Leo ningependa kujibu hoja ambayo inaulizwa kila siku kuhusu Manabii/Mitume wa kike. Je, hawa Manabii/Mitume wa kike ni wa Kibiblia?
Biblia inatujibu kuwa Manabii wa Kike ni wa Kibiblia na zipo aya zinawaruhusu wanawake kuwa Manabii. Soma:
Yoeli 2: 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Nukuu zaidi soma 1 Wakoritho 11:5, Matendo 2:17-18, Matendo 21:9, Phl 4:3,
Baada ya kusoma hiyo aya, swali linafuata, nionyeshe Nabii wa Kike kwenye Biblia? Hili ni swali nililo ulizwa na Muislam. Bila ya kupoteza muda naweka uthibitisho wa aya.
Kutoka 15: 20 Na Miriamu, nabii wa kike, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.
Lakini kwenye imani zingine na au dini zingine kama Waislam, wao hawana Nabii wa kike kwasababu Allah wao hapendi Wanawake. Hii ndio tofauti kubwa sana kati ya YEHOVA "YAHUH" na ALLAH.
Miriam, Mtume wa Kike AU KWA KIINGEREZA TUNAMWITA "THE PROPHETESS" alikuwa dada ya Haruni "Aaron" Soma Kutoka 15:20, ni mwanamke wa kwanza kutajwa kwenye Biblia mwenye wadhifa huo wa Kitume. Hannah katika 1 Samuel 1:2 naye alifanya kazi kama Mtume na vile vile Huldah, ambaye alimtabiria Mfalme Josiah mara kadhaa. Debora katika Judges 4:5 alitajwa kama Mtume, 2 Wafalme 22:14.
Ndugu msomaji, kuna sababu kubwa sana ya mimi kuwa Mkristo, na moja ni hii ya Yehova wetu kuwa ni Mwenyezi Mungu mweye upendo na asiye bagua bagua kama yule Allah ambaye hapendi Wanawake.
SASA KAMA ALLAH NI MUNGU, NA ALLAH ANAWAPENDA WATU WOTE, KWANINI HAKUNA NABII AU MTUME WA KIKE KWENYE UISLAM?
Ndio maana huwa nasema Uislam ni dini ya kutengeneza tu.
Shalom.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment