Wednesday, June 7, 2017

JE, UNAMFAHAMU MALAIKA ANAYEWEZA KUFUNGUA MILANGO YAKO?

Image may contain: one or more people and text
Malaika wako na hekima (Mathayo 8:29; 2 Wakorintho 11:3; 1 Petero 1:12), inaonyesha hisia (Luka 2:13; Yakobo 2:19; Ufunuo 12:17), na kujaribu kufanya penzi lao (Luka 8:28-31; 2 Timotheo 2:26; Yuda 6). Malaika ni viumbe vya kiroho (Waebrania 1:14) bila na kuwa na mwili. Ingawa hawana mwili, bado wako na hali ya mwili.
Kutoka 23:20-22 "Tazama, mimi namtuma Malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. 21. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe Makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 22. Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao."
Matendo ya Mitume 5: 19 “lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,”
Malaika wanaleta majibu ya maombi (Matendo Ya Mitume 12:5-10).
Huyu Malaika ameenda mpaka gerezani akawatoa watu wa Mungu gerezani. Tunajifunza wakati wa kwenye maombi unaweza kumtuma malaika huyu aende akafungue milango ya biashara iliyofunga, ndoa illiyofunga, kazi, milango ya kupata kiwanja, milango ya kupata visa, milango ya promotion iliyofunga na akaenda kufungua milango uliokwama kwa damu ya Yesu. Watu wa duniani kwenye Ufalme wao huenda kwa waganga wa kienyeji lakini sisi Mungu wa Ufalme wetu anazo nguvu nyingi kuliko mungu wao na tunaweza kutenda mambo makubwa kuliko wao.
Unapowatumia malaika fahamu kwamba wana lugha zao ambazo ni Biblia(katiba) ambayo ni Neno la Mungu na kunena kwa lugha(lugha ya Ufalme), unapomtuma Malaika uwe unataja sheria inayomhusu kwenye Biblia na uombe.
Mfano Unatakiwa useme:-
“Baba Mungu katika jina la Yesu imeandikwa kwenye sheria ya Matendo ya mitume 5:19 sheria ya kumtuma malaika mwenye uwezo wa kufungua milango yeye aliyeifungua milango ya gereza la akina Paulo aende akafungue mlango ya magonjwa ulionishikilia, biashara yangu iliyofunga, milango ya safari iliyofunga ifunguke kwa jina la Yesu Amina.” Unaomba na kutaja maeneo uliyofungwa na Fahamu kuwa malaika huyu atatenda sawasawa na maneno yako.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW