
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,”
Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe?
Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe.
Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment