Najua wengi wenu hamlifahamu hili na labda mnasoma hii aya kwa jujuu tu na au teyari umesha nihukumu ndani ya moyo wako.
Ni amri kuliamini Jina la Yesu Kristo – sio ombi.
“Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.” (1 Yohana 3:23)
Naam, kuliami Jina la Yesu Kristo ni AMRI na sio tafadhari.
Nini maana ya Amri?
Amri hutolewa na Mtu mwenye Mamlaka na inaweza kuwa juu ya Sheria wakati inapo tolewa.
Amri hutolewa na Mtu mwenye Mamlaka na inaweza kuwa juu ya Sheria wakati inapo tolewa.
Nini maana ya Sheria?
Sheria ni mfumo wa kanuni, ambazo kwa kawaida hutekelezwa kupitia seti ya taasisi. Inaunda siasa, uchumi na jamii kwa njia mbalimbali na huratibu mahusiano baina ya watu.
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. (Yohana 3:18)
SASA, ZISOME FAIDA UNAZO PATA UNAPO LIAMINI JINA LA YESU KRISTO:
Mtume Petro alipomwona hakumwomba Mungu amponye bali alimwamuru asimame na kutembea kwa Jina la Yesu Kristo!
Alisema hivi, “kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende”. Halafu; “akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu: (Yule aliyekuwa kilema). Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani ya hekalupamoja nao, akienda, akirukaruka, na kumsifu Mungu.” (Matendo ya Mitume 3:6-8)
Kile alichoamuru Mtume Petro kitokee kwa Jina la Yesu Kristo kilitokea. Aliamuru Yule kilema asimame na kutembea kwa jina la Yesu Kristo na ikawa hivyo!
Na wewe unaweza kufanya hivyo ikatokea! Kwa nini? Kwa sababu na wewe pia umepewa jina la Yesu Kristo lenye uwezo usiobadilika! Kumbuka Yesu Kristo alisema hivi,
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
KUNA UPONYAJI KATIKA JINA LA YESU KRISTO:
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. (Marko 16:17-18)
Watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. (Marko 16:17-18)
“Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa” (Yoeli 2:32)
KUNA WAKOVU KATIKA JINA LA YESU KRISTO:
“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Matendo ya Mitume 4:12)
“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” (Mathayo 1:21)
“bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.” (Yohana 1:12-13)
“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.” (warumi 10:12-13)
KULIAMINI JINA LA YESU KRISTO NI AMRI NA SIO OMBI.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment