Tuesday, September 13, 2016

ALLAH ATHIBITISHA KUWA YEHOVA NI MWENYEZI MUNGU NA NDIE ALIYE UMBA KILA KITU


Kila mtu mwenye kufuata Dini au Imani huamini kuwa Mungu ndiye muumbaji ambaye ameumba wanandamu, wanyama na vyote tunavyoviona na vile tusivyoviona. Hivi yafaa tuangalie kile kinachosemwa na Yehova kuhusu uumbaji na vile Allah anavyosema. Je, kauli zao zinapatana au zinatofautiana?
Swali kwako mfuatiliaji: Je, Allah ndiye Yehova aliye umba kila kitu?
Kuapa kwa ALLAH kuhusu viumbe:
Qurani 91:1-7 Suratul Ash-Shams (Jua): Naapa kwa jua na kwa mwangaza wake. Na kwa mwezi unapoliandama. Na kwa mchana unapolidhihirisha. Na kwa usiku unapolifunika. Na kwa mbingu NA KWA ALIYEZIJENGA. Na kwa ardhi NA ALIYEZITENGENEZA. Na kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza.
HUYO ANAYE APA NI ALLAH. TENA ANAAPA KWA ALIYETENGENEZA ARDHI NA KWA ALIYEZIJENGA MBINGU. KUMBE ALLAH HAKUTENGENEZA WALA UMBA ARDHI NA MBINGU.
Qurani 92:1-3 Suratul Al-Layl (Usiku)
Naapa kwa usiku ufunikapo (kila kitu). Na kwa mchana uangazapo. Na KWA ALIYEUMBA KIUMBE NA KIKE.
Hapa tunaona Allah anayeabudiwa na Waislamu anaapa kwa mbingu na kwa aliyezinjenga, kwa ardhi na aliyeitandaza.
Kama Allah ndie Mwenyezi Mungu, kwanini anaapa kwa mwengine? ALLAH ANASEMA: NAAPA KWA ALIYEZITENGENEZA, ALIYEZIJENGA, NK. Kwanini Allah anaapa kwa mwengine, tena huyo mwengine ndie aliye ITENGENEZA NA JENGA MBINGU NA ARDHI.
Je, huyo mtandazi wa ardhi na mjengaji wa mbingu ni nani? Qurani inaendelea kuhadithia hivi……..
Qurani 45:22 Suratur AL- Jathiyah (kiyama/ kupiga magoti)
Na mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki…
Qurani 44:7-8 Suratul Ad-Dukhan (moshi)
Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, ikiwa mnayo yakini (basi yakinisheni haya) Hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye anahuisha na kufisha. Mola wetu na ni mola wa wazee wenu (wote) wa mwanzo (na mola wa kila kitu)
Hapa tunaona kuwa Allah kupitia Qurani anasema kuwa Mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi na tena anasema hakuna aabudiwaye ila yeye. ALLAH HASEMI MIMI NIMEZIUMBA MBINGU NA ARDHI.

Mjengaji wa mbingu na mtandazaji wa ardhi anajieleza hivi ……
Isaya 44:24
BWANA, mkombozi wako yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi, “Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote, nizitandaye mbingu peke yangu, niienezaye nchi. Ni nani aliye pamoja nami?”
Mungu wetu Yehova anasema mimi ninafanya vitu vyote.
(Soma Isaya 45:6-7, 11-12, Yeremia 27:5) Bila shaka Yehova ndiye muumbaji wa vitu vyote
JE Mungu Yehova aliapia vitu alivyoviumba kama Allah?
Isaya 45:22-23
Niangalieni mimi mkaokolewe, Enyi ncha zote za dunia. Maana mimi ni Mungu hapana mwingine. Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba, mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Waebrania 6:13-16
Kwa maana Mungu alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake. akisema “Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza, Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo kwa kuyathibitisha.
Hapa tunaona Mungu wetu Yehova haapi kwa mtu wala vitu alivyoviumba kama Allah anavyoapa, bali Yehova anasema “Naapa kwa nafsi yangu”. Waweza pia kusoma jinsi Yehova alivyoapa kwa nafsi yake katika aya hizi;-(Isaya 14:24 na Mwanzo 22:16).
Leo tumejifuza kuwa Allah anaapa kwa Yehova ambaye ni Mwenyezi Mungu. Allah hakuapa kwa nafsi yake hata mara moja, bali aliapa kwa Yehova.
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW