Katika jina la Bwana wangu Yesu Kristo ninakemea, ninafunga na kuyaangamiza mapepo yote yanayozuia maombi Angani, katika nchi na Baharini. Pia naharibu kila pepo anayeninginia, kila pepo arukaye na wale walionyimwa chakula. Ninawatuma hadi kuzimu katika jina la Yesu. Ninaharibu vipingamizi vyenu vyote vya maombi yangu, ninawatupa katika giza la milele. Ninawafungia huko hata siku ya Bwana ya hukumu. Pia ninakemea, na kufunga na kuharibu mapepo yote yanayozuia ukombozi wangu, mafanikio yangu na miujiza. Ninaharibu kazi zenu dhidi ya maisha yangu, ninawatupa wote katika giza la milele na kamwe msiweze kuinuka tena hata siku ya hukumu ya Bwana. Ninawatumia moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote katika jina la Yesu Kristo, Amen!
UKUNGU WA KIPEPO
Ninatumia moto wa Roho Mtakatifu na Damu ya Yesu kuharibu ukungu wa kipepo unaofunika anga. Ninaharibu kila mfuniko ambao, umenifunika katika jina la Yesu Amen. Ninaharibu kila kifuniko, minyororo, mafundo na uchawi dhidi yangu. Ninauamuru moto wa Roho Mtakatifu kuviteketeza vyote na kuvifanya majivu kabisa. Ninauzimisha moshi wangu shetani dhidi ya maombi yangu. Ninatumia damu ya Yesu kuviharibu vyote, katika jina la Yesu, Amen.
Shetani, imeandikwa katika kitabu cha LUKA 1:13 kusema ''Hakuna lisilo wezekana kwa Mungu.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment