Napenda nikutie moyo wewe mzazi ambaye unauguza mtoto au ndugu na hasa wale ambao watoto/ndugu wao wana magonjwa ya kuwafanya wateseke kwa muda mrefu. Hakuna kitu kigumu kama kumuona mtoto/ndugu wako anateseka nawe huna cha kufanya. Kuna watoto/ndugu wanateseka na kansa, vidonda vya kuungua, ajali, na magonjwa mengine mbalimbali. Wazazi hawa wanahitaji maombi yetu sana sana, kibinadamu wanaumia sana na kuchoka sana.
Mungu awatie nguvu, Mungu awakumbuke, Mungu awaponye watoto/ndugu wenu na pia Mungu awape nguvu na neema ya kukabiliana na jambo hilo. Mungu yupo upande wako usikate tamaa, endelea kusimama katika nafasi yako kama mzazi bila kukata tamaa, sisi tunakuombea. Ni njema na inapendeza ukiweza kumtembelea mzazi wa aina hii, mfariji na pia msaidie gharama za matibabu kadiri unavyoweza, hakika wanahitaji sana faraja na maombi na msaada pale inapobidi.
Zaburi 46:1-2, 11
“Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.”

Ezra 10:4
“Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.”
“Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.”
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment