA MUNGU”
Maneno haya aliyasema Malaika Gabrieli alipokuwa akimweleza Mariamu juu ya kuzaliwa Yesu na matokeo yake ilikuwa hivi “Mathayo 1:18 “kabla hawajakaribiana alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”.
Yesu ni Mungu na katika kitabu cha Waebrania anasema Waebrania 1:8 “lakini kwa habari ya mwana asema kiti chako cha enzi Mungu ni cha milele na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili”
Si wanadamu tu waliokili kuwa yesu ni mungu bali hata malaika waliotumwa na mungu walikiri kuwa yesu ni mungu “Luka 1:32-33 huyo atakuwa mkuu ataitwa mwana wa aliye juu, Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake, ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” na tunajua ufalme wa mungu pekee ndio hauna mwisho na kupitia Yesu atamiliki nyumba ya Yakobo milele na milele. twaweza sema kwamba ufalme wake hauna mwisho kwa sababu yeye ni Mungu wa milele.
Matendo ya Mitume 1:8 Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa “mtapokea nguvu akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wan chi”
Tangu siku za yohana ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu tena nguvu za rohoni (nguvu za ROHO Mtakatifu) unapomwamini Yesu Roho Mtakatifu
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW