Tangia Agano la Kale, kila aina ya kafara iliyofanyika Damu ilitumika. Ndiyo maana hata sasa, wachawi na waganga wa kienyeji wakitaka kufanya kazi zao za uharibifu huhitaji damu, aidha ya wanyama kama kondoo, mbuzi, kuku n.k.
Damu inanena / au ina uwezo wa kuongea. WAEBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.]
Yesu Kristo alimwaga damu yake kwa ajili ya ukombozi wetu – tumekombolewa na damu ya Yesu. (Waefeso 1:7; Wakol.1:20; 1 Petro 1:19; Ufunuo 5:19; Waebrania 9:12).
TABIA ZA DAMU
Damu ina uhai ndani yake. WALAWI 17:11….[Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.]….
MWANZO 9:4… [Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. 5 Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.]… Hii ina maanisha kwamba, kwa kuwa uhai u ndani ya damu, ndiyo maana wanasayansi wameshindwa kutengeneza damu, la sivyo wangeweza kutengeneza uhai pia.
Damu ina Sauti.
Damu inanena / au ina uwezo wa kuongea. WAEBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.]
Damu inaweza kulia…. MWANZO 4:10…[Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.]… Kwa hiyo Mungu alisikia sauti ya damu ya Habili ikilalamika, “Mungu nimeuawa bila sababu”. Yawezekana uliwahi kumwaga damu ya mtu, kwa kujua au kujua. Damu hiyo inalia hata sasa. Yawezekana uliwahi kutoa ujauzito kipindi Fulani. Yawezekana ulishiriki kumpa binti ujauzito na wewe ukatoa fedha ili afanye abortion (kutoa mimba). Damu zote hizo zinalia hata leo. Yawezekana ulikuwa na cheo na ukakitumi hicho cheo kwa naman ambayo mtu fualni alipoteza maisha yake kwa sababu yake.m damu ile inalia hata leo. Kwa sababu ulimwaga damu ambayo Mungu alisema nitaitaka.
Damu inaweza kutamka laana. MWANZO 4:11…[Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.]… Yamkini zipo laana zinaendelea kukupata wewe kwa sababu ya damu za aina hii. Au ipo damu iliyomwagwa na wachawi ili kukulaani wewe.
Damu ina uwezo wa kufuata. Damu yaweza kufuatilia kutoka ukoo mmoja hadi mwingineie, familia moja hadi nyingine, kizazi kimoja hadi kingine au hata taifa moja hadi jingine. MATHAYO 27:24….[Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.]…
Kwa damu yake mwenyewe Yesu aliingia mara moja tu katika patakatifu, ndio maana sisi tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, yaani, uwepo wa Mungu katika Roho. (Waebr.9:12; 10:19).
Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.
Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.
YESU NI MUNGU.
YESU NI MUNGU.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.
1 comment:
Ameni
Post a Comment