Monday, May 15, 2017

JE, MAMA WA ISA WA QURAN NA YESU WA BIBLIA NI YULE YULE?

Image may contain: text
Biblia inatufundisha hivi.
Yohana 19:25, Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama, Mamaye, na umbu la mamaye Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.
Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu mama wa Isa na mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu baba na kaka wa Mariamu mama wa Isa hivi.
Quran 66:12,
Na Maryamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humo roho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyeke.
Quran 19:28,
Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.
Hapa tunaona kuwa Maryamu mama wa Isa, baba yake ni Imrani na kaka yake aliitwa Haruni.
Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa:
Hesabu 26:59,
Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.
Pia soma 1Nyakati 6:1-3 na Kutoka 6:20.
Huyo Amrani aliishi miaka mingi kabla ya Yesu, tena ametokana na kizazi cha Lawi mtoto wa watu wa mzee Yakobo.
Mwanzo 29:34; Kutoka 2:1-10
Ukweli huu hapa,
Ikiwa Mariamu wa Qurani na waislamu baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1 500 kabla mama yake Yesu hajazaliwa!
Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?
Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi, Mathayo 1:1; Marko 10:47 na Luka 1:27,32, ndiyo maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu wa Yesu ni mmoja.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW