Tuesday, April 4, 2017

JE, YESU ALIKUWA AMEOA?

Image may contain: text
Ni kwa nini DaVinci code husema kwamba Yesu alikuwa ameoa?
Je, Yesu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Maria Magdalena?
Yesu Kristo ni dhahiri kwamba hakuwa ameoa na au bibi. Kuna hadithi maarufu leo hii (kama za Da Vince Code) ambazo husema kwamba Kristo amemwoa Maria Magdalene. Hadithi hizi ni za uongo kabisa na hazina msingi kiteolojia, kihistoria, au kibiblia.
Huku baadhi ya injili hutaja kuwa Yesu alikuwa na uhusiano wa karibu na Maria Magdalene, hakuna hata moja yao hasa inasema kwamba Yesu alikuwa amemwoa Maria Magdalene, au kuwa na uhusino wowote wa kimapenzi pamoja naye. Ukaribu unaokisiwa ni pale Yesu alimbusu Maria Magdalene, ambayo kwa urahisi inaweza kuwa “kumbukumbu ya busu ya kirafiki” Zaidi ya hayo, hata kama injili ya Aginostiki moja kwa moja ilisema kwamba Yesu alikuwa amemwoa na Maria Magdalene, hawatakua na mamlaka, kwa vile taarifa za Injili ya Agnostiki zimethibitika kuwa za udanganyifu zikinuia kujenga mtazamo Kiagnostiki kumhusu Yesu.
Kama Yesu alikuwa ameoa, Biblia ingekuwa imetuambia hivyo, au kungekuwa na baadhi ya taarifa zisizo na utata na ukweli kwa hoja hiyo. Maandiko kamwe hayawezi kimya kabisa juu ya suala hilo muhimu. Biblia inamtaja mama yake Yesu, baba mlezi, ndugu na dada zake wa kambo. Ni kwa nini iache kutaja ukweli kwamba Yesu alikuwa na mke? Wale wanaoamini / kufundisha kwamba Yesu alikuwa ameoa wanafanya hivyo katika jaribio la “kumfanya Yesu kuwa mwanadamu.” ili wamfanye kuwa kama mtu wa kawaida, hasa kama kila mtu mwingine. Watu kwa ufupi hawataki kuamini kwamba Yesu alikuwa Mungu katika mwili (Yohana 1:1, 14; 10:30). Kwa hivyo, wao hutunga na kuamini hadithi kuhusu Yesu kuwa na mke na watoto, na kuwa kama mtu wa kawaida.
MADAI YA DaVince:
Jacobovici si mtu wa kwanza kudai uhusiano wa kimapenzi unaowezekana kati ya Yesu na Maria . Sinema, Jaribio la Mwisho la Kristo, na vitabu kama Damu Takatifu, Kikombe Kitakatifu, na maandishi ya Da Vinci, yalifanya siri uhusiano kati ya Yesu na Maria kuwa sehemu kuu ya habari zao.
Maandishi ya Da Vinci yanaanza na ukurasa wa ukweli ambao unafanya hadithi ya kutunga kuonekana kuwa kweli katika madai yake yote. Kitabu kimevunja rekodi zote katika orodha ya mauzo bora ya New York, na imefuatiwa na sinema fanikifu kibiashara. Ukusanya hodari wa ukweli wa mtunzi Dan Brown pamoja na ubunifu umewaaminisha wasomaji wengi kwamba Yesu na Maria Magdalena walikuwa wameoana na walikuwa na mtoto (Angalia saa Tabasamu la MonaLisa). Lakini madai haya ya kimapenzi yanatangaza sana vitabu na sinema ingawa hakuna ushahid wa Kihistoria au kiteologia au Kibiblia kuwa Yesu alioa.
Swali la pili litakuwa, “
Je, Yesu Kristo angekuwa ameoa?
Hakuna dhambi kwa kuoa. Hamna dhambi juu ya kuwa na uhusiano wa kingono katika ndoa. Kwa hivyo, naam, Yesu angeweza kuwa ameoa na bado kuwa mwanakondoo Mungu asiye na hatia na Mkombozi wa ulimwengu. Wakati huo huo, hakuna sababu ya kibiblia ya Yesu kuoa. Hiyo sio hoja katika mjadala huu. Wale wanaoamini Yesu alikuwa ameolewa hawaamini kwamba alikuwa na dhambi, au kwamba yeye ni Masihi. Kuoa na kupata watoto sio sababu kuu ambayo Mungu alimtuma Yesu. Marko 10:45 inatuambia ni kwa nini Yesu alikuja, “ Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”
Imeratibiwa na Max Shimba
Imenukuliwa kutoka:
Je, unaswali?
Y, Jesus Org.
Christ Nations Org.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW