Tuesday, May 16, 2017

ISA WA QURAN ALIUMBWA LAKINI YESU ALIKUWEPO MILELE YOTE

Image may contain: text
YESU NI MUNGU:
ISA BIN MARYAM KAUMBWA
Quran. 3 au Surat Imran 59
“Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa”
Quran inadai kuwa Isa Bin Maryam aliumbwa kwa udongo, na kisha Allah akasema kuwa, na Isa bin Maryam akawa.
YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU
Yohana 1:1,14,
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”
Mika 5:2
“Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”
Yohana: 8:58 “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”.
Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe
Yohana 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”
Kolosai 1:16-17
“Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”
c) Baada ya kuishi na kufa kwa Isa bin Maryam wa waislamu, inadaiwa na uislam kama hajawahi kumtokea kimaono yeyote yule!
1. Baada ya panda mbinguni Yesu Kristo aliwatokea wengi na hasa Sauli kabla awe Paulo.
Matendo 9:4
“Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe”
d) Isa bin Maryam wao alitabiri kwamba baada yake atakuja nabii Muhammad
Quran 61 au Surat As-Saff 6
“Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! Mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad (Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri). Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”.
e) Yesu Kristo aliahidi msaidizi akamtuma Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste
Yohana 14:26
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia”
Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji
Yohana 15:26
“Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia”
Yohana 16:7
“Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”.
umesoam mwenyewe kuwa Isa Bin Mrayma yeye aliumbwa kwa udongo, lakini Yesu yeye alikuwepo milele yote.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW