Ibrahimu alikuwa amemtii Mungu mara nyingi katika kutembea kwake pamoja naye, lakini hakuna jaribio ambalo lingekuwa kali zaidi kuliko lililo katika Mwanzo 22 Mungu aliamuru, "Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia" (Mwanzo 22: 2a).
Mwanzo 22: 6 Baada ya hayo Abrahamu alichukua kuni za toleo la kuteketezwa akamtwika Isaka mwana wake, naye akachukua mikononi mwake moto na kisu cha kuchinjia, na wote wawili wakasonga mbele pamoja. 7 Na Isaka akaanza kumwambia Abrahamu baba yake: “Baba yangu!” Naye akasema: “Mimi hapa, mwanangu!” Basi akaendelea kusema: “Hapa pana moto na kuni, lakini yuko wapi kondoo kwa ajili ya toleo la kuteketezwa?”
Unaweza kuona Ibrahimu anafanya nini hapa? Ana kisu, ni kama anataka kumwua mwanawe Isaka. Kwa nini afanye hivyo?
Hebu kwanza yuone namna Ibrahimu na Sara walivyopata mwana wao, Isaka.
Kumbuka, Mungu aliwaahidi kwamba wangezaa mwana. Lakini lilikuwa jambo gumu, kwa sababu Ibrahimu na Sara walikuwa wazee sana. Lakini Ibrahimu aliamini kwamba Mungu anaweza kufanya jambo gumu. Basi jambo gani lilitokea?
Mungu alipokwisha kutoa ahadi yake, mwaka mzima ukapita. Ndipo, Ibrahimu alipokuwa mwenye miaka 100 na Sara 90, wakazaa mtoto wa kiume jina lake Isaka. Mungu alikuwa ametimiza ahadi yake!
Lakini Isaka alipokuwa mtu mzima, Mungu alijaribu imani ya Ibrahimu. Akasema: ‘Mchukue mwana wako Isaka uende kwenye mlima ambao nitakuonyesha. Ukamwue huko mwana wako umtoe dhabihu.’ Lakini kumbuka, Mungu alikuwa ameahidi kwamba watoto wa Ibrahimu wangekaa Kanaani. Ingekuwa namna gani kama Isaka angekufa? Ibrahimu hakufahamu hilo, lakini alimtii Mungu.
Alipofika kwenye mlima, Ibrahimu alimfunga Isaka na kumweka juu ya madhabahu aliyojenga. Lakini alipotaka kumwua Isaka, malaika wa Mungu alitoa sauti kubwa: ‘Ibrahimu, usimwumize mtoto wala kumfanya lolote. Sasa najua kwamba unaniamini, kwa sababu hukuninyima mwana wako mmoja tu!’
Lo! Ibrahimu alimwamini Mungu sana! Aliamini kwamba hakuna jambo gumu kwa Mungu, hata angemfufua Isaka katika wafu. Lakini Mungu hakutaka Ibrahimu amwue Isaka. Basi Mungu aliongoza kondoo akamatwe na miti midogo iliyokuwa karibu. Kisha akamwambia Ibrahimu amtoe kondoo huyo awe dhabihu mahali pa mwana wake.
Kwanini Mungu aliijaribu imani ya Ibrahimu?
Mungu anatumia imani ya Ibrahimu kama mfano kwa wote waliokuja baada yake kama njia pekee ya wokovu. Mwanzo 15: 6 inasema, "Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki." Ukweli huu ni msingi wa imani ya kikristo, kama ilivyorudiwa kusemwa katika Warumi 4: 3 na Yakobo 2:23. Haki ambayo ilikuwa sifa kwa Ibrahimu ni haki sawa na ile tuliyopewa wakati sisi tulipokea kwa imani sadaka abayo Mungu aliitoa kwa ajili ya dhambi zetu - Yesu Kristo. "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye" (2 Wakorintho 5:21).
Mwanzo 21:1-7; 22:1-18.
Mwanzo 21:1-7; 22:1-18.
Hadithi ya Agano la Kale kuhusu Ibrahimu ni msingi wa mafundisho ya Agano Jipya ya upatanisho,toleo la sadaka ya Bwana Yesu juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu. Yesu alisema, karne nyingi baadaye, "Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi "(Yohana 8:56).
Zifuatazo ni baadhi ya tofauti kati agano mbili za Biblia:
• "Chukua mwanao, mwana wako wa pekee, Isaka" (v 2.); "Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake wa pekee ..." (Yohana 3:16).
• "Nenda mkoa wa Moria. mtoe sadaka huko ... "(v 2.); inaaminika kwamba eneo hili ndipo mji wa Yerusalemu ulijengwa miaka mingi baadaye, mahali ambapo Yesu alisulubiwa nje ya kuta zake (Waebrania 13:12)
• "mtoe sadaka hapo kama sadaka ya kuchomwa" (v 2.); "Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na Maandiko" (1 Wakorintho 15: 3).
• "Ibrahimu akazichukua kuni za sadaka ya kuchomwa na kuziweka juu ya mwana wake Isaka" (mstari 6.); Yesu, "akibeba msalaba wake mwenyewe. . . "(Yohana 19:17).
• "Lakini ipo wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuchomwa?" (V 7.);yohana akasema, "Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, achukuaye dhambi za ulimwengu!" (Yohana 1:29).
• Isaka, mwana, alifanya kwa imani kwa baba yake katika kuwa sadaka (v 9.); Yesu akaomba, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kinipite. Hata hivyo si kama mimi nitakavyo, bali kama wewe utakavyo "(Mathayo 26:39).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment