Sunday, April 30, 2017

SABABU KUMI (10) KWANINI NAMPENDA YESU



1. YESU NI MCHUNGAJI MWEMA
Yohana 10: 10Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi imekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele. 11‘‘Mimi ndimi Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema huutoa uhai Wake kwa ajili ya kondoo.
Yesu ninae mpenda ni mwenye Mikono Wazi na yupo tayari kutupokea sote. Sote tumefanya makosa, lakini habari njema ya Ukombozi ni kuhusu Upendo wa Mungu kwetu sisi ambao tunaupata kutoka na kupitia Yesu Kristo ambaye ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu. Karibu kwa Mchungaji Mwema ambaye ni Yesu Kristo aliye kufa Msalabani kwa ajili ya dhambi zako.

2. YESU ALIKUJA KUWASAIDIA WALIO LEMEWA NA MIZIGO AU MATATIZO YAO
Matayo 11: 28 “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.’’
Ukristo sio kuhusu kufanya sheria bali ni kupokea jibu ambalo Yesu alisha kujibu pale Msalabani. Hii ndio Raha ya kuwa na Yesu. Yesu alisha maliza matatizo yako yote pale Msalabani, alisha maliza au ponya Magonjwa yako yote. Ndio Maana Yesu anasema kwako kuwa, NJOONI NINYI NYOTE MLIO LEMEWA NA MIZIGO. Kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kuja kwa Yesu, halafu yeye atakupa Majibu yako yote. Sasa njoo kwa Yesu na upokee majibu ya matatizo yako.

3. YESU AMEKUSAMEHE -UPENDO WA MUNGU
Zaburi 103: 2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake, 3 akusamehe dhambi zako zote na kuponya magonjwa yako yote, Kumfahamu Yesu ni kujua kuwa Yesu alisha maliza kazi zote pale Msalabani, ikiwa pamoja na kukusamehe dhambi zako zote. Sasa basi, najua unasema kuwa labda ulifanya vitu vibaya hapo nyuma na unashindwa elewa kivipi Yesu atakusamehe dhambi zako. Ndugu msomaji, Yesu hajali nini umefanya hapo nyuma, Yesu anacho taka kutoka kwako ni kuwa, umkabidhi matatizo yako yoke na yeye alisha maliza kazi pale Msalabani. Sasa basi, mwambie Yesu kuwa wewe ni mwenye dhambi na omba msamaha na amini kuwa amesha kusikia na kukujibu/samehe. Yesu ni Mungu na Mungu wetu ni Upendo.

4. YESU NI UHURU
Warumi 8: 1. Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, Yeye aliihukumu dhambi katika mwili, 4ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.
Kuna Uhuru Mkubwa sana unapo kuwa ndani ya Yesu Kristo. Unapo mkabidhi Yesu maisha yako na kuwamchia yeye ayaendesha, basi unakuwa huru kabisa. Yesu ni Mungu, na yeye anampango mzuri sana kwa maisha yako. Hivyo basi, nakusihi uache kuwa mungu wa maisha yako na Mkabidhi Yesu maisha yako ili akuonyeshe nini cha kufanya. Anza maisha ya Kiroho na Yesu ambaye ndie muumba wako. (2 Wakorintho 5:19) Dhambi haina mamlaka juu yangu kwa sababu mimi sasa naishi chini ya neema. (Warumi 6:14) Neema ni msingi wangu na ukombozi katika Kristo. Neema ya Mungu sio leseni ya dhambi, ni nafasi ya kufanikiwa.

5. YESU NI HAKI YANGU
Warumi 5: 1 Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wokovu ni zawadi ya haki. (Warumi 5:17) Katika Ufalme wa Mungu, hakuna kufanya kazi ili kupata haki yako, bali haki yako ni zawaidi kutoka kwa Mungu. Dini zingine zinafundisha kuwa, wewe ufanye kazi na Mungu ndio nakupa haki yako, Katika UKRISTO, tunapokea zawadi ya Wokovu. Hivyo basi, elewa kuwa Yesu alisha kulipia kwa kupitia damu ya Msalaba.
Nakukaribisha kwa Yesu aliye hai ambaye ni Mungu na amekupa haki ya kuwa Mwana wa Mungu kwa kupitia damu yake.

6. YESU NI FURAHA YANGU
"Mambo haya mimi nimesema nanyi ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu ikamilike." (Yohana 15:11)
Furaha ni kitu kinacho toka ndani yako. Yesu anakaa ndani yako ndio maana YESU NI FURAHA YANGU. Maana yeye ndio mwanzo wa furaha na yeye ndie anayetupa furaha ndani ya maisha yetu.
Yesu anayeishi ndani yangu na yeye ndie anayetoa furaha, Yeye ni mwanga wa maisha yangu.. Yesu ndio anayenijua mimi ni bora, ananipenda zaidi. Yeye alitoa maisha yake kwa ajili yangu maisha yangu. Furaha ya Bwana ni nguvu zangu. (Nehemia 8: 9) Yesu ni yule ambaye ananipenda nani faraja kwangu. Nafurahi kwa furaha isiyo na kifani na kamili ya utukufu. (1 Petro 1: 8)

7. YESU NI UFUFUO
"Mimi ndiye ufufuo na uzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi." (Yohana 11:25)
Yesu ndie anatoa maisha mapya na ya milele. Yeye ni ufufuo na uzima. Kwahiyo hauhitaji kutafuta wapi ulipo ufufuo na wapi ulipo uzima, "YESU YEYE NDIE UFUFUO NA YEYE NDIE UZIMA" na anaishi ndani yako. Anatoa ushindi katika maisha na maisha katika kifo. Hakuna haja ya kuishi kwa hofu, na hakuna haja ya kuogopa kifo.Yesu anasema, "Kwa sababu mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai." (Yohana 14:19) Pia anatangaza, "Mimi nimeushinda ulimwengu." (Yohana 16:13)
Karibu kwa Yesu ambaye ni Ufufuo na Uzima.

8. YESU NDIE ANAYE DHIHIRISHA YOTE

"... Mimi najua yule niliyemwamini .." (2 Wakorintho, 1:12)
Maisha ya Mkristo au Kikristo sio maisha ya kukata tamaa. Ni maisha ya ushindi katika Yesu aliye hai. Tunajua Mungu kwa njia ya Neno lake. Kwa Neno lake anaongea na moyo wetu. Kwa Neno lake uwaangazia mioyo yetu. Neno lake huponya moyo wako. Kama unataka kujua Mungu ni nani, basi mwangalie Yesu. Kama unataka kujua Yesu ni nani, basi jifunze Neno lake. Neno inaonyesha Mungu ni nani na nini Mungu amefanya kwa ajili yetu. Neno pia linaonyesha sisi ni nani katika Kristo.

9. YESU NDIE ANAE NIONGOZA KATIKA KUFANYA MAAMUZI MUHIMU KATIKA MAISHA YANGU
"Kwa nini, kuna faida ya mtu, kama yeye kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake." (Marko 8:36)
Jambo la muhimu zaidi tunaweza kufanya katika maisha haya ni kujiandaa kwa ajili ya maisha yajayo. Barabara inayoongoza kwenye uzima ni nyembamba. Ni nyembamba, lakini ina faida. (1 Timotheo 3: 8) Yesu ni mlango. Sisi hutembea kwa njia ya Yesu ndani ya ukamilifu wa Mungu. Hivyo basi, Yesu ndie Njia itupelekayo kwenye uzima wa milele.
Ndugu msomaji, kama huna uhakikisho wa maisha baada ya kifo, nakushauri umpokee Yesu, hakika utapata uzima wa milele.

10.YESU NI DAKTARI WANGU
"4Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba,tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa. " (1 Petro 2:24)
Yesu alichukua udhaifu wangu. Yesu alichukua magonjwa yangu. Kwa kupigwa kwake mimi nikapona. Uponyaji wa Mungu ni kitu rahisi na rahisi kuamini, na uponyaji wa Mungu ni kitu rahisi na rahisi kupata. Roho Mtakatifu aliyemfufua Kristo kutoka wafu nI HUYO HUYO ANAYE FANYA MIUJIZA YOTE KWAKO. Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu. (Warumi 8:11) Mungu alimtuma Neno lake kuniponya. (Zaburi 107: 20) Neno lake ni uzima na afya kwa mwili wangu wote. (Mithali 4: 20-22) Neno la Mungu kunilinda kutokana na maambukizi ya dunia hii.
Karibu kwa Yesu Kristo ambaye ni Daktari wa Madaktari.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Ministries Org.

YESU NI MUNGU KUTOKANA NA QURAN (SEHEMU YA NNE)

Image may contain: text
1. Allah kasema Yesu ni NENO
2. Biblia inasema kuwa Neno ni Mungu
Allah anasema kuwa Yesu wa Quran ni NENO litokalo kwake. Ikiimaanisha kuwa, asili ya Yesu si binadamu bali ni Neno litokalo kwa Mungu. Quran hiyo hiyo inasema kuwa Neno la Allah halina mwanzo, ikiimaanisha kuwa NENO la Allah lilikuwa na Allah karne zote na NENO la Allah halikuumbwa. (Allah's word is eternal) Sura 6:115, Sura 10:64, Sura 18:27.
Hebu tusome aya kutoka Quran kuwa Yesu ni NENO:
Surat Al Imran 45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
Quran inakiri kuwa Maryam alipata MWANA KWA KUPITIA NENO LA ALLAH. Hivyo basi Yesu asili yane ni NENO na sio binadamu. Rejea Surat Al Imran aya 45.
Surat An Nisaai 171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na NENO LAKE tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.
Allah anaendelea kusema kuwa Yesu ni NENO LAKE. Kumbe basi Yesu ambaye ni Neno la Mungu alikuwa na Mungu siku zote. Soma Sura 6:115, Sura 10:64, Sura 18:27.
Je Biblia nayo inasema nini kuhusu NENO?
BIBLIA INASEMA KUWA NENO NI MUNGU
Yohana 1: 1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye NENO alikuwa Mungu.
Katika Yohana Sura ya Kwanza aya ya Kwanza, tunafundishwa kuwa NENO alikuwepo na Mungu hapo Mwanzo kabla ya kuumbwa kitu chochote kile. Wakati huo huo, Quran nayo inasema kuwa Allah aliumba Yesu kwa kutumia Neno ambalo lilikuwa na Allah tokea Mwanzo.
Ningependa mfahamu kuwa, Quran ambayo inasema kuwa Yesu aliumbwa kutoka NENO iliandikwa miaka 632 baada ya Biblia. Ikimaanisha kuwa Biblia ndio ya kwanza kuandikwa halafu Quran ndio ikafuata.
ALLAH ANAKWAMBIA WEWE MWENYE SHAKA KUWA, KAMA HUAMINI ASEMAYO MAX SHIMBA, Basi waulize watu wa Kitabu. Sisi Wakristo na Wayahudi ndio watu wa Kitabu. Allah anamaanisha kuwa, Watu wa Kitabu ambao ni Sisi Wakristo na Wayahudi ndio tunayo haki na mamlaka ya kuthibitisha maneno ya Quran kama ni ya kweli au uongo. Soma
Surat Yunus 94. Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Aya hiyo katika Surat Yunus iliyoteremka Makka na kutafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani inathibitisha kuwa Watu wa Kitabu ndio wenye Mamlaka ya kuhakikisha na au thibitisha ukweli wa Quran. Hakika Mimi nathibitisha kuwa YESU NI NENO na NENO NI MUNGU, maana hayo yalisema miaka mia 632 kabla ya kuteremshwa kwa Surat Yunus Makka na yamo katika Injili kutokana na Yohana aya ya kwanza na sura ya kwanza.
Allah anamwambia Muhammad katia Suratul Yunus aya 94 kuwa, kama Muhammad anashaka na ukweli kuwa Yesu ni Neno na Neno ni Mungu. Basi Muhammad atuulize Wakristo kuwa, Je, hayo madai ya Allah ni ya kweli? Hakika Biblia imekamilika na kusema bila ya shaka yeyote ile kuwa Yesu ni Neno na Neno alikuwa na Mungu kabla ya Mwanzo kuwepo. Allah na yeye amekiri hayo kuwa Yesu ni Neno ambalo lilikuwa na Mungu hata kabla ya Mwanzo kuwepo.
Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni NENO na Biblia inasema kuwa NENO NI MUNGU.
Katika huduma yake,
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2015

UNAZIJUA KAMBA ZA MAUTI ZILIZO KUFUNGA?

Image may contain: 1 person, text
Habari njema ni kuwa waliofungwa na kamba za mauti leo hii watawekwa huru na kufunguliwa kwa Jina la Yesu. Lengo la kufungwa na kamba za mauti ni kusababisha kifo; kifo katika uwezo wako wa kuomba, kifo cha uwezo wa kumtumikia Mungu, kifo cha uwezo wa kufanya kazi n.k.
Zaburi 18:4…[Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.]…
Ina maana Daudi alikuwa anatembea kama wewe na mimi lakini tayari katika ulimwengu wa roho Daudi amejiona akiwa amefungwa kamba za mauti.
Zaburi 116:3….[Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;]...
Pindi ufungwapo kamba za mauti, shida za kuzimu zitaanza kukufuata. Kamba za mauti ni 'ishara ya kifo'. Sanda vivyo hivyo, huvishwa watu wanapokuwa wamepoteza uhai wao (wafu).
Endapo watoto wako watakuwa wamefungwa kamba za mauti, utakuta kuwa, wale waliowafunga wameshawafanya 'maiti' ingawa wanatembea. Kwa hiyo, mtu anakuwa hai kimwili lakini katika ulimwengu wa roho mtu huyo walishamuua na hata pengine walishaadhimisha ‘arobaini’ ya huyo mtu bila yeye kujua.
MAOMBI: kwa Jina la Yesu , Ewe kamba uliyefungwa kwenye hatua zangu za maendeleo, funguka, kamba iliyofunga elimu yangu, kamba iliyofunga sura yangu isionekane, nakuamuru funguka na uondoke kwa Jina la Yesu. Amen
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

WALEENI WATOTO KATIKA NJIA YA KRISTO

Image may contain: 4 people, people smiling, text
Mithali 22:6 inasema; “mlee mtoto katika njia impasayo, naye
hataiacha, hata atakapokuwa mzee”.
Hivyo ni malezi ndiyo yafanyayo watoto kuwa wema au wabaya au watukutu, kumbuka huwezi kuwatenga watoto na jamii, nchi au dunia hii iliyojaa yote mema na mabaya Isipokuwa kwa kuwajaza nguvu ya kushinda majaribu ya dunia ambayo imo katika Neno la Mungu.
Torati 6:6-7. "Na maneno haya ninayokuamuru leo yata kuwa katika moyo wako nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii nakuyanena uketipo katika nyumba yako na utembeapo njiani na ulalapo na uondokapo."
Nidhamu ni namna yakuonyesha upendo kwa mtoto. Imeandikwa katika Mithali 13:24 "Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali ampendaye humrudi mapema."
Nidhamu njema humfunza mtoto Imeandikwa Mithali 29:15 "Fimbo na maonyo hutia hekima bali mwana aliyeachiliwa humuaibisha mamaye."
Sababu ya kumwathibu mtoto nikumfanya akuwe vema. Imeandikwa Waefeso 6:4 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana."
Watoto hutoa matunda ya wazazi wao. Imeandikwa katika Kutoka 34:7 "Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; Wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia hata kizazi cha tatu na cha nne."
Mungu ana tarajia matokeo gani kwa watoto? Imeandikwa katika Waefeso 6:1 "Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana maana hii ndiyo haki."
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

MWANA MASUMBWI MANNY PACQUIAO ANASOMA BIBLIA ASUBUHI, MCHANA NA JIONI

Image may contain: 1 person, sitting, eating and indoor
Huu ni ushuhuda mzuri na utakutia moyo na wewe uwe na utamaduni wa kusoma Biblia kila siku. Manny Pacquiao - (Boxing Fighter) ni tajiri na anampenda Yesu na haoni haya kusema kuwa, Yesu ni Mungu na kamwe hato muacha.
Je, wewe unampenda Yesu? Je, unawashuhudia marafiki zako kuhusu Yesu? Usiogope na wala usikate tamaa, Mshuhudie Yesu, Kazini, Shuleni kwenye Basi na njiani popote pale.

JE, TALAKA INARUHUSIWA KWENYE UKRISTO?

No automatic alt text available.
Somo gumu sana hili na linatatanisha na kutikisa akili za watu. Hebu tusome Biblia kwa umakini sana na kuweka theolojia pembeni.
Haya tuanze utafiki kwa umakini.
Kwanza ni muhimu kukumbuka maneno ya Biblia katika Malaki 2:16a: “ nachukia talaka, asema Bwana Mungu wa Israeli,” kulengana na biblia, mpango wa Mungu juu ya ndoa ni iwe ushikamano wa siku zote za mwanadamu duniani. “ Hata si wawili tena bali mmoja. Kwa hivyo kile Mungu amekiunganisha mwanadamu asikitenganishe” (Mathayo 19:6). Mungu antambua ya kwamba kwa kuwa ndoa ni ya wenye dhambi wawili, talaka haina budi kutokea. Katika agano la kale aliweka sheria za kulinda haki za watalaka hasa wanawake (Kumbukumbu la Torati 24:1-4). Yesu akasema sheria hizi zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu lakini hayakuwa mapenzi ya Mungu (Mathayo 19:8).
JE, UASHERATI UNARUHUSU TALAKA?:
Utofauti wa maoni juu ya talaka na kuoa tena unatokana na maneno ya Yesu katika Mathayo 5:32 na 19:9. “isipokuwa kwa habari za uasherati” ndicho kipengele peke yake ambacho Mungu anatoa ruhusa ya talaka na kuoa tena katika maandiko. Wengi hutafsiri maneno haya kuwa ni kile kitendo cha zinaa kinachofanyika baada ya kuolewa. Katika mila na desturi za wayahudi mke na mme walihesabiwa kuwa wameoana toka wakati wa kuposwa kwa msichana. Kitendo cha mapenzi kilichofanyika wakati huu pia kingehesabiwa sababu ya kutosha talaka.
ARGUMENT YA KWANZA:
Neno la kigiriki lilitafsiriwa kumaanisha uasherati ni neno linaloweza kumaanisha kila aina ya uchafu wa kimapenzi kama zinaa, uasherati, ukahaba na kadhalika. Yesu anathibitisha kuwa talaka inakubalika mahali uchafu huu wa kimapenzi unapotendeka. Kitendo cha ngono ni cha umuhimu mkubwa katika ndoa “nao wawili watakuwa mwili mmoja” (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:5; Waefeso 5:31). Kwa hivyo kosa la kufanya kitendo hicho nje ya ndoa inaweza kuwa sababu mwafaka ya talaka. Kama ni hivyo basi pia Yesu alikuwa na hoja ya kuoa tena.
ANGALIA NENO "KUOA MWENGINE" ALILO SEMA YESU:
Katika kusema “na kuoa mwingine” (Mathayo 19:9) inathibitisha talaka na kuoa tena vinakubalika. Jambo muhimu ni kutambua ya kwamba ni wale waathiriwa na hali mbaya ya mapenzi nje ya ndoa pekee wanaokubaliwa kuoa tena. Kukubaliwa huku, ijapokuwa hakukutajwa moja kwa moja katika maandiko, ni huruma ya Mungu kwa yule aliyetendewa dhambi wala si kwa aliyetenda dhambi ya zinaa. Katika maandiko haya hayaelezi kama mwenye kutenda dhambi ya zinaa naye aruhusiwa kuoa au la.
KITENDO CHA ZINAA SI SHARTI LA TALAKA BALI NI NAFASI YA TALAKA:
Kitendo hiki cha zinaa si sharti la talaka bali ni nafasi ya talaka. Hata kitendo hiki kikitendeka, kwa neema ya Mungu, mke na mme wanaweza kunusuru ndoa yao kwa kusameheana. Mungu ametusamehe mengi. Tunaweza kuiga mfano wake hata kiasi cha kusamehe dhambi ya zinaa (Waefeso 4:32). Lakini mara nyingi watu hukosa toba halisi katika swala hili hata kiasi cha kuishi katika maisha ya zinaa. Hapo ndipo Mathayo 19:9 hutumika. Wakati mwingine watu huoa mapema baada ya talaka hata kama Munhu baado anawataka wakae bila ndoa. Mungu wakati mwingine huita mtu akiwa peke yake ili ushirika wake na Mungu usitatizwe na mtu. (Wakorintho wa Kwanza 7:32-35). Kuoa tena baada ya talaka ni mapenzi ya mtu binafsi lakini haimaanishi kuwa ndilo suluhisho pekee.
SAMEHE SABA MARA SABINI:
Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa talaka za wakristo zimekuwa nyingi karibu sawa na za wale wasioamini duniani kote. Biblia inasisitiza kuwa Mungu hapendezewi na talaka (Malaki 2:16 ) na kusameheana huko na kupatana upya ni alama mwafaka ya mwenye imani maishani (Luka 11:4; waefeso 4:32). Mungu anatambua kuwa talaka itatendeka hata kati ya wanawe. Mwenye kutalakiwa au mwenye kuoa tena asijisikie kuwa hapendwi na Mungu sawa na wengine kama jambo hili limetukia maishani mwake wala si sawa na Mathayo 19:9. Mungu hutumia hata hali ya dhambi ya mwanadamu kukamilisha mapenzi yake mema.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UPENDO WA YESU

Image may contain: 2 people, people standing and outdoor
Yesu alionyesha upendo wa kujidhabihu kwa njia bora sana. Kujidhabihu ni kutanguliza mahitaji na masilahi ya wengine bila ubinafsi. Yesu mwenyewe alieleza hivi: “Hakuna aliye na upendo mkubwa zaidi kuliko huu, kwamba mtu fulani aisalimishe nafsi yake kwa niaba ya marafiki wake.” (Yohana 15:13) Yesu alitoa uhai wake mkamilifu kwa hiari kwa ajili yetu. Huo ulikuwa wonyesho mkuu zaidi wa upendo kuwahi kuonyeshwa na mwanadamu yeyote. Lakini Yesu alionyesha upendo wa kujidhabihu kwa njia nyinginezo pia.
Yesu alisema hivi: “Nampenda Baba.” (Yohana 14:31) Hakuna mtu yeyote anayeweza kumpenda Mungu kama Mwana huyo, ambaye alikaa na Baba yake kwa muda mrefu sana kabla kiumbe yeyote hajaumbwa. Upendo ulimchochea Mwana huyo mwaminifu kutaka kumwiga Baba yake.—Yohana 14:9.
Wakati wa huduma yake duniani, Yesu alijidhabihu kwa upendo katika njia mbalimbali. Hakuwa na ubinafsi wowote. Alijishughulisha mno na huduma yake hivi kwamba alijinyima mambo ya kawaida ambayo wanadamu wamezoea. “Mbweha wana mapango na ndege wa mbinguni wana viota, lakini Mwana wa binadamu hana mahali popote pa kulaza kichwa chake.” (Mathayo 8:20) Yesu alikuwa seremala stadi sana, kwa hiyo angeweza kujijengea nyumba nzuri sana au angeweza kupata pesa kwa kutengeneza na kuuza fanicha maridadi sana. Lakini hakutumia ustadi wake kupata vitu vya kimwili.
Yesu alikuwa na huruma kama Baba yake. Maandiko yanaonyesha jinsi ambavyo Yesu alijitahidi kuwasaidia watu waliotaabika kwa sababu aliwahurumia sana. Biblia inafafanua huruma ya Yesu kwa kutumia neno la Kigiriki linalotafsiriwa “sukumwa na sikitiko.” Msomi mmoja anasema hivi: ‘Neno hilo linafafanua hisia ya ndani sana ambayo inamchochea mtu kutoka moyoni. Hakuna neno jingine la Kigiriki linalofafanua hisia ya huruma kwa mkazo sana kama neno hilo.’ Ebu ona pindi fulani-fulani ambapo huruma ilimchochea Yesu kutenda.
Yesu aliiga kikamili upendo wa Baba yake katika njia nyingine muhimu—alikuwa “tayari kusamehe.” (Zaburi 86:5) Jambo hilo lilionekana wazi hata alipokuwa kwenye mti wa mateso. Yesu alisema nini alipokuwa amepigiliwa misumari mikononi na miguuni, kabla ya kufa kifo cha aibu? Je, alimlilia Mungu awaadhibu wale wanaomwua? La hasha! Kati ya maneno ya mwisho ambayo Yesu alisema ni: “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui wanalofanya.”—Luka 23:34.
Kumbuka kuwa, Yesu anakupenda sana na upendo wake ndio ulimfanya afe kwa ajili ya dhambi zako.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Friday, April 28, 2017

A Group Of LIONS Save Christians From Execution By Islamic Militants, Says Pastor

It is a remarkable story of God’s intervening hand to save his people. Pastor Paul Ciniraj, director of Bibles for Mideast, says that he and other Christians were rescued from the clutches of death by a group of three lions. Ciniraj and his group were under attack from Islamic militants when the giant cats attacked and scared the murderous group away.
“My risen Lord Jesus Christ has saved my life once again,” Pastor Paul wrote, “and I praise and thank God for His unspeakable grace!” It was Easter Sunday when the miracle took place. The pastor was recovering in the home of some friends following a stoning attack by Islamists earlier that day. “Suddenly, a group of militants reached the house, armed with steel bars and other weapons,” he reported to WND.
Pastor Ciniraj thought this was the end of the road for him, and feared for the life of the 80-year-old resident, and several children who were taking refuge in the house alongside him. “Losing all hope, we thought for sure this was our last day,” he said. They only had just one more thing to do: pray. Then, something truly Biblical took place!
“Completely unexpectedly, a lion ran from the forest, leapt toward the militants, and seized one by the neck. When other combatants tried to attack the lion, two other lions bounded toward them. The terrified militants fled the site, and the lions left us completely alone,” he said.
“Equally astonishing, records show no
https://hellochristian.com/7296-a-group-of-lions-save-christians-from-execution-by-islamic-militants-says-pastor

Thursday, April 27, 2017

BROOKLYN MOSQUE and Muslim-owned store were totally gutted in a fire


A fire ripped through a building housing a mosque and a deli in Bedford-Stuyvesant, Brooklyn Saturday morning. The building houses the Sunshine Express Deli and the Brooklyn Broadway Jame Masjid and Islamic Center.

CBS  The mosque, which has served the community there since 2004, has 250 members, who are now struggling to find a new place to worship for the holy month of Ramadan, which starts in a few weeks. “It’s horrible, it’s horrible. It’s a disaster, I don’t know. We’re like almost crying,” Hussein said. “People are asking, ‘Where are you going to pray?’ So I said, ‘I don’t know.” (There’s always the street, where Muslims love to lift their asses to Allah so they can throw their Islamic supremacy in our faces)
MIC  The New York Fire Department is currently investigating the cause of the fire incident. The New York Police Department said in an email that, at this time, there are no signs or reason to believe the fire was intentionally started as part of a hate-motivated crime. 
WARNING BNI Readers: be careful what you say in your comments:


Somali Muslim sues employer because the firm held an all-pork barbecue for employees


Not only that…Leyla Hashi has filed a discrimination suit against a national furniture retailer, Aaron’s, in Portland, Maine, claiming that she was harassed by fellow employees and ultimately fired from a job at its local branch in 2015 because she is Muslim, a Somali Muslim (not because she kept requesting time off to observe Muslim holidays?).

BangorDailyNews  According to the lawsuit, the termination allegedly followed a pattern of harassment in which other employees mocked and demeaned Hashi, a black Somali immigrant, based on her , appearance, attire and religion.

Somali Muslim women in Maine and other states are infamous for stirring up trouble:

Hashi is suing the store’s Georgia-based parent corporation, SEI/Aaron’s Inc., for reinstatement of her job, lost wages and benefits with interest, punitive damages and legal costs.

At Aaron’s, Hashi claims that she was subjected to a stream of verbal harassment that was brushed off by management and deliberately was excluded from workplace activities. At one point, after Hashi had told her boss that observant Muslims don’t eat pork, the Aaron’s “office put on an all pork barbecue,” the suit states.

When she asked to take off work on a Friday to celebrate the Eid holiday, she claims her request was denied at first, and then granted. 

The next Monday, when Hashi returned to work, she was greeted by a new person sitting behind her desk and laughter from other employees, the suit states. Her manager then allegedly fired her without providing an explanation. The manager later listed “Not a fit” as the reason for Hashi’s termination, according to the court documents.

Damn right, they don’t fit in, look at how they dress for work:

CHINA bans several Islamic baby names, including Mohammed, in volatile Muslim-majority region of Xinjiang


In its ongoing crackdown on Islam in China, dozens of popular Muslim baby names including Islam, Quran, Mecca, Jihad, Imam, Saddam, Hajj, and Medina are banned under ruling Chinese Communist Party’s “Naming Rules For Ethnic Minorities.”

Hindustan Times  China has banned dozens of Islamic names for babies belonging to the restive Muslim-majority Xinjiang province, in a move that would prevent children from getting access to education and government benefits, a leading rights group said on Tuesday.

Xinjiang authorities have recently banned dozens of names with religious connotations common to Muslims around the world on grounds that they could “exaggerate religious fervour,” the Human Rights Watch said. Children with banned names will not be able to obtain a “hukou,” or household registration, essential for accessing public school and other social services, it said.

The new measures are part of China’s fight against terrorism in this troubled region, home to 10 million Muslim Uyghur ethnic minority. This is the latest in a slew of new regulations restricting religious freedom in the name of countering “religious extremism,” the HRW said.

Conflicts between the Uyghur and the Han, the majority ethnic group in China that also controls the government, are common in Xinjiang. A full list of names has not yet been published and it is unclear exactly what qualifies as a religious name, it said.

On April 1, Xinjiang authorities imposed new rules prohibiting the wearing of “abnormal” beards or veils in public places, and imposing punishments for refusing to watch state TV or radio programmes.

These policies are blatant violations of domestic and international protections on the rights to freedom of belief and expression, the HRW said. Punishments also appear to be increasing for officials in Xinjiang who are deemed to be too lenient.

MAPIGO 10 KWA FARAO NA MISRI

Image may contain: text
Basi wakati wa Mungu ukafika wa kuonyesha yeye ana uwezo kuliko Farao. Unajua alivyofanya? Ni kwa kuleta mapigo 10 au taabu kubwa, juu ya Misri.
TAZAMA picha hapo chini katika mada hii. Kila moja inaonyesha pigo ambalo Yehova alileta juu ya Misri.
PIGO LA KWANZA:
Katika picha ya kwanza unaweza kumwona Harui akiupiga Mto Nailo kwa fimbo yake. Alipoupiga, maji ya mto yakawa damu. Samaki wakafa, nao mto ukaanza kunuka vibaya.
PIGO LA PILI:
Farao anawafukuza vyura kitandani mwake, pigo la pili
Kisha, Yehova akafanya vyura watoke katika Mto Nailo. Walikuwa mahali pote—katika majiko ya kuokea mikate, vikaangio, katika vitanda vya watu—mahali pote. Vyura hao walipokufa Wamisri waliwakusanya wengi sana, na nchi ikanuka vibaya.
PIGO LA TATU:
Halafu Haruni akaipiga ardhi kwa fimbo yake, nayo mavumbi yakawa chawa. Hao ni wadudu wadogo wanaouma. Chawa walikuwa pigo la tatu juu ya nchi ya Misri.
PIGO LA NNE:
Mapigo mengine yaliumiza Wamisri peke yao, si Waisraeli. Pigo la nne lilikuwa mainzi wakubwa waliojaa katika nyumba za Wamisri wote.
PIGO LA TANO:
Pigo la tano lilikuwa juu ya wanyama. Ng’ombe na kondoo na mbuzi wengi wa Wamisri wakafa.
PIGO LA SITA:
Kisha, Musa na Harui wakachukua majivu na kuyatupa angani. Yakawa vidonda vibaya juu ya watu na wanyama. Hilo lilikuwa pigo la sita.
PIGO LA SABA:
Baada ya hapo Musa akainua mkono wake kuelekea angani, naye Mungu akapeleka ngurumo na mvua ya mawe. Ilikuwa mvua ya mawe iliyo mbaya zaidi kuipiga Misri.
PIGO LA NANE:
Pigo la nane lilikuwa kundi la nzige. Nzige hao wengi sana hawakuwa wameonekana kabla ya hapo wala baadaye. Walikula kila kitu ambacho mvua ya mawe haikuharibu.
PIGO LA TISA:
Pigo la tisa lilikuwa giza. Kwa muda wa siku tatu giza zito liliifunika nchi, lakini Waisraeli wakawa na nuru katika makao yao.
PIGO LA KUMI:
Mwishowe Mungu akawaambia watu wake wapake damu ya mwana-mbuzi au mwana-kondoo juu ya milango yao. Kisha malaika wa Mungu akapita juu ya Misri. Malaika huyo alipoiona damu, hakuua mtu ye yote katika nyumba hiyo. Lakini katika nyumba zote ambazo damu haikupakwa juu ya milango, malaika wa Mungu aliua wazaliwa wa kwanza wa wanadamu na wa wanyama. Hilo lilikuwa pigo la 10.
Baada ya pigo hilo, Farao akawaambia Waisraeli waondoke. Watu wa Mungu wote walikuwa tayari kwenda, na usiku uo huo wakaanza kutoka Misri.
Kutoka sura ya 7 hadi 12.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

MUNGU IBARIKI ISRAEL


Image may contain: sky, ocean and outdoor

1. OMBEA NCHI YA ISRAELI
Nchi ya Israeli haipo pale kama nchi kwa ajili ya raia wake tu, na kwa watu waishio ndani yake tu; lakini iko pale ili Mungu aitumie kwa ajili ya kujijulisha na kuwafikia watu wote ulimwenguni. Kumbuka ya kuwa Mungu anaitumia nchi ya Israel kama Lango la kupitisha yale yote aliyokusudia uyapate kutokana na agano lake alilolifanya na Ibrahimu. Unapoiombea Israeli – Mungu anailinda na kuitunza ili itumike kupitisha vitu ambavyo Mungu anataka vikufikie.
2. OMBEA MJI WA YERUSALEMU
Kufuatana na Ezekiel 26:2; “Yerusalemu” ni “lango la kabila za watu”. Tena kufuatana na Mathayo 5:35; “Yerusalemu” ni “mji wa mfalme mkuu” …yaani Yesu Kristo! Ikiwa umeungwa kwa Kristo Yesu, basi mji huu wa Yerusalemu unakuhusu sana! Ni lango la Mungu kwa ajili ya kabila za watu – na wewe ukiwa mmojawapo! Ndiyo maana katika Zaburi 122:6 tunahimizwa kuuombea mji huu amani na kuupenda!
3. UWE NA BENDERA YA ISRAELI
Jitahidi uwe na bendera kadhaa za nchi ya Israel. Halafu ziweke au zipeperushe ofisini kwako, au sehemu yako ya biashara, au nyumbani kwako, au mahali pengine panapokuhusu wewe binafsi kama vile Roho Mtakatifu atakavyokuongoza. Hii itakuwa nafasi ya kueleza uhusiano wako na taifa la Israeli kama uzao wa Ibrahimu kwa Imani uliyonayo katika Kristo Yesu. Hii ni sawa na mstari wa Wagalatia 3:29 usemao:”Na kama ninyi ni wa Kristo,basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi”
4. FUTA LAANA DHIDI YA NCHI YA ISRAELI ZILIZOTAMKWA KUTOKEA TANZANIA.
Mungu alimwambia Ibrahimu ya kuwa:”…Akulaaniye nitamlaani…” (Mwanzo 12:3) kumbuka ya kuwa kuwepo kwa taifa la Israeli ni tunda mojawapo la agano kati ya Mungu na Ibrahimu. Kwa hiyo unaposikia mtu yeyote ambaye ni mtanzania anailaani nchi ya Israeli; au si mtanzania lakini anailaani Israeli akiwa katika nchi ya Tanzania – usikae kimya! Unayo mamlaka katika jina la Yesu kutumia Damu ya Yesu (i) kuomba toba kwa ajili ya, na kwa niaba ya Tanzania kwa ajili ya laana hiyo dhidi ya nchi ya Israeli; (ii) kuomba maombi ya kuifuta laana hiyo, na badala yake achilia maneno ya kuibariki nchi ya Israeli.

Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE, UNAYO HEKIMA KUTOKA KWA MUNGU?




(a) Solomoni alionyeshaje hekima ya pekee katika kuamua ni nani aliyekuwa mama ya mtoto?
(b) Mungu anaahidi kutupatia nini, na ni maswali gani yanayozuka?
Ilikuwa kesi ngumu sana—wanawake wawili walibishania mtoto mmoja mchanga. Wanawake hao waliishi pamoja, na mmoja wao alijifungua mwana siku chache tu baada ya mwingine kujifungua. Mtoto mmoja alikuwa amekufa, na kila mwanamke alidai kwamba mtoto aliyekuwa hai alikuwa wake. * Hapakuwa na watu wengine walioshuhudia lililotukia. Yaelekea kwamba kesi hiyo ilikuwa imesikilizwa katika mahakama ya chini lakini haikusuluhishwa. Mwishowe, kesi hiyo ilipelekwa kwa Solomoni, mfalme wa Israeli. Je, angefunua ukweli wa mambo?
Baada ya kuwasikiliza wanawake hao wakibishana kwa muda, Solomoni aliomba upanga. Kisha, akaamuru mtoto huyo akatwe vipande viwili na kila mwanamke apewe kipande kimoja. Mara moja mama ya mtoto huyo akamsihi mfalme amkabidhi yule mwanamke mwingine mtoto wake mpendwa. Lakini mwanamke yule mwingine aliendelea kusisitiza mtoto huyo akatwe vipande viwili. Sasa Solomoni akajua ukweli wa mambo. Alijua jinsi ambavyo mama humhurumia na kumpenda sana mtoto wake, naye alitumia ujuzi huo kutatua kesi hiyo. Hebu wazia furaha ya mama huyo Solomoni alipompa mtoto wake na kusema: “Yeye ndiye mama yake.”—1 Wafalme 3:16-27.
Solomoni alikuwa na hekima ya pekee, sivyo? Watu walistaajabu sana waliposikia jinsi Solomoni alivyosuluhisha kesi hiyo, “maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake.” Naam, hekima ya Solomoni ilikuwa zawadi kutoka kwa Mungu. Mungu alikuwa amempa “moyo wa hekima na wa akili.” (1 Wafalme 3:12, 28) Lakini vipi sisi? Je, Mungu anaweza pia kutupatia hekima? Ndiyo. Solomoni aliongozwa kuandika hivi: “BWANA huwapa watu hekima.” (Mithali 2:6) Yehova aahidi kuwapa hekima, yaani, uwezo wa kutumia ujuzi, ufahamu, na utambuzi, wale wanaoitafuta kwa unyofu. Tunawezaje kupata hekima inayotoka juu? Na tutaitumiaje maishani mwetu?
Tunahitaji kushika hekima kwa sababu ni zawadi kutoka kwa Mungu. Solomoni alisema: “Mwanangu, . . . shika hekima kamili na busara.” (Mithali 3:21) Kwa kusikitisha, Solomoni mwenyewe alishindwa kufanya hivyo. Alikuwa mwenye hekima maadamu alitii kutoka moyoni. Lakini mwishowe, wake zake wengi wa kigeni waliugeuza moyo wake kutoka kwa ibada safi ya Yehova. (1 Wafalme 11:1-8) Hali iliyompata Solomoni inaonyesha kwamba tusipotumia ifaavyo ujuzi tulio nao hautatufaidi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Wednesday, April 26, 2017

Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya I


Waislamu wanashikilia kwamba Muhammad alitabiriwa kwenye Biblia. Andiko lao kuu wanalotumia kutetea hoja hii ni Kumbukumbu la Torati 18:18. Andiko hilo linasema:
Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Haya ni maneno ambayo aliambiwa Musa na Yehova.
Mmojawapo wa watu ambao walijaribu sana kuonyesha kuwa andiko hili lilimhusu Muhammad, alikuwa ni mwanaharakati wa Kiislamu, marehemu Ahmed Deedat wa Afrika Kusini.
Unaposoma au kusikiliza sababu wanazotoa ili kuthibitisha madai yao hayo, kwa kweli ni sababu zenye nguvu sana (kwa mtu ambaye haelewi Biblia); ingawaje hazina uzito hata chembe ukijua Biblia inasema nini katika ujumla wake na ni nini makusudi na malengo ya Mungu kwa uzao mzima wa Adamu.
Siku moja Ahmed Deedat alimkaba mchungaji mmoja kwa maswali kuhusu mstari huu wa Kumbukumbu 18:18 kiasi kwamba, kwa maneno yake, Deedat anasema kuwa mchungaji yule alikosa cha kusema.
Deedat alimpomsomea mstari huo, alimwuliza, “Unabii huu unamhusu nani?”
“Unamhusu Yesu,” mchungaji alijibu.
“Unajua,” alisema Deedat, “Maneno ya msingi kabisa kwenye unabii huu ni ‘mfano wako’. Sasa, ni kwa vipi Yesu ni mfano wa Musa?”
“Musa alikuwa Myahudi na Yesu alikuwa Myahudi. Pili, Musa alikuwa nabii na Yesu alikuwa nabii,” alijibu mchungaji.
Deedat anaendelea kusema, “Kama hizi ndizo sababu mbili pekee zinazotuwezesha kumtambua mhusika wa unabii huu wa Kumbukumbu 18:18, basi unabii huu unaweza kumhusu yeyote kati ya wafuatao baada ya Musa: Sulemani, Isaya, Ezekieli, Danieli, Hosea, Yoeli, Malaki, Yohana Mbatizaji, n.k. maana hawa wote nao walikuwa Wayahudi na pia manabii. Kwa nini basi useme kuwa unabii huu unamhusu Yesu na si hawa wengine?”
Deedat anasema kuwa mchungaji yule alikosa cha kusema. Kisha Deedat akasema, “Mimi nadhani Yesu ndio hafanani kabisa na Musa.”
Zifuatazo sasa ndizo sababu ambazo Deedat na watoa hoja wa Kiislamu juu ya suala hili wanazozitoa ili kutetea hoja hii:
1. Yesu ni Mungu (kulingana na Biblia), lakini Musa si Mungu. Kwa hiyo, hafanani na Musa.
2. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (kulingana na Biblia), lakini Musa hakufa kwa ajili hiyo. Kwa hiyo, hafanani na Musa.
3. Yesu alienda kuzimu siku tatu (kulingana na Biblia), lakini Musa hakwenda huko. Kwa hiyo, hafanani na Musa.
Deedat akaendelea sasa kuonyesha jinsi Musa anavyofanana na Muhammad. Zifuatazo ndizo hoja zake au hoja zao Waislamu:
1. Musa na Muhammad walikuwa na baba na mama, lakini Yesu hakuwa na baba wa kibinadamu. Hivyo, aliye mfano wa Musa ni Muhammad na sio Yesu.
2. Musa na Muhammad walizaliwa kwa njia ya kawaida lakini Yesu aliumbwa kwa njia maalumu ya kimuujiza.
3. Musa na Muhammad walioa na kuzaa wana lakini Yesu hakuoa wala kuzaa kwenye maisha yake yote.
4. Musa na Muhammad walikubaliwa kama mitume na watu wa nyakati zao, lakini Yesu alikataliwa. Na hata leo bado Wayahudi hawamkubali. Na pia Biblia yenyewe nayo inasema: Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. (Yohana 1:11).
5. Musa na Muhammad walikuwa manabii na pia wafalme. Walikuwa manabii kwa vile walipokea ufunuo kutoka kwa Mungu na kuwapatia viumbe wa Mungu. Walikuwa wafalme kwa vile walikuwa na mamlaka ya uzima na mauti juu ya watu wao. Ndiyo maana kwa mfano, Musa alitoa amri auawe mtu aliyekamatwa akiokota kuni siku ya sabato (Hesabu 15:13). Muhammad naye alikuwa na nguvu hizo. Manabii wengine kama vile Yona, Danieli, Ezra, n.k. walikuwa na karama ya unabii lakini hawakuwa na mamlaka ya kuondoa uhai wa mtu. Yesu naye alikuwa kwenye kundi hili la pili. Hivyo, hafanani na Musa.
6. Musa na Muhammad walileta sheria mpya kwa watu wao. Lakini Yesu hakuleta sheria mpya. Hata Yeye mwenyewe anakiri kwamba: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie. (Mathayo 5:17-18).
7. Musa na Muhammad walikufa kifo cha kawaida, lakini kulingana na Ukristo, Yesu aliuawa kikatili msalabani.
8. Musa na Muhammad walikufa na wamelala mavumbini, lakini kulingana na Ukristo, Yesu yuko mbinguni.
Deedat anasema, “Mchungaji yule alikuwa hana la kujitetea, nilimwambia, Hapa nimekuthibitishia jambo moja tu. Lakini unabii una zaidi ya hapo. Kuna sehemu inayosema kuwa nabii yule atatoka, ‘miongoni mwa ndugu zake’.
Kwa hiyo akaendelea kutoa hoja zake kwamba:
9. Abrahamu alikuwa na watoto wawili. Ishameli kutoka kwa Hajiri, na Isaka kutoka kwa Sara. Hawa walikuwa ndugu. Watoto wa Isaka ni Wayahudi na watoto wa Ishamaeli ni Waarabu. Kwa hiyo, watoto wa Ishmaeli ni ndugu wa watoto wa Isaka. Kama basi nabii huyo alitakiwa kutoka miongoni mwa ndugu zake, basi ni kwa Waarabu na si kwa Wayahudi wenyewe. Muhammad, ambaye ni wa uzao wa Ishmaeli ndiye nabii miongoni mwa ndugu za Wayahudi, yaani Waarabu, anayetajwa kwenye Kumbukumbu 18:18, na si Yesu ambaye ni Myahudi. Je, hata Biblia yenyewe haimsemi Ishmaeli kwamba: Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote (Mwanzo 25:18)?
10. Unabii unasema: nami nitatia maneno yangu kinywani mwake. Huyu ni Muhammad kwa sababu alikuwa ni mtu asiye na kisomo, yaani hakuwa amesoma, lakini malaika Jibrili alipomtokea kwenye pango la Hira (au Jabal-un Noor), alimwambia ‘iqra’ au ‘soma’ au ‘sema’. Matokeo yake Muhammad alianza kusema maneno ambayo Allah alikuwa akiyaweka ndani ya kinywa chake kwa miaka 23 iliyofuata – ambayo ndiyo yamekuja kuzaa kitabu cha Quran.
11. Nabii Isaya anasema: Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi (Isaya 29:12). Andiko hili linamtaja Muhammad kwa sababu alipokuwa anapokea ujumbe kutoka kwa Allah, alikuwa ni mtu asiye na elimu isipokuwa ile iliyotoka kwa Allah mwenyewe.
12. Unabii huu unaendelea kusema: Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake (Kumbukumbu 18:19). Deedat anasema kuwa Quran katika sura Nas aya 114 inaanza kwa kwa kusema: in the name of God, most gracious, most merciful. Pia anaendelea kusema kuwa kila sura nyuma yake, yaani 112, 111, 110, n.k., zinaanza hivyo hivyo. Kwa hiyo, yale ambayo Muhammad anayasema, anafanya hivyo kwa jina la Allah – sawasawa na unabii wa Kumb. 18:19 unavyosema. “Lakini,” Deedat anasema, “Wakristo huanza ‘Kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.’”
Hoja hizi ukiziangalia ni hoja zenye nguvu sana na ambazo, katika hali ya kawaida, zina mantiki kubwa. Hizi ni hoja ambazo zinaweza kabisa kumtoa mtu kwenye uzima wa milele ndani ya Kristo na kumtumbukiza kwenye upotevu na uangamivu wa milele. Na ninaamini zitakuwa zimeshafanya hivyo kwa baadhi ya watu.
Sijui ndugu msomaji, kama ungekuwa ni wewe ungesemaje? Ni kwa kiasi gani imani yako itabakia imara baada ya kukutana na hoja nzito kama hizi?
Unaweza kuzisoma hoja hizi kwa Kiingereza kwa kubofya HAPA.
Basi nakuomba ufuatane nami katika sehemu ya pili ya makala haya, ambapo nitaeleza jinsi ambavyo hoja hizi hazina ukweli wowote kimaandiko licha ya kuonekana zenye uzito namna hii.
Yesu Kristo ndiye njia, na kweli, na uzima wa milele. Yesu Kristo ndiye safina ya nyakati hizi. Gharika inakuja, ambapo kila aliye nje ya safina atasombwa na moto wa milele.
Mtume Paulo anasema vizuri sana.
Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. (1 Wakorintho 2:4-15).
Shika sana ulicho nacho asije mwovu akakichukua; maana siku tulizonazo ni nyakati za uovu mwingi.

Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya II


Katika makala yaliyopita tuliona hoja za ndugu wa Kiislamu wanavyojaribu kwa juhudi nyingi kuonyesha kwamba Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia. Katika makala hayo niliahidi kuwa nitaeleza jinsi ambavyo hoja zao hazina ukweli wowote. Licha ya kwamba Mungu wanayemwamini amewahakikishia kwamba Muhammad ametajwa kwenye Biblia, ukweli ni kwamba hajatajwa hata kidogo!


 Katika sehemu ya kwanza ya mfululizo huu, nilimalizia kwa kunukuu kile ambacho Yehova, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, anasema juu ya Neno lake. Hebu tuangalie tena baadhi ya maneno hayo. Imeandikwa: 

Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho,tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. (1 Wakorintho 2:12-15). 

Tatizo mojawapo kubwa ninaloliona mara nyingi kwenye Uislamu na Waislamu ni kutazama mambo kwa jinsi ya mwili. Hapo ndipo penye shida kubwa yanapokuja masuala ya rohoni. Kama uko kwenye safari ya kimaisha katika ulimwengu wa kimwili na unalenga kuishia kwenye ulimwengu wa kiroho (jambo ambalo ndilo linaloendelea kwa wanadamu wote), basi ni lazima utafute maana ya mambo ya ulimwengu wa mwilini kulingana na ulimwengu wa rohoni. Ukiishia tu kutazama mambo katika mwili, una hasara kubwa!! Ni lazima kutambua kuwa Mungu hatupi ujumbe wake ili tuweze kuwa matajiri, maarufu na wenye vyeo wa hapa duniani. Kama hayo ndiyo malengo yako makuu katika maisha haya, basi wewe una hasara kuliko watu wote. Hayo si mambo ya msingi. Mungu ametuweka duniani kwa makusudi makubwa zaidi ya hayo.

Yeye analenga mambo yadumuyo; si mambo ya kupita. Hivyo, kiini hasa cha ujumbe wa Mungu wa kweli ni maisha ya milele yajayo kwenye ulimwengu wa roho.
 Sasa, kwa kuwa ndugu zangu hawa, wao wako zaidi katika mambo ya hapa duniani, ya kimwili, haishangazi basi kumwona Ahmed Deedat na wenzake wakiishia kuangalia tabia za kimwili za Musa na kuzilinganisha na tabia za kimwili za Muhammad na kusema kwamba eti, huo ndio uthibitisho kwamba maandiko ya Biblia wanayonukuu yanamzungumzia Muhammad. Inasikitisha sana kuwa na juhudi kubwa hivyo ambayo mwisho wake ni uangamivu. Na inasikitisha zaidi kwa sababu uko msururu mrefu nyuma yao wa watu wanaowaamini akina Deedat. Hata hivyo, nina uhakika kabisa kwamba nia yao ya ndani kabisa ni nzuri sana. Ni watu waliojitoa kwa moyo mkuu sana kwa Mungu wao na kwa dini yao. Suala tu linabaki kwamba, Je, wako sahihi? 

Lakini mara zote unapowaangalia ndugu hawa wanavyojitahidi katika kuhalalisha Uislamu, tena kupitia Biblia, kwa kweli unawahurumia. Wanahangaika kwa kweli. Kisaikolojia, ni dalili za mtu ambaye nafsi inamsuta usiku na mchana juu ya jambo ambalo nafsi hiyo hailikubali, lakini anajaribu kila njia kuituliza kwa kufunika hali halisi, ili angalau apate amani fulani ya ndani. Naamini umeshaona mtu ambaye amepatwa na jambo zito, kwa mfano kufiwa na mtu wake wa karibu. Kwa sababu nafsi inakataa kukubali ukweli huo, basi ataanza kuongea mambo mengi.

Kwa mfano, anaweza kusema, “Haiwezekani! Musa, tulikuwa naye jana tu. Musa mbona alikuwa mtu mzuri tu? Kwa nini afe? Hii si sawa. Hapana. Musa yupo. Hizi ni njama tu za watu!” n.k, n.k.
 Mtu huyu atahangaika huku nafsi yake ikitamani sana kwamba lile lililotokea lisiwe kweli, bali liwe kama asemavyo yeye. Lakini mwisho wake ni nini? Itambidi akubali tu. Hicho ndicho ninachokitafsiri kwa hawa ndugu ambao wanajaribu kwa juhudi kubwa kutafuta kumhalalisha Mtume wao kupitia Biblia.

Lakini haitawezekana! Ukiikataa kweli, jitihada zozote za kujaribu kuhalalisha uongo, haziwezi kuzaa matunda unayotarajia; hata kama nia yako ni nzuri. Nia nzuri haigeuzi uongo kuwa kweli hata siku moja!
 Na ni jambo la kushangaza sana kwamba Mungu wao amewaambia kuwa Mtume huyo ametajwa kwenye Biblia, jambo ambalo si kweli kabisa! Hili peke yake linatosha kumfanya kila Mwislamu aliye na nia ya kuwa na uzima wa milele kujiuliza mara mbilimbili. Shida tu ni kwamba, wamefundishwa kuogopa kuliko kuuliza na kuhoji mambo. 

Quran inasema kuwa Allah atawarehemu watu mbalimbali, lakini wakiwamo: ...those that shall follow the Apostle – the Unlettered Prophet – whom they shall find mentioned in the Torat and the Gospel. (Sura 7:157). Kwa tafsiri ya jumla ni kuwa anasema, atawarehemu pia wale (Wakristo) wanaomfuata Mtume (Muhammad) ambaye ametajwa kwenye Torati na Injili (Biblia). Ndiyo! Hivyo ndivyo anavyosema. Labda kama watasema kuwa andiko hilo limeongezwa na watu – jambo ambalo hawawezi  kulisema maana ni wepesi sana kung’ang’ania kwamba Biblia imebadilishwa na kupotoshwa, lakini si Quran. 

Kutokana na andiko hili, Waislamu wamejitahidi kwelikweli kutafuta ni wapi humo kwenye Torati na Injili ambako Muhammad ametajwa kama Allah alivyowaambia. Ndio sasa juhudi na bidii yao ikaangukia kwenye maandiko kadhaa yakiwamo Kumbukumbu 18:18 na Isaya 29:12. Kwa hiyo wametoa hoja nyingi (ambazo kama nilivyosema, ni za kimwili tu) ili kujaribu kutimiza hamu yao ya kuona kwamba kile ambacho Mungu wao amewaambia, ni kweli kipo kwenye Biblia. [Waislamu amkeni; tafakarini; mhoji yale mnayoamini]. Kama hujasoma hoja zao hizo, tafadhali tazama kwenye sehemu yakwanza ya makala haya. Nini kinazifanya hoja hizi za Waislamu zikose mantiki? Hata Waswahili husema: Siri ya mtungi aijuaye kata.

Yehova, ambaye ndiye mwenye Biblia, tumeona kuwa anasema katika Wakorintho ya kwamba twayanena maneno: yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
 Yule mwenye Neno kaweka msimamo juu ya Neno lake mwenyewe – kwamba ukitaka kumwelewa anachomaanisha, ni lazima ufasiri Neno lake kwa namna ya rohoni. Itakuwa ni ajabu kama wewe usiye mhusika uje na sheria zako kwa ajili ya kuendesha mambo ya nyumbani kwa mwingine ambazo mwenye nyumba hakuzipanga. Kisha unataka watu wengine wasimwamini mwenye nyumba, bali wakuamini wewe! 

Dunia hii inapita. Siku zijazo dunia hii pamoja na vitu yote tunavyoviona kwenye anga havitakuwapo kabisa. Kutakuwapo, badala yake, ulimwengu mpya utakaodumu milele. Mungu katika kujishughulisha kwake na mwanadamu, analenga kwenye mambo ya MILELE. Haya mambo ya ugali na nguo na wake na waume, n.k. ni mambo tu ya hapa duniani ambayo yanatuwezesha kuishi tu hapa ili tufikie ile hatima kuu – yaani kuishi MILELE! 

Mambo yote anayoongea Mungu kwenye Biblia yanalenga maisha hayo yajayo ya milele. Hii ni kusema kuwa, yanalenga kwenye ulimwengu ujao wa roho; si ulimwengu huu wa mwili. Mungu anatumia maisha yetu ya kimwili ili kutengeneza au kuandaa maisha yetu ya kiroho yajayo. Pia, ametumia maisha ya kimwili ya taifa na watu wa Israeli kuelezea ujumbe wa mambo ya rohoni. Bibliasi kitabu cha historia juu ya taifa la Israeli. Biblia ni kitabu chenye ujumbe wa rohoni wa sasa na baadaye ambao unawasilishwa kupitia maisha ya kimwili ya taifa la Israeli. Kwa hiyo, kama utasoma Biblia na ukaishia kuona tu kwamba: 
  • Kulikuwa na mwanadamu anaitwa farao.
  • Kulikuwa na watu wanaitwa Waisraeli. Hawa walikuwa utumwani Misri baadaye wakatoka kwenda Israeli.
  • Wayahudi walipita jangwani na baadhi wakafia humo.
  • Musa alikuwa na mke.
  • Aliishi Nuhu akajenga safina. Watu wengi walikufa kwa gharika.
  • Yesu alivua viatu kila alipoingia kwenye sinagogi.
  • Wayahudi waliwatahiri watoto wao.
  • Mtu akikamatwa kwenye uzinzi alipigwa mawe hadi kufa.
  • Wayahudi walinawa mikono kabla ya kula.
  • Wayahudi walifuga ndevu.
  • Musa alikufa kama wanadamu wengine, n.k., n.k.
 Kama haya ndiyo tu unayoyaona, wewe hauna tofauti na mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari anayesoma somo la Historia ya mambo yaliyotokea zamani. Hapo hujajua kamwe kwamba Mungu si mwalimu au mwandishi wa historia. Kufunza Historia si jambo ambalo Mungu anajishughulisha nalo hata kidogo. Hata kidogo!! Ndugu zangu Waislamu, Mungu yuko kwenye kazi inayoamua UZIMA na MAUTI kwa wanadamu. Ujumbe wa Mungu unahusiana na wapi kila mwanadamu atakuwa MILELE! Je, ni mbinguni milele; au ni jehanamu milele? Ni lazima uvuke ngazi ya kimwili ya kutazama mambo, uingie kwenye ngazi ya rohoni. Hapo TU ndipo utaanza kuzungumza mambo ya Mungu ambaye ni Roho; na si damu na nyama kama sisi wanadamu. Ni muhimu sana kutafuta ujumbe wa milele ndani ya ujumbe wa kupita. Hebu tusome tena andiko hilo la Biblia wanalotumia Waislamu kumhalalisha mtume wao: Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. (Kumbukumbu 18:18). Tutaangalia andiko hili hatua kwa hatua na jinsi ambavyo kamwe halimhusu Muhammad. 
  1. Maneno ‘miongoni mwa ndugu zao’
Yehova alimwambia Musa kuwa atawaletea Israeli nabii ambaye angetokea miongoni mwa ndugu zao. Ni wazi kabisa kwamba katika andiko hili, Mungu wa Israeli anamlenga nabii mmoja tu, licha ya kwamba Israeli kumekuwako na manabii wengi. Kwa hiyo, ili lisimhusu kila nabii basi nabii huyo ni lazima awe tofauti na manabii wengine kwa jinsi atakavyokuwa anafanana na Musa. Na Ahmed Deedat na Waislamu wenzake wanasema kuwa nabii huyo ni Muhammad kulingana na sababu ambazo tuliziona kwenye sehemu yakwanza ya makala haya. Hebu tuanze kwa kuweka msingi. Mungu aliweka amri inayohusu watawala wa Israeli. Amri hiyo inasema kwamba:Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu; usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katikandugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako. (Kumbukumbu 17:14-15). Ahmed Deedat anadai kwamba maneno ndugu zao kwenye Kumbukumbu 18:18 yanamaanisha uzao wa Ishmaeli (yaani Waarabu). Katika karne na karne za watawala wa Israeli,  je, ni lini alishawahi kuwako mfalme wa Israeli aliye Mwishmaeli (Mwarabu)? Jibu ni HAIJAWAHI KUTOKEA! Andiko hili tu peke yake linatosha kabisa kumwondolea mbali Muhammad katika uhusiano na Kumb. 18:18. Lakini hata hivyo, ngoja tuendelee. Hebu tazama maandiko yafuatayo: 
  • Lakini Benyamini hawakukubali kuisikia sauti ya ndugu zaowana wa Israeli. (Waamuzi 20:13)
  • Kisha itakuwa, hapo baba zao au ndugu zao, watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa ihisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; wala ninyi hamkuwapa wao, au kama sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia. (Waamuzi 21:22)
  • Basi itakuwa hata lini usijewaamuru watu warudi na kuacha kuwafuatia ndugu zao? (2 Samweli 2:26)
  • Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu yandugu zao Wayahudi. (Nehemia 5:1)
  • lakini watatumika pamoja na ndugu zao katika hema ya kukutania, kushika ulinzi, lakini wasitumike katika huo utumishi tena. (Hesabu 8:26).
  • Na wazao wako utakaozaa baada ya hawa watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao. (Mwanzo 48:6).
  • lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. (Yoshua 22:7).
 Maandiko haya yanataja maneno ‘ndugu zao.’ Lakini yoteyanamaanisha Waisraeli na si Waarabu. Ninachotaka kuonyesha hapa ni kwamba, maneno ‘ndugu zao’ yametumika mara nyingi sana katika Biblia. Pamoja na kwamba kuna sehemu chache ambako yametumika kumaanisha wana wa Ishmaeli, lakini kwa ujumla yanamaanisha Waisraeli wenyewe. Na uzuri ni kwamba, katika Kumbukumbu 18 hiyohiyo ambayo Waislamu wanainukuu, maneno hayo yametumika. Mungu anaeleza kuhusu kabila la Walawi kwamba watakuwa ni makuhani. Anasema: Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia. (Kumb. 18:2). Je, hapa nako akina Ahmed Deedat wanataka kutuambia kuwa hawakutakiwa kuwa na urithi kati ya Waarabu? Kwa kifupi ni kuwa nabii yule alitabiriwa kuwa angetoka kwenye mojawapo ya makabila ya Israeli na si nje ya hapo. Yesu Kristo alitoka kwenye kabila la Yuda. 
  1. Maneno ‘mfano wako wewe’
Ni kwa vipi Yesu Kristo ni mfano wa Musa? Kama nilivyosema, Mungu analeta ujumbe wa kiroho na wala si wa kimwili katika Biblia. Ufuatao ni baadhi tu ya ulinganisho kati ya Musa na Yesu: 
  • Musa aliacha maisha ya kitajiri na kifalme nyumbani kwa farao na kwenda kuishi pamoja na ndugu zake Waisraeli waliokuwa maskini na watumwa. Imeandikwa:
 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. (Waebrania 11:24-26). Yesu naye aliacha utukufu mkuu mbinguni. Imeandikwa: Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. (Wafilipi 2:5-8). 
  • Musa alitumwa na Mungu kwenda kuwatoa Israeli kwenye nchi ya utumwa wa farao na watesi wake ili kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi. Yesu alitumwa na Mungu kuja kuwatoa wanadamu kwenye utumwa wa ibilisi (farao wa kiroho) ili kuwaingiza kwenye mbingu.

  • Musa alikuwa ni mpatanishi kati ya wana wa Israeli na Mungu pale walipotenda dhambi. Maombi yake ndiyo yaliyoepusha mapigo kutoka kwa Mungu. Yesu ndiye mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Yeye huwaombea wale wanaomwamini ili hatimaye wasije kuingia jehanamu ya moto.

  • Musa aliwakomboa wana wa Israeli kutoka kwenye utumwa wa Misri kupitia sadaka ya damu. Waisraeli waliambiwa wachinje mwanakondoo wa Pasaka na kupaka damu yake kwenye miimo ya milango ya nyumba zao. Kisha Biblia inasema:

Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. (Kutoka 12:13, 23)
 Bwana Yesu naye aliwakomboa wanadamu wote kutoka kwenye utumwa wa shetani kupitia sadaka ya damu. Biblia inasema:

 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.(Waebrania 9:11-12).  
  • Musa aliwaagiza Waisraeli waokote mana iliyodondoka jangwani kila siku ili wapate kula na kuishi jangwani. Imeandikwa:
Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa … (Kutoka 16:21). Kwa kuwa hayo yalikuwa ni ishara ya mambo yajayo, alipokuja Bwana wa uzima mwenyewe, Yesu Kristo, akawa ameleta kile halisi ambacho kilikuwa kinasubiriwa. Imeandikwa: Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. (Yohana 6:31-33). 
  • Watu waliumwa na nyoka jangwani. Mungu akamwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba. Amwinue juu ili mtu aliyeumwa na nyoka akitaka kupona, ainue macho yake na kumtazama yule nyoka wa shaba. Waliofanya hivyo walipona. Walioshindwa kufanya hivyo walikufa. Imeandikwa:
 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi. (Hesabu 21:9). Yesu alipokuja naye kafanya yaleyale. Nyoka ni ishara ya ibilisi na mashetani wote. Kuumwa na nyoka ni ishara ya kuwa na dhambi. Kila mwenye dhambi anatakiwa kumtazama Yesu kwa imani, naye atapona mauti – yaani kutupwa jehanamu ya moto. Anayekataa kumtazama Yesu anakuwa amechagua kufa! Imeandikwa:

Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.(Yohana 3:14-15)
  
  • Musa alikataliwa na watu wake. Walimwambia: Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana. (Kutoka 2:14).
  •  
 Kisha aliondoka na kwenda nchi ya Midiani. Huko alioa mke ambaye hakuwa Mwisraeli. (Tazama: Kut. 2:16-21). Lakini baada ya hapo alirudi tena Misri na kuwatoa Israeli utumwani. Yesu naye alikataliwa na watu wake. Imeandikwa: Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. (Yohana 1:11). Ni jambo lililo wazi kuwa hadi sasa Wayahudi hawamtambui Yesu kama Masihi wao. Lakini kama ilivyokuwa kwa Musa, Bwana Yesu akatoka kwa hao walio wake akaja kwa Mataifa, yaani watu wengine wote wasio Wayahudi. Huko amejipatia na anaendelea kujipatia ‘bibi harusi’ – maana Kanisa la Yesu, kwa ujumla wake, linaitwa ni bibi harusi wa Bwana Yesu (Tazama 2 Wakorintho 11:2). Na tena imeandikwa: Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.(Warumi 9:25). Lakini kabla ya kuingia Kanaani (yaani dunia kufika mwisho), Bwana Yesu, kama Musa, atamrudia Israeli. Imeandikwa: Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. (Warumi 11:25-26).  
  • Musa aliteua watu kumi na mbili akawatuma Kanaani. Imeandikwa: Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila. (Kumbukumbu 1:23). Bwana Yesu naye aliteua mitume kumi na mbili akawatuma. Imeandikwa: Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri.(Marko 3:14).

  • Musa aliteua watu sabini kwa ajili ya kusimama mbele za Bwana. Imeandikwa:  Kisha Bwana akamwambia Musa, Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli, ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe. (Hesabu 11:16). Bwana Yesu naye alifanya vivyo hivyo. Imeandikwa: Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. (Luka 10:1).

  • Musa alikuwa kuhani. Imeandikwa:  Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia (Zaburi 99:6). Bwana Yesu naye ni kuhani. Imeandikwa kumhusu Yeye kwamba: bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. (Waebrania 7:24).

  • Musa aliwapa watu wake maji katikati ya jangwa. Imeandikwa: Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. (Hesabu 20:11). Yesu naye anafanya jambo lilelile. Imeandikwa:  Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.(Yohana 7:37).

  • Musa alibeba dhambi ya watu wake, hivyo akaadhibiwa yeye kwa niaba yao. Imeandikwa: Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao (Zaburi 106:32). Kila mtu anafahamu kuwa Bwana wetu Yesu naye alibeba dhambi ya ulimwengu wote. Aliadhibiwa kwa niaba yetu. Imeandikwa: Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. (Isaya 53:5-6).
  •  
 Tungeweza kuendelea zaidi na zaidi, lakini mifano hii michache inatosha kuonyesha kwamba kweli Musa alikuwa ni mfano wa nabii aliyekuwa anasubiriwa. Alikuwa ni mfano kwa sababu yeye alikuwa akitenda wajibu wake kimwili, ilhali Yule aliyekuwa anasubiriwa angeyatenda kiroho, ambalo hasa ndilo kusudi la Mungu. 
  1. Maneno ‘nitatia maneno yangu kinywani mwake’
  2.  
Nabii Yeremia anasema: Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako (Yeremia 1:9). Kwa hiyo, kama Kumbukumbu 18:18 inahusu nabii ambaye Mungu aliweka neno kinywani mwake, kwa nini tudhani kuwa ni Muhammad, ambaye ni mgeni wa mbali, na si Yeremia ambaye ni Mwisraeli? Vipi kuhusu Isaya?

Imeandikwa: Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu. (Isaya 51:16).
 Kila nabii wa kweli wa Mungu alisema maneno ambayo Mungu aliyatia ndani yake. Hayakuwa ni maneno yao waliyotunga; wala hayakuwa ni maneno waliyoenda kuyasomea kwenye shule au vyuo fulani. Yalikuwa ni maneno ambayo Roho wa Mungu alikuwa anasema kutokea ndani yao. Kwa kifupi ni kuwa, maneno haya hayamtambulishi Muhammad kamwe. Kwa nini asiwe Yeremia? Kwa nini asiwe Isaya? Lakini Bwana Yesu naye anasemaje?  Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. (Yohana 17:8). Kwa hiyo, kama ambavyo Deedat alimpa changamoto yule mchungaji kwamba Uyahudi na unabii unaweza kumhusu nabii yeyote, si lazima awe Yesu, kanuni ileile inamfunga yeye. Kuwekewa maneno kinywani kunaweza kumhusu nabii yeyote na wala huo si ushahidi kwamba anayesemwa ni Muhammad. Na haiingii akilini kwamba Mungu ambaye ametumia maelfu ya miaka kuandaa hili taifa teule aje aishie kumweka mgeni juu yao!! 
  1. Maneno ‘sina maarifa’
  2.  
Nabii Isaya ameandika kwamba: Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi (Isaya 29:12). Waislamu walipoona andiko hili wakadhani kuwa tayari wameshapata ushahidi kuwa Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia kwa kuwa Muhammad alikuwa ni mtu ambaye hakuwa amesoma. Ukifuatilia sura nzima ya 29 na mantiki iliyozaa mstari huu wa 12, unaweza kuishia kucheka tu, ingawaje hili si jambo la kucheka. Wanachofanya Waislamu ni upotovu mkubwa ambao unaangamiza mamilioni ya watu wa Mungu milele katika jehanamu ya moto. Watu wanaaminishwa uongo na wao wanaukumbatia kana kwamba ni ukweli. Kwa ujumla, ukisoma sura ya 29 ni sura ambayo inatamka hukumu juu ya Ariel (Yerusalemu) kutokana na uasi wao juu ya sheria na maagizo ya Mungu, Yehova.

Hebu tusome sura hiyo kwa karibu:
 1  Ole wa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi alifanya kituo chake ndani yake; ongezeni mwaka baada ya mwaka; sikukuu na zirudi wakati wake, 2  ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli. 3  Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke. 4  Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini. 5  Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula. 6  Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sautikuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao. 7  Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku. 8  Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni. 9  Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo. 10  Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji. Maneno yaliyo katika wino mwekundu ndizo hukumu zenyewe. Mbali na hukumu hizo hapo juu, Mungu bado akaendelea kusema kuwa, kutokana na uasi wao, hata neno lake hawatalielewa. Yaani hawataweza kusikia au kujua Mungu anasema nini hata kama watasoma au kusikia neno lake. Hii ni pamoja na wale ambao ndio wanatarajiwa kuwa wenye kuelewa neno hili – yaani manabii na waonaji – ukiachilia mbali wale wasio na maarifa juu ya neno la Mungu, yaani watu wa kawaida. Kwa hiyo, anaendelea kusema: 11  Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri; 12  kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi. Sasa basi, kama kweli Muhammad ndiye anayetajwa kwenye Isaya 29:12, kimantiki ina maana kuwa yeye ni kati ya wasioelewa lolote kwa kuwa wako chini ya hukumu ya Mungu; maana kama tulivyoona, sura hii ni tamko la hukumu ya Mungu kutokana na uasi. Si vibaya hata hivyo! Ndiyo maana nikasema kwamba unaposoma hoja hii ya Waislamu unaweza kuishia kucheka tu.

Hata hivyo, kwa kuwa sasa Muhammad ni nabii asiyeelewa chochote kutokana na kuwa chini ya hukumu ya Mungu kulingana na mantiki ya andiko hili, maana yake ni kuwa ujumbe alioleta kwa wanadamu hautoki kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Ndiyo! Labda kama, kwa makusudi tu, hutaki mantiki iliyopo. Kwa nini basi umfuate mtu wa namna hiyo?
 
*******************
 Enyi Waislamu, swali langu hapa ni moja. Kwa mtu yeyote anayependa kweli atatambua kwamba Kumbukumbu la Torati 18:18 au Isaya 29:12 hazimhusu Muhammad hata kidogo licha ya kwamba Wanazuoni wa Kiislamu kwa makundi wanajaribu kuwaambia hivyo. 

Shida moja kubwa kuhusiana na maarifa ya aina yoyote ni pale unapokuwa mtu wa kumeza tu kila unachoambiwa bila kuchunguza ukweli wa mambo. Hata haya ambayo mimi nimekuambia katika makala haya, itakuwa ni vema usiyameze tu. Fanya uchunguzi wako mwenyewe juu ya ukweli na uongo wa hoja za pande zote mbili. Kama wanazuoni wanasema kweli, basi shika kweli. Kama makala haya yanasema kweli, basi shindana na hofu yako na ukatae uongo. 

Sasa, swali langu ni kwamba, kama kweli Allah amesema kuwa Muhammad ametajwa katika Torati na Injili wakati sio kweli, hiyo maana yake nini? Kazi kwako! 

Yesu anakupenda. Njoo kwa Yesu kungali mapema. Hakuna wokovu nje ya Yesu. Jitihada zako zote unazofanya kujaribu kumpendeza Mungu wakati huna Yesu nina uhakika asilimia mia moja kuwa hujafanikiwa. Na kila unapojitahidi, unajikuta unatafunwa na hatia na hofu moyoni mwako. Hauko tayari kukiri hilo wazi, lakini huwezi kuudanganya moyo wako. Moyo wako unajua wazi kwamba umeshindwa vibaya sana! 

Na kadiri unavyozidi kumkataa Yesu, kushindwa kwako huko kuishi maisha matakatifu ndilo litakuwa fungu lako hadi mwisho. Yesu anakupenda MNO! Alikufa kwa ajili yako.

Njoo kwa Yesu sasa.

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW