Friday, April 14, 2017

Vitabu vya Korani vyapatikana katika vyoo Dallas Marekani



Polisi wameanza uchunguzi baada ya nakala za korani kupatikana ndani ya vyoo katika jumba moja la chuo kikuu cha Texas huko Dallas.
Picha kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha vitabu hivyo vikiwa ndani ya vyoo.
Polisi wa chuo wanasema kesi hiyo ni ya "kushangaza sana" na "isiyo ya kawaida" kwani chuo hicho kina wanafunzi kutoka makabila na dini mbali mbali.
Polisi wanajaribu kumtambua mmoja kati ya watu sita walioonekana wakiingia chooni wakati wa tukio hilo la tarehe 28 mwezi wa Machi. Wachunguzi wamekuwa wakikagua video za CCTV wakiwatafuta waliohusika.
Hakuna kitu kilichoguswa katika chumba kimoja ambacho huwa na vitabu vya dini tofauti, kulingana na wachunguzi.
Mkuu wa polisi Larry Zacharias aliiambia Dallas Morning News: "Hakuna anayemjua mmiliki wa vitabu hivyo."
Mohammad Syed ambaye ni rais wa chama cha wanafunzi wa Kiislamu chuoni aliambia vyombo vya habari tukio hilo ni la "kuhuzunisha kweli na pia linatatiza."
"Licha ya kuwa kuna sauti kidogo ya chuki, kuna sauti kubwa ya upendo na unaotuunga mkono na kweli tunashukuru," alisema.
Aliongeza kuwa "mazingira chuoni ni mazuri ."
Korani hizo ziligunduliwa na viongozi wa wanafunzi baada ya mkutano wao jioni hiyo.
"Nilishangaa sana," alisema Jonathan Schuler, aliyepata vitabu hivyo takatifu katika vyoo.
"Tukio hilo liliifanya maneno mengi ya chuki i niliyokuwa nikisikia na kuona kwenye taarifa za habari kuwa halisi, na karibu sana."
Maseneta wa wanafunzi wametoa taarifa wakisema hilo ni ni tukio la kipekee na haliwakilishi jamii ya chuo kikuu.
http://www.bbc.com/swahili/39601347?ocid=socialflow_facebook

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW