Thursday, September 29, 2016

WAISLAM WATATU WAMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUCHOMA MAKANISA, BUKOBA, TANZANIA


Hakimu Mkazi wa Bukoba, Kagera, Tanzania, Mh Victor Biambo, amewahukumu watu watatu kwenda jela Maisha kwa makosa ya kuchoma Makanisa.
Wakili wa Serikali, Emmanuel Manyere, amesema kuwa, zaidi ya kupata hiyo hukumu, Watuhumiwa hao wana makosa mengine ya ya kuua watu 20 kwa kutumia Visu ambavyo vilitumika kukata shingo zao.
Bwana Manyere amesema, watuhumiwa hao watatu ni Ally Dauda, Rashidi Mzee na Ngesela Keya, ambao wote walikiri kuwa ni Waislam, wanatuhuma ya kuchoma Makanisa zaidi ya 16 ya madhebu mbali mbali ya Kikristo mkoani Kagera.
Hakimu Bigambo alisema, ushahidi ulio tolewa na Wakili wa Serikali ulimlazimu kutoka hukumu kali, kwa jinsi ambavyo watu hao wana roho ambayo si ya kibinadamu.
Wakati huohuo, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Oliomi, ameisifia Mahakama hiyo kwa kufanya kazi nzuri ya kutoa hukumu kali kwa watuhumia ambao hawafai kushi na binadamu wa kawaida na iwe fundisho kwa watu wengine.
Zaidi ya hapo, kesi ya mauaji inayo wakabili watuhumiwa hao hao ambayo ni namba 67, bado inaendelea na imepelekwa mahakama kuu ya mkoa.
Source: Find Truth Faith

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW