“Siku Hii Itakuwa Ukumbusho Kwenu”
TORATI INAITAMBUA PASAKA:
“Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaisherehekea ikiwa sherehe kwa Mungu Yehova.”—Kutoka 12:14.
“Kristo Pasaka yetu ametolewa dhabihu.” (1 Korintho 5:7)
Nisani 14 ndiyo iliyokuwa siku ya Pasaka, lakini siku zote nane za sherehe hiyo ziliitwa pia Pasaka. (Kutoka 12:14-17; Luka 22:1; Yohana 18:28; 19:14) Pasaka ilikuwa mojawapo ya sherehe rasmi (“sikukuu,” Union Version) ambazo Wayahudi walipaswa kusherehekea kila mwaka.—2 Nyakati 8:13.
YESU ALISHEREKEA PASAKA, LAKINI WASABATO NA WAISLAM WANAIPINGA PASAKA:
Yesu na mitume wake walisherehekea Pasaka kila mwaka kwa sababu walikuwa Wayahudi na hivyo walikuwa chini ya Sheria ya Musa. (Mt. 26:17-19) Mara ya mwisho waliposherehekea Pasaka, Yesu alianzisha mwadhimisho mpya ambao wafuasi wake wangekumbuka kila mwaka, yaani, Mlo wa Jioni wa Bwana. Lakini walipaswa kuuadhimisha siku gani?
Kwa kuwa Yesu alianzisha Mlo wa Jioni wa Bwana baada tu ya Pasaka hiyo ya mwisho, mwadhimisho huo mpya ulifanywa katika siku ambayo Pasaka ilikuwa ikisherehekewa.
Kristo aliwaambia hivi Petro na Yohana: “Nendeni mkatutayarishie pasaka ili tule.” (Luka 22:7, 8) ‘Mwishowe, saa ikafika’ ya mlo wa Pasaka, baada ya jua kutua mnamo Nisani 14, ilikuwa Alhamisi jioni. Yesu alikula mlo huo pamoja na mitume wake, kisha akaanzisha Mlo wa Jioni wa Bwana. (Luka 22:14, 15) Usiku huo, alikamatwa na kushtakiwa. Yesu alitundikwa mtini karibu saa sita mchana Nisani 14, naye akafa siku hiyohiyo alasiri. (Yohana 19:14)
Hivyo, ‘Kristo pasaka yetu akatolewa dhabihu’ siku ileile ambayo mwana-kondoo wa Pasaka alichinjwa. (1 Korintho 5:7; 11:23; Mt. 26:2) Yesu alizikwa mwishoni mwa siku hiyo ya Kiyahudi, kabla ya Nisani 15 kuanza. *—Lawi 23:5-7; Luka 23:54.
Baada ya kusoma aya zote hapo juu, kwanini Wasabato "SDA" na Waislam wanaikataa sikukuu hii ya Sabato iliyo kwenye Torati?
Kama kweli Wasabato na Waislam wanaitambua TORATI, Kwanini wanasema PASAKA ni sikukuu ya WAPAGANI?
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment