Friday, June 9, 2017

JE! BIBLIA NI MANENO YA MUNGU?

Image may contain: one or more people
Hili ni swali ambalo huulizwa sana na marafiki zangu waislamu, wakitaka waoneshwe neno BIBLIA kwenye maandiko yaliyomo ndani ya BIBLIA, maana wamesoma Biblia ya Kiswahili, hawajaliona ndani, wakasoma Bible napo neno BIBLIA hawakuliona, kwa hivyo mashaka yakawaingia, wakaona BIBLIA ni Title tu ya nje ndani haimo.
roho hiyo ikawavaa Jamaa zangu wa Siloamu, bila kufanya utafiti wa kina wakakurupuka na kuchana ganda la juu lililoandikwa 'BIBLIA' Walileta madai hayo hayo ya Waislamu kwamba ndani ya maandiko neno BIBLIA hakuna.
Leo imempendeza Mungu niwaletee somo hili ili kuwafumbua macho watu wasiojua waweze kuelewa kuwa BIBLIA ni maneno hakika ya Mungu muumba wa mbingu na aridhi.
NENO BIBLIA: siyo neno la lugha ya kiswahili wala kingereza, ndiyo maana wanaosoma BIBLIA ya kiswahili, na BIBLE ya kingereza neno hilo hawalikuti ndani ya maandiko, kwa kuwa ni neno la lugha ya kiyunani Greak language...
Kama Waislamu na Wafuasi wa Siloamu wangesoma Biblia ya lugha ya kiyunani basi wasingepata tabu wala swali hilo wasingeuliza tena, maana humo limo kwani NENO BIBLIA kwa kiswahili ni mkusanyiko wa Vitabu, in English books.
Daniel 9: 2 In the first year of his reign I Daniel understood by books the number of the years, whereof the word of the LORD came to Jeremiah the prophet, that he would accomplish seventy years in the desolations of Jerusalem.
Hapo Daniel alisoma vitabu vya Mungu na kujua mwaka ambao neno la MUngu lilimjia Yeremia. hapo kumetajwa books (Vitabu vya MUNGU)
Ukisoma kwenye kiyunani unakutana na BIBLIA (βιβλία) kama kuna mwenye kujua kiyunani asome hapa.
Daniel 9: 2 κατά τον πρώτο χρόνο τής βασιλείας του, εγώ ο Δανιήλ εννόησα μέσα στα βιβλία τον αριθμό των χρόνων, για τους οποίους έγινε ο λόγος τού Κυρίου στον προφήτη Ιερεμία, ότι θα συμπληρώνονταν 70 χρόνια στις ε
Humo ukiingia neno BIBLIA unalikuta, kwa sababu wao wayunani Vitabu, wanaviita βιβλία, (BIBLIA)
Na kitabu kimoja wanakiita Biblos (βιβλιου)
Ukisoma kitabu cha ufunuo 22:18-19 Utakutana na onyo kwa watu wasiongoze wala kupunguza maneno yaliyomo kwenye kitabu hicho cha unabii, kwani atakaeongeza ataongezewa mapigo yaliyoandikwa kwenye kitabu hicho..... sasa hapo kwenye kiswahili kuna kitabu, kwenye Biblia ya Kiyunani utakuta neno BIBLOS.
Ufunuo 22: 18 συμμαρτυρουμαι γαρ παντι ακουοντι τους λογους της προφητειας του βιβλιου τουτου εαν τις επιτιθη προς ταυτα επιθησει ο θεος επ αυτον τας πληγας τας γεγραμμενας εν βιβλιω τουτω
19 και εαν τις αφαιρη απο των λογων βιβλου της προφητειας ταυτης αφαιρησει ο θεος το μερος αυτου απο βιβλου της ζωης και εκ της πολεως της αγιας και των γεγραμμενων εν βιβλιω τουτω.
Kingereza utakuta Book, swahili Kitabu, kwa kiyunani βιβλου, sasa ngoja tuiangazie BIBLE.
Revelation 22:18 For I testify unto every man that heareth the words of the prophecy of this book, If any man shall add unto these things, God shall add unto him the plagues that are written in this book:
19 And if any man shall take away from the words of the book of this prophecy, God shall take away his part out of the book of life, and out of the holy city, and from the things which are written in this book.
Tena hata vitabu vya Mungu ambavyo vinaandika matendo yote ya wanadamu ambayo siku ya mwisho Mungu atawahukumu kwayo wanadamu, Kiyunani ni BIBLIA, kingereza books.
Revelation 20:12 And I saw the dead, small and great, stand before God; and the books were opened: and another book was opened, which is the book of life: and the dead were judged out of those things which were written in the books, according to their works
KIYUNANI:-
Ufunuo 20:12 και ειδον τους νεκρους μικρους και μεγαλους εστωτας ενωπιον του θεου και βιβλια ηνεωχθησαν και βιβλιον αλλο ηνεωχθη ο εστιν της ζωης και εκριθησαν οι νεκροι εκ των γεγραμμενων εν τοις βιβλιοις κατα τα εργα αυτων.
Pia vitabu ambavyo viliandika habari za Yesu (INJILI)
Mathayo
Marko
Luka
Yohana.
Navyo pia Kiyunani vinaitwa BIBLIA.... Maana kiswahili ukisoma Yohana 21:25 inasema.
"Kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu kama yangeandikwa moja moja, basi yasingetosha kwa vile Vitabu ambavyo vingeandikwa"
KIYUNANI INASOMEKA HIVI.
Yohana 21:25 εστιν δε και αλλα πολλα οσα εποιησεν ο ιησους ατινα εαν γραφηται καθ εν ουδε αυτον οιμαι τον κοσμον χωρησαι τα γραφομενα βιβλια αμην
Hapo mwishoni kuna maneno
βιβλια αμην (Biblia ingeandikwa, Kama mtu anahitaji kulipata neno BIBLIA, WINGI WA VITABU. basi azame ndani ya BIBLIA ya Kiyunani, kwenye hii ya KISWAHILI utakutana na neno VITABU, ambalo ukilihamishia kwenye KIYUNANI, unakutana na hilo neno BIBLIA (MKUSANYIKO WA VITABU) kwa lugha nyepesi, Wingi wa VITABU.
BIBLIA KATIKA AGANO LA KALE ILIANDIKWA KIEBRANIA, NA AGANO JIPYA ILIANDIKWA KIYUNANI.... pengine unaweza kujiuliza ni kwa nini iandikwe katika lugha ya Kiyunani wakati Yesu yeye alikuwa anaongea Kiaramu? (Aramic)?
Ni kwa sababu Kiyunani ilikuwa ni lugha kubwa na yenye kuongelewa sana, kama ilivyo LEO kwa Lugha ya kingereza, (international language)na hata Wayahudi kwa kipindi fulani walikuwa chini ya Utawala wa Kigiriki, kabla ya Warumi kuitawala Israeli.
Kwa hivyo mtu awaye yote asiulize neno BIBLIA kwenye Biblia iliyoandikwa katika lugha ya kiswahili au kingereza, bali atafute GREAK BIBLE, ataona kwa wingi.. kwani kuuliza kwenyE BIBLIA ya kiswahili ni sawa na kumuuliza mwarabu asiyejua kiswahili unamjua Mungu? atabaki anakushangaa maana ni neno geni, ukimtaja Ilahi au Allah hapo mtakuwa mmeelewana.
By ABEL SULEIMAN SHILIWA
WHATSAPP 0753229221
email Abelshiriwa@gmail.com.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW