Friday, September 2, 2016

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA TANO)




Mwalimu Chaka
Injili ya Barnaba ni ushuhuda pinzani dhidi ya Qur'an:
Tayari nimekwisha onyesha jinsi Kitambu hiki kilivyo na mafundisho yaliyo kinyume na Biblia Takatifu.. Yafuatayo ni baadhi ya maandiko yaliyomo katika Injili hii ya Uzushi ya Barnaba ambayo, kwa kweli pia, yanakwenda kinyume na kile kilichomo ndani ya Qur'an: Pamoja na hayo Bado Waislamu wengi Maamuma, wanashabikia kitabu hiki japo baadhi ya wasomi kama vile Sheikhy Shabir Ally wamekiri wazi kuwa Injili hii ni uzushi wa miaka ya karne ya kumi na saba. Ebu tutizame baadhi ya Aya za injili hii tukilinganisha na yaliyomo ndani ya Qurani
1. Yusufu akaenda kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, na mke
wake ambaye alikuwa na
mimba ... kuandikishwa kutokana na amri ya Kaisari. Alipo fika
Bethlehemu,
hakupata nafasi ya kupumzika kwa sababu mji ulikuwa mdogo
na wageni walikuwa wengi. Alikwenda nje ya mji mahali
ambapo wachungaji hukaa.
Wakati Yusufu alikuwa angali huko, siku za Mariamu za
kujifungua mwanawe zikatimia. Bikira alikuwa kuzungukwa na
mwanga mkali sana, NA ALIJIFUNGUA MTOTO WAKE BILA
UCHUNGU WALA MAUMIVU YOYOTE YA KUZALIWA KWA
MTOTO
( Surah 3:5-10).
Ujumbe wa Qur'an unathibitisha kwamba Mariamu alijifungua mwanawe kwa njia ya uchungu wa uzazi-kama mwanamke yoyote yule. Qur’ani inasema,

"Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. KISHA UCHUNGU WA MTOTO KUZALIWA-AKAMPELEKA KATIKA SHINA LA MTENDE. (akawa anazaa na huku) Anasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya na ningekuwa niliyesahaulika kabisa!" (Surat Maryam 19:22-23). "
Zaidi ya hayo hamna ushahidi wa Qurani wala hadithi unaomtaja Yusufu kama MUME wa Mariamu. Qurani pia haionyesi kamwe kuwa SIKU ZA KUZAA zilitimia; ila tunamwona Ruh mwaminifu ambaye tunaambiwa ni Jibril akijimithilisha kwa umbile la Mwanadamu huku Mariamu yumo upande wa Mashariki mwa Msikiti; anampa taarifa za kupata mimba na wakati huo huo anashika mimba, anaondoka mpaka chini ya mtende anazaa huko na jioni anarejea nyumani na mtoto ambaye mtoto huyu ana uwezo wa kuongea siku hiyo hiyo
QU 19:16. Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. 17. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu. 18. (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.19. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.20. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?21. (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.23. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! 24. Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!25. Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.26. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. 27. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! 28. Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. 29. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi.30. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai.31. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai.32. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.33. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.34. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
2. "Jinsi mlivyo wanyonge enyi, Wanadamu, kwa maana Mungu
amekuteuweni, kama Wana na akakupeni paradiso. Lakini
ninyi wanyonge mkaanguka chini kwa ghadhabu ya Mungu,
kwa hadaa ya Shetani, nanyi mkatolewa peponi ".
(Surah 102:18-19).
Qur'an inapinga swala la ubaba wa Mungu na kudhai kuwa jambo ili ni kashfa, inayostahili adhabu katika moto wa Jehanamu. Inatoa onyo kwa wale walio sema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mwana (Surat Al-Kahf 18:4-5).
"4. Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana. 5. Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu. 5
3.Ndoa: Injili ya Barnaba inafundisha wazo la Biblia kuhusu ndoa, kwamba ndoa inamfunga mwanamme na mwanamke sawasawa kwa pamoja:
"Mwanamme atosheke na mwanamke ambaye Muumba
wake amempa yeye, naye asahau kila mwanamke mwingine
( Sura 116:18);
"Basi Mwanamume awe radhi na kutosheka na mkewe
ambaye muumba wake amempa, na asahau kila Mwanamke
mwingine"(Surah. 115).
Wakati ambapo Qur'an inafundisha mitala na ndoa ya wake wengi ikisema,
"Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au
watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya
uadilifu, basi oeni mmoja au wawekeni (Masuria) wale
ambao mikono yenu ya kuume ya kuume imewamiliki ...
"(Surat Al-Nisaa, Wanawake '4:03).
4."Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: ‘Bwana, kuna waumini katika Jahannamu ambao wamekuwepo huku miaka sabini elfu. Iko wapi rehema yako, Ee Bwana? Nakusihi, Bwana, waweke huru kutokana na adhabu hii kali. Kisha Mungu akuamuru Malaika wanne wenye kibali zaidi kwenda Jehanamu na kuleta kila mtu ambaye ni wa dini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kuwaongozaa hadi peponi.” (Surah 137:1-4).
Aya hizi zinapingana na Qur'an, ambayo kabisa inakanusha suala la msamaha, kwa watakao kuwa jehenamu, kwa maana inasema:
"Kwa Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na
amewaandalia Moto unao waka kweli kweli na watadumu
humo milele daima; hawatapata mlinzi wala msaidizi "(Surat
Al-Ahzab 33:64-65).
Lakini pia liko fundisho la Kiislamu kuwa wapo baadhi ya Waumini wa Kiislamu ambao mwanzo wataingia Jehenamu, walipie makosa na dhambi zao kwa muda mle motoni kisha baadaye Allah atawatoa mle eti kwa kuwa walikuwa wanatamka japo shahada
5. Masihi: "Na Yesu alikiri na kusema, 'Amin nawaambieni kwamba mimi sio Masihi.' Nao wakamwuliza, `Je, wewe ni Eliya au Yeremia au mmojawapo wa Manabii wa zamani? ' Yesu akamwambia 'Hapana'. Kisha akamwambia, 'Wewe ni nani ili tupate kuwashuhudia wale waliotutuma? Yesu alisema, 'Mimi ni sauti ya
mtu aliaye katika Yudea, Mtayarishieni njia Mtume wa Bwana ". (Surah 42:5-11).
Qur'an inasema:
"Malaika alisema: Ewe Maryamu! Tazama! Mwenyezi Mungu anakubashiria Neno kutoka kwake, ambaye jina lake ni Masihi Isa, mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, ni mmoja wa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu) "(Surat Al Imran 3:45) .
Katika Sura ya 97 ya Injili ya Barnaba, ni wazi kuwa Muhammad ndiye aitwaye Masihi.. Qur'an, kama vile Biblia inampa jina hili Yesu pekee.
Ni jambo la ajabu na la kuchekeza kutambua kwamba katika utangulizi wa Injili wa Barnaba; Yesu ameitwa “KRISTO” na katika Sura ya 42 na 82 "Barnaba" anakana kwamba Yesu ni MASIHIi. Ni mtu asiye na ufahamu wa kiteolojia na mjinga kilugha anayeweza kufanya kosa kama hili; kwa sababu "Christos" ni neno la Kigiriki yaani Kiyunani ambalo kwa Kihebrania ni "Masihi".
ndugu wapendwa, Je, kuna, kwa kweli, ushahidi wa uzushi na kughushi dhidi ya Injili na Qur'an zaidi kuliko ushahidi huu? Je, kuna Muislamu ambaye anaamini huu upotoshaji kwamba Masihi ni Muhammad mwana Abdullah (s.a.w) na wala sio Bwana Yesu ?
6. Mbingu:
Qur'an inafundisha kwamba kuna mbingu saba:
“Zinamtukuza zote mbingu saba na vilivyomo ndani
yake
(Qur'an Bai Israil, Wana wa Israeli 17:44).
Hata hivyo Injili ya Barnaba inafunza ya kuwa kuna mbingu tisa;
"Kweli nakwambia kwamba mbingu ni tisa, ambazo kati yake
kumewekwa sayari, ambazo zina umbali wa safari ya mtu,
miaka mia tano moja hadi nyingine."
(Surah. 178).
Fuatilia sehemu ya 6 ambapo nitakuwa nikihitimisha mfululizo wa uchambuzi huu wa Kitabu cha Injili ya Barnaba.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW