Unapopitia magumu na mambo ya kukatisha tamaa wakati mwingine unaona kama Mungu amekuacha. Yesu alipokuwa msalabani alipitia hali hiyo, na Ayubu katika majaribu magumu alipitia pia hali ya kukata tamaa na kuona kuwa Mungu amemuacha.
Mathayo 27:46
“Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
“Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
Ayubu 13:24
“Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako?”
“Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako?”
Maumivu makubwa ya moyo lazima yataleta simanzi na kukata tamaa. Lakini hatupaswi kwenda huku na kule kuuliza kwa watu kwanini tunapitia hayo bali tumwendee Mungu, muulize yeye maswali yote na hakika atakuonyesha ni kwanini ameruhusu upitie hayo. Baada ya majaribu magumu Mungu alimuinua Yesu na kumfanya juu ya vyote, na baada ya Ayubu kushinda Mungu alimzidishia mara dufu ya yale aliyoyapoteza.
Unapokuwa huelewi, usitafute jibu kwa wanadamu bali kwa Mungu na ameahidi hatakuacha wala kukupungukia.
Ebrania 13:5b
“kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.”
“kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.”
USIKATE TAMAA, MUNGU HATAKUACHA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment