MALAIKA MKUU URIEL
Malaika wanatajwa karibu mara 400 katika Biblia. Katika Kiebrania na Kigiriki, neno “malaika” linaweza kutafsiriwa kuwa “mjumbe.”
1 Wakorintho 14:33 inasema kwamba “Mungu si Mungu wa machafuko, bali ni wa amani.” Kwa hiyo, Mungu amewapanga wanawe wa roho katika makundi matatu makuu:
(1) Maserafi, ambao ni watumishi kwenye kiti cha Ufalme cha Mungu, wanatangaza utakatifu wake, na kuhakikisha kwamba watu wake wako safi kiroho;
(2) Makerubi, ambao wanategemeza enzi kuu ya Mungu; na
(3) Malaika wengine ambao wanatenda mapenzi yake. (Zaburi 103:20; Isaya 6:1-3; Ezekieli 10:3-5; Danieli 7:10)
Malaika Mkuu Urieli, ambaye jina lake linamaanisha "Nuru ya Mungu, Light of God." au Moto wa Mungu "Fire of God".
Jina la Urieli linalotajwa katika Biblia inayo tumiwa na Waluteri, Anglikana na Wakristo wa Ki-Orthodox wa Urusi.
Hili jina la URIEL linaweza gawanyika kama ifuatavyo.
U= Nafasi; RI = Nuru/Jua; EL = Mungu IKIMAANISHA NURU YA MUNGU na wakati mwingine anaitwa MOTO WA MUNGU.
U= Nafasi; RI = Nuru/Jua; EL = Mungu IKIMAANISHA NURU YA MUNGU na wakati mwingine anaitwa MOTO WA MUNGU.
Biblia inasema, Yesu atakuja “pamoja na malaika zake wenye nguvu katika MWALI WA MOTO.” Kusudi lao litakuwa ‘kuleta kisasi juu ya wale wasiomjua Mungu na wale wasiotii habari njema juu ya Bwana wetu Yesu.’ (2 Wathesalonike 1:7, 8) Hatua hiyo itakuwa na matokeo makubwa kama nini kwa wanadamu! Wale wanaokataa kukubali habari njema ya Ufalme wa Mungu inayotangazwa leo duniani pote wataharibiwa. Ni wale tu ambao wanamtafuta Mungu (Walio okoka), wanatafuta uadilifu na upole ndio ‘watakaofichwa katika siku ya hasira ya Mungu.’—Sefania 2:3.
Mtumishi wa Elisha alikuwa ameamka mapema, akaona jeshi la Shamu lilikuwa limeuzingira mji ambao yeye na Elisha walikuwamo. Kwa hofu, akamwambia Elisha, “Ole wetu, Bwana wangu! Tufanyeje? [kwa maneno mengine, tutawezaje kutoka katika hali hii tukiwa hai? Kisha Elisha akamwambia mtumishi wake], Usiogope: kwa maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha Akaomba [kwa MUNGU] akasema, BWANA, NAKUSIHI, mfumbue macho yake, apate kuona. Na BWANA akayafumbua macho ya mtumishi yule; naye akaona: Na, tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na MAGARI YA OTO yaliyomzunguka Elisha pande zote” (2 Wafalme 6:15-17).
Jeshi lile lile au majeshi ya MUNGU ambayo Elisha alimwomba Mungu amuonyeshe mtumishi wake (mtumishi wa Elisha) ndilo jeshi lile lile ambalo MUNGU alitumia kuziangusha kuta za Yeriko (Yoshua 6:20). Yoshua alikutana na MKUU wa majeshi ya BWANA kule Yeriko katika njia hii : “Ikawa hapo, Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akainua macho yake na kuangalia, na, tazama, mtu mwanamume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wa wazi mkononi MWAKE; Yoshua AKAMWENDEA na KUMWAMBIA, Je! WEWE u upande wetu, au upande wa adui zetu? Naye akasema, LA; LAKINI NIMEKUJA SASA KAMA AMIRI WA MAJESHI YA BWANA [YESU kabla hajachukua mwili wa binadamu]. Naye Yoshua akaanguka kifudifudi mbele zake hadi chini, na kuabudu, na AKAMWAMBIA, BWANA wangu anamwambia nini mtumishi WAKE? Na AMIRI wa majeshi ya BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako kutoka miguuni mwako; kwa kuwa mahali usimamapo ni Patakatifu. Na Yoshua akafanya vivyo.
“Basi mji wa Yeriko ulikuwa umefungwa kwa sababu ya wana wa Israeli: hapana mtu aliyetoka, wala hapana mtu aliyeingia. [Hii ilikuwa kwa sababu walijua kuwa MUNGU alikuwa pamoja na Israeli, na pia walijua kuwa MUNGU alikuwa anakwenda kuwaangamiza.] BWANA akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake.
Katika kitabu cha Enoki, Nabii mkuu Enoki anatabiri kuhusu walinzi. Hawa walinzi ni malaika wa MUNGU, na ni jeshi la mbinguni la BWANA. Wakati mwingine wanasemekana kuwa malaika walinzi wa watakatifu wa MUNGU hapa duniani.
Kunao malaika wabaya (Malaika walio asi), na kuna malaika wazuri. Ufunuo 12:4 inasema kwamba theluthi moja ya malaika hawa – wale wabaya – walitupwa kutoka Mbinguni pamoja na kiongozi wao, Shetani mwenyewe (Luka 10:18). Lakini kumbuka, theluthi mbili ya malaika – wale wazuri – walibakia kwenye utumishi wa MUNGU. Wale wabaya, theluthi moja, si wabaya tu, bali ni hatari sana.
Ufunuo 16:1 inasema, “Kisha nikasikia sauti kuu kutoka Hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, enendeni mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya MUNGU juu ya nchi.” Katika Danieli 4:13, “Mlinzi [malaika] na mtakatifu walishuka kutoka mbinguni” Wakileta hukumu ya MUNGU kwa mfalme aliyekuwa na kiburi Nebukadreza, aliyesema kwenye kitabu cha Danieli 4:30, “Mji huu sio Babeli kubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu [badala ya nguvu za MUNGU], ili uwe utukufu wa enzi yangu [badala ya utukufu wa MUNGU]?”
Hii hapa ni hukumu ambayo MUNGU alimpa mlinzi ili kuifanya dhidi ya Mfalme Nebukadreza: “Hata neno lile lilipokuwa [bado] katika kinywa cha mfalme [aliyejawa na kiburi] sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee Mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa [na walinzi] mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni ; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa yeye ALIYE JUU SANA ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa AMTAKAYE ye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza: Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege” (Danieli 4: 31- 33).
USIKOSE SEHEMU YA TISA .....MALAIKA MKUU RAPHAEL
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment