Thursday, April 27, 2017

MUNGU IBARIKI ISRAEL


Image may contain: sky, ocean and outdoor

1. OMBEA NCHI YA ISRAELI
Nchi ya Israeli haipo pale kama nchi kwa ajili ya raia wake tu, na kwa watu waishio ndani yake tu; lakini iko pale ili Mungu aitumie kwa ajili ya kujijulisha na kuwafikia watu wote ulimwenguni. Kumbuka ya kuwa Mungu anaitumia nchi ya Israel kama Lango la kupitisha yale yote aliyokusudia uyapate kutokana na agano lake alilolifanya na Ibrahimu. Unapoiombea Israeli – Mungu anailinda na kuitunza ili itumike kupitisha vitu ambavyo Mungu anataka vikufikie.
2. OMBEA MJI WA YERUSALEMU
Kufuatana na Ezekiel 26:2; “Yerusalemu” ni “lango la kabila za watu”. Tena kufuatana na Mathayo 5:35; “Yerusalemu” ni “mji wa mfalme mkuu” …yaani Yesu Kristo! Ikiwa umeungwa kwa Kristo Yesu, basi mji huu wa Yerusalemu unakuhusu sana! Ni lango la Mungu kwa ajili ya kabila za watu – na wewe ukiwa mmojawapo! Ndiyo maana katika Zaburi 122:6 tunahimizwa kuuombea mji huu amani na kuupenda!
3. UWE NA BENDERA YA ISRAELI
Jitahidi uwe na bendera kadhaa za nchi ya Israel. Halafu ziweke au zipeperushe ofisini kwako, au sehemu yako ya biashara, au nyumbani kwako, au mahali pengine panapokuhusu wewe binafsi kama vile Roho Mtakatifu atakavyokuongoza. Hii itakuwa nafasi ya kueleza uhusiano wako na taifa la Israeli kama uzao wa Ibrahimu kwa Imani uliyonayo katika Kristo Yesu. Hii ni sawa na mstari wa Wagalatia 3:29 usemao:”Na kama ninyi ni wa Kristo,basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi”
4. FUTA LAANA DHIDI YA NCHI YA ISRAELI ZILIZOTAMKWA KUTOKEA TANZANIA.
Mungu alimwambia Ibrahimu ya kuwa:”…Akulaaniye nitamlaani…” (Mwanzo 12:3) kumbuka ya kuwa kuwepo kwa taifa la Israeli ni tunda mojawapo la agano kati ya Mungu na Ibrahimu. Kwa hiyo unaposikia mtu yeyote ambaye ni mtanzania anailaani nchi ya Israeli; au si mtanzania lakini anailaani Israeli akiwa katika nchi ya Tanzania – usikae kimya! Unayo mamlaka katika jina la Yesu kutumia Damu ya Yesu (i) kuomba toba kwa ajili ya, na kwa niaba ya Tanzania kwa ajili ya laana hiyo dhidi ya nchi ya Israeli; (ii) kuomba maombi ya kuifuta laana hiyo, na badala yake achilia maneno ya kuibariki nchi ya Israeli.

Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW