Wengi wetu wanaweza kushangaa, kama kweli binadamu anaweza kuwa rafiki wa Mungu. Biblia inathibitisha kuwa, wewe unaye soma hii makala unaweza kuwa rafiki wa Mungu.
Isaya 41:8. “Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu (Mungu)”
Yakobo 2:23.”Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu”
Sasa tusome kidogo habari ya Ibrahimu:
Uru ulikuwa mjia ambao watu walikaa baada ya Gharika. Pakawa mji wa maana wenye nyumba nzuri. Lakini watu wa huko waliabudu miungu ya uongo. Ndivyo walivyofanya hata katika Babeli. Watu wa Uru na Babeli hawakuwa kama Nuhu na Shemu mwanawe, waliozidi kumtumikia Mungu.
Mwishowe, ilipopita miaka 350 tangu gharika, Nuhu mwaminifu akafa. Ilipopita miaka miwili mtu unayemwona katika picha hii alizaliwa. Alikuwa mtu wa pekee sana kwa Mungu. Jina lake ni Ibrahimu. Alikaa pamoja na jamaa yake katika mji huo wa Uru.
Kabla ya kuitwa Ibrahimu, jina lake lilikuwa Abram, laikini Mungu alimpa jina la Ibrahimu lenye maana ya Baba wa Mataifa mengi.
Vinyo hivyo, Serai jina la awali la Sara lilibadilishwa na Mungu. Maana ya jina jipya la Sara ni Mama wa mataifa mengi.
Siku moja Mungu alimwambia Ibrahimu (Abrahamu): ‘Ondoka Uru, wewe na ukoo wako, uende kwenye nchi ambayo nitakuonyesha.’
Je! Ibrahimu alimtii Mungu na kuacha starehe zote za Uru? Ndiyo. Ibrahimu alijulikana kuwa rafiki ya Mungu kwa sababu alimtii Mungu sikuzote.
Wengine wa jamaa ya Ibrahimu walimfuata alipoondoka Uru. Tera baba yake alimfuata. Hata Lutu mpwa wake. Na pia Sara mke wa Ibrahimu. Halafu wote wakafika Harani, na huko Tera akafa. Walikuwa mbali sana na Uru.
Muda kidogo Ibrahimu na jamaa yake wakaondoka Harani kuja Kanaani. Mungu akasema: “Hii ndiyo nchi nitakayowapa watoto wako.’ Ibrahimu alikaa Kanaani katika hema.
Mungu alianza kumsaidia Ibrahimu hata akawa na kondoo na wanyama wengine wengi na mamia ya watumishi. Lakini yeye pamoja na Sara hawakuwa na watoto wowote.
Ibrahimu alipokuwa mwenye miaka 99, Mungu alimwahidi hivi: ‘Utakuwa baba ya mataifa mengi.’ Lakini watoto wangezaliwa namna gani, maana Ibrahimu na Sara ni wazee mno?
Je, ninawezaje kuwa rafiki wa Mungu?
Yohana 15:14. “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo”.
Kwa hiyo katika mstari huo hapo juu tunaona jinsi Yesu Kristo anavyokiri kuwa kuna watu wanaoweza kuwa rafiki wa Mungu. Lakini ipo gharama katika kuwa rafiki wa Mungu, gharama hiyo ni kutenda kila Mungu analokuamuru kulitenda pasipo kuchagua.
Hii ndio faida ya kuwa Mkristo, unakuwa rafiki wa Mungu na mtoto wa Mungu, tofauti na imani au dini zingine ambazo Mungu kwao ni kama adui yao.
Usikose somo la: Mungu anajaribu imani ya Ibrahimu.
Mwanzo 11:27-32; 12:1-7; 17:1-8, 15-17; 18:9-19.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment