Mathayo 2:
1 Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu, 2 wakauliza, "Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu."
11 Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane.
Mwenye haki ya kuabudiwa na kusujudiwa ni Mungu peke yake. Sasa iweje hawa wataalamu wa Nyota na wajuzi kutoka Mashariki ya Mbali wamwabudu na kumsujudia Yesu?
Kwanini mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye?
Ndio utafahamu kuwa YESU NI MUNGU.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment