Ndugu msomaji,
Kwenye somo letu la leo ninakuletea uthibitisho Saba (7) wa Yesu kuitwa Mungu.
Bila ya kupoteza muda tuanze kusoma aya za Biblia.
1. THOMASO ANAMWITA YESU MUNGU
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.

Baada ya Thomaso kumwita Yesu "Bwana na Mungu wangu", tunasoma kuwa Yesu anakubali na kumwabia, wewe Thomaso unameniona ndio unasadiki. Sasa Thomaso anasadiki nini? Kumbe Thomaso sasa anasadiki aliyo sema kuwa Yesu ni Bwana na Mungu.
2. YESU ANAITWA MUNGU MKUU NA WAFUASI WAKE
Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
KUMBE HATA WANAFUNZI NA WAFUASI WA YESU WALIMWITA YESU MUNGU tena MKUU. Tumesoma katika Tito Mlango wa 2 na aya ya 13 kuwa, Kristo Yesu ni Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Sasa wapi Yesu alikataa kuitwa Mungu Mkuu?
3. PETRO ANAKIRI KUWA YEYE NI MTUMWA WA YESU AMBAYE NI MUNGU WETU NA MWOKOZI WETU
2 Petro 1:1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.
Petro anajitambulisha kuwa yeye ni mtumwa wa Yesu Kristo ambaye ni Mungu wetu na Mwokozi wetu.
Kumbuka Petro aliishi WAKATI WA YESU NA ALIKUWA MMOJA WA WANAFUNZI WAKE. Kama Petro aliye kuwa na Yesu anamwita Yesu Mungu, je, wewe ni nani kupinga ukweli huu?
4. MUNGU BABA ANAMWITA MWANA - YESU "MUNGU"
Waebrania 1:8-9 8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, MUNGU, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.” ==> Baba anasema kuwa kiti cha Enzi ni cha Yesu, na zaidi ya hapo anaongeza kwa kumwita "MUNGU"
KUMBE HATA Baba aliye Mbinguni anamwita Yesu ni Mungu. Hatusomi na wala hakuna aya ambayo Yesu anamwambia Baba yake asimwite Mungu.
AYA YA 9, Mungu Baba anamaliza kabisaa kwa kusema yafuatayo "KWAHIYO MUNGU, MUNGU WAKO". Hapo teyari Mungu Baba anasisitiza kuwa MWANA NI MUNGU NA YEYE BABA NI MUNGU.
5. MALAIKA WANAMWABUDU YESU: KUMBE YESU NI MUNGU
Katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru Mtume Yohana kumuabudu Mungu tu (Ufunuo wa Yohana 19: 10). Mara nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile Malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

6. VIONGOZI WA KIYAHUDI WASEMA YESU AMEKUFURU BAADA YA KUKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU
Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu” (Mathayo 26:63). “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia, wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64) viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66).

7. WAYAHUDU WANAZIDI KUSISITIZA KUWA YESU NI MWANA WA MUNGUBaadaye mbele ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) ni kwa nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili hukumu ya kifo?
Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu. Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”
Tumesoma tena kwa ushahidi wa aya kadhaa kuwa Mungu Baba anamwita MWANA NI MUNGU, Wanafunzi wake wanamwita Yesu ni Mungu, Malaika wanasema tumwabudu Yesu ambaye ni Mungu, na Wayahudi wanasema Yesu alikufuru alipo kubali kuitwa Mwana wa Mungu na Pilato.
Kwakuwa inafahamika Yesu hakuwa na dhambi wala hakuwai tenda dhambi:
1. Je, kukubali kwake kuitwa Mungu kunamaanisha nini?
2. Kwanini Yesu hakumkatalia Thomaso pale alipomwitwa "Bwana na Mungu wangu?
3. Kwanini Petro anamwita Yesu ni Mungu wetu na Mwokozi wetu?
4. Kwanini Mungu Baba anamwita Mwana ambaye ni Yesu KUWA NI "MUNGU"
5. Kwanini Malaika wanasema tumwabudu Yesu, huku wakisisitiza kuwa anaye abudiwa ni Mungu pekee?
6. Kwanini Kuhani Mkuu alimtaka Yesu kukiri kuwa ni Mwana wa Mjungu? Je, jinu la yesu lilisababisha nini kwa Wayahudi?
7. Kwanini Wayahudi walimshataki Yesu mbele ya Pilato kuwa kajiita Mwana wa Mungu, na kufanya hivyo ni kukufuru?
Ni maombi yangu kuwa, hizi aya chache tulizo ziweka hapa zitakufungua macho na uelewe Uungu wa Yesu na kwanini Yesu hakukana kuitwa Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
No comments:
Post a Comment