Friday, April 7, 2017

USIWAOGOPE MAADUI ZAKO, MKABIDHI BWANA AWASHUGHULIKIE

Image may contain: sky and outdoor
Kumbukumbu La Torati 28:7
7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Ayubu 8:22
22 Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.
Isaya 54:15,17
15 Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.
17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.
Kumbukumbu la Torati 20:4
4 kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
Ipo mistari mingi mno kwenye Biblia inayotueleza nini msimamo wa Mungu juu ya adui zetu. Lakini pia Bwana Yesu alisema jambo hili katika Matayo 5:44
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi
Ni ngumu kumeza lakini inawezekana. Kumbuka Stephano wakati anapigwa mawe anakufa alifanyaje? Aliwaombea waliokuwa wakimuua kwa mawe Matendo 7:54-60
Ukishayafahamu haya ni vyema kabisa kuyazingatia na kamwe vita inapoinuka juu yako haitakusumbua, tena utashangilia maana kwanza fahamu umemtia wivu shetani mpaka kafikia kukuchukia. Ujue sasa muda umefika wa kutumia silaha ulizonazo.
Mimi Max Shimba nimesha tumiwa vitisho vikubwa sana, na watu kadhaa kunihakikishia kuwa sita vuka mwaka 2016 na kuingia 2017. Waliapa kwa miungu yao, lakini leo hii naandika huu ujumbe wa upendo kwao kuwa, VITA VYOTE NI VYA BWANA.
Mimi sina wasiwasi kabisa, ninaendelea kuitangaza Injiri ya Bwana wetu Yesu Kristo aliye kufa kwa ajili yetu na kutupa uzima wa milele. Kamwe vitisho vya maadui havinizuii bali kunipa nguvu zaidi ya kulitangaza Jina la Yesu.
Mungu awabariki sana, USIOGOPE VITA, MPE VITA YAKO BWANA, MPE TATIZO LAKO BWANA na hakika yote yanawezekana kwake.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW