MSIKITI WA IJUMAA TABORA WAUZWA
Baadhi ya viongozi wa msikiti wa Ijumaa ambao ndio msikiti mkuu wa mkoa wa Tabora wametuhumiwa kula njama na kuuza msikiti huo bila kuwahusisha waumini na viongozi wenzao.
Chanzo cha kuaminika kilichopo mjini Tabora kimeiambia 100.5 Times Fm kuwa waumini waliingiwa na shaka baada kuona msikiti huo umefungwa ghafla kwa siku mbili mfululizo na kwamba baada ya kufuatilia waligunduamkuwa viongozi hao wameuuza kwa matajiri ambao ni wenyeji wa Nairobi,Kenya.
Hali ya sintofahamu ilibuka katika eneo hilo na kutokea mzozo mkubwa baina ya watuhumiwa na waumini wanaodai msikiti huo.
Imeelezwa kuwa ilimlazimu mufti kusafri haraka mpaka mjini Tabora ili kuutatua mgogoro huo.
Hadi taarifa hii inaenda hewani Mufti alikuwa akiendelea na zoezi la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo huku akihoji sababu za kufungwa kwa msikiti huo ikiwa ni kinyume cha taratibu.
Bado haijafahamika lengo la matajiri hao kuununua msikiti huo.
http://www.habari5.com/zilizopita/item/5391-msikiti-wa-ijumaa-tabora-wauzwa-kimyakimya-mufti-simba-aingilia-kati-kuunusuru
No comments:
Post a Comment