ALLAH ANAULIZA KUWA, JE ALIYEUMBA NI KAMA ASIYE UMBA?
Surat An Nahl 17. Ati anaye umba ni kama asiye umba? Basi hebu, hamkumbuki?
Ndugu msomaji, hilo ni swali kutoka kwa Allah wa Waislam. Allah anataka ajibiwe, Je, aliye umba unaweza mlinganisha na asiye umba?
Ndugu zanguni, huu ni MSIBA MKUBWA sana kwa Waislam, maana Allah sasa anakiri kuwa, aliye umba hawezi kuwa sawa na asiye umba.
JE, ISA ALIWAI KUUMBA?
Ndugu msomaji wangu bilashaka umeanza kufunguka masikio kupitia Aya hiyo ya Quran katika Aya hiyo inaonekana orodha ya matendo makuu ambayo Bwana (Isa) anatangaza kuwa na uwezo wa kuyatenda bila shaka matendo hayo ikiwa umeyachunguza kwa makini, yanaonekana kuhusika na uwezo wa kiutendaji wa Mungu Mwenyezi, sasa hebu tufuatilie kwa makini.
Nukuu kwa muktasari Qur-an 3:49 Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
a) Nakuumbieni katika udongo kama sura ya ndege.
Bila shaka tendo hili hufanana fikiri na kile alichofanya Mungu pindi alipokuwa akimuumba Adamu maandiko yanaonyesha kuwa Mungu alifinyanga udongo na kumuumba Adamu vivyo hivyo Isa (Yesu) nae anafanya Uumbaji kwa kufinyanga udongo kwa sura ya ndege.
Ref: Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamuumba mwanadamu kutoka katika udongo wa ardhi
Qur-an 22:5…… tulikuumbeni kwa udongo mzee wenu Nabii Adamu ………
Hivyo Yesu anafanya tendo la Uumbaji kwa hatua zinazo fanana fika na kile alichofanya Mungu (kufinyanga udongo).
b) Kisha nampulizia mara anakuwa ndege.
Ndugu mpendwa yawezekana liletendo la kufinyanga udongo lisiwe na nguvu sana kwa wajenga hoja , lakini hapa ndipo panapo nishangaza zaidi Qur-an inapoonyesha wazi kuwa Isa aliweza kupulizia udongo nao ukapata uzima na kuwa kiumbe hai.
Wanasayansi huu ndio uumbaji na wanabaiolojia wamejitahidi kuumba na kutengeneza mtu lakini wamegonga mwamba inapofikia hatua ya kumfanya kuwa kiumbe hai, aweze Kutembea, Kunusa, kuona n.k
Lakini maandiko ya Qur-an ufunua siri hii ya ajabu, bilashaka tendo hili la kupuliza pumzi na kitu kikawa hai ndiyo uleta maana halisi ya Uumbaji na hili ndilo tendo linaloleta maana na uzito haswa unaofanya tendo hilo kuwa rasmi na kumhusu Mungu pekee.
Mafunuo ya Qur-an huonyesha kuwa tendo hilo haswa ndilo alilotenda Mungu alipokuwa akimuomba Adamu nalo ni tendo la kutoa uhai (Maisha) kwa kuomba.
Qur-an surat 15:28 Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
Tunajua fika juu ya tabia ambazo Mungu umshirikisha mwanadamu na pamoja na ha yo zipo zile ambazo Mungu kamwe hawezi kumshirikisha mwanadamu, lakini katika andiko hilo tunaona Yesu akitenda kazi hiyo kuu yenye uhusiano kwa asilimia miamoja na uwezo wa Kiuungu bilashaka huyo Yesu anayo asili inayopita ubinadamu aliokuwa nao na siyo asili ya kawaida.
Je! Mbona Qur-an inasema aliumba kwa idhini ya Mungu?
Inawezekana ndugu msomaji wangu ukawa na swali la namna hiyo ndani ya moyo wako hebu niruhusu sasa niweze kuondoa mashaka uliyonayo.
Inawezekana ndugu msomaji wangu ukawa na swali la namna hiyo ndani ya moyo wako hebu niruhusu sasa niweze kuondoa mashaka uliyonayo.
Je! Neno kwa idhini humaanisha nini?
Katika tafsiri ya kawaida Neno “Idhini” humaanisha “ruhusa” au “Ukubali”
Katika tafsiri ya kawaida Neno “Idhini” humaanisha “ruhusa” au “Ukubali”
Hivyo Qur-an inapomnukuu Nabii Isa akisema kwa “idhini” inaleta maana tu ya ukubali, ruhusa toka kwa Mungu.
Swali:- je kwanini apewe ruhusa na hali yeye ni Mungu? Au Je kuna miungu wangapi?
Jibu:- katika mafunuo ya Biblia mara kadhaa Bwana Yesu ametumia kauli hiyo ya kuruhusiwa au kukubaliwa na Mungu (eg: Yohana 5:30) mara kadhaa Yesu alisema “ninenalo si neni yaliyoyangu nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo”
Kwanini aseme hivyo (kwa idhini)?
Kwa msingi ujio wa Yesu hapa Duniani ulimlazimu kufunika uwezo na mamlaka yake ya asili ya Kimungu, ilimpasa kumwelekeza mwanadamu kwa vielelezo hai vya kimwenendo, hali na mazingira hayo yalimfanya kujipa cheo cha chini mara kadhaa alipozumngumza na watu.
Kwa msingi ujio wa Yesu hapa Duniani ulimlazimu kufunika uwezo na mamlaka yake ya asili ya Kimungu, ilimpasa kumwelekeza mwanadamu kwa vielelezo hai vya kimwenendo, hali na mazingira hayo yalimfanya kujipa cheo cha chini mara kadhaa alipozumngumza na watu.
Rejea Qur-an 20:9-11 Mungu alijifunua kwa Musa kupitia kichaka cha moto bila shaka alichukua ufinyu huo ili kuwa Asili na mwanadamu.
Pamoja na hayo Bwana Yesu akuadhimu mara chache kufunua taratibu mamlaka aliyonayo kiasili, mfano ni pale aliposema.
Yohana 10:30 mimi na Baba tu umoja.
Kauli hiyo iliwafunulia mafarisayo juu ya mamlaka ya Yesu ya Kimungu, lakini haikuwa jambo rahisi kwao kukubaliana na hilo
na katika aya hiyo tunaona wakiadhimu kumpiga mawe kwa kujiita yeye ni Mungu.
Kauli hiyo iliwafunulia mafarisayo juu ya mamlaka ya Yesu ya Kimungu, lakini haikuwa jambo rahisi kwao kukubaliana na hilo
na katika aya hiyo tunaona wakiadhimu kumpiga mawe kwa kujiita yeye ni Mungu.
Bilashaka Yesu alitambua saikolojia ya imani ya watu hao anaowajua hata mioyo, hivyo Yesu aliamua kushuka kwa kumtaja Mungu wanayemdhani kama Mungu aliye ng’ang’ana Mbinguni tu lakini kwa hakika hiyo ndiyo asili yake binafsi.
Ndiyo maana alisema kwa Idhini.
Katika wazo hilohilo ndiyo maana Yesu Utumia neno kwa “Idhini”alipenda watu watambue mamlaka yake katika utendaji wake zaidi kuliko katika maneno yake
Katika wazo hilohilo ndiyo maana Yesu Utumia neno kwa “Idhini”alipenda watu watambue mamlaka yake katika utendaji wake zaidi kuliko katika maneno yake
Hata hivyo neno kwa “Idhini” halimaanishi kwa “uwezo” Idhini na uwezo ni mambo mawili yanayo tofautiana sana
Mfano:- wewe unaweza kupewa Idhini ya kuhubiri lakini usiweze (usiwe na uwezo ) wa kuhubiri hivyo idhini( ruhusa ) na uwezo nitofauti kulingana na maandiko tabia ya Yesu ihusuyo Uumbaji uonekana akiwa nayo katika asili (Yohana 1:1-3) hivyo ni tabia ya kiuwezo na mamlaka yake ya Kimbinguni kabla ya kujishusha na kuvaa ubinadamu (nitalieleza mbele kwaupana ) na kuja hapa duniani.
Neno idhini Isa (Yesu) analitumia anapo kuwa hapa Duniani kama sehemu ya hatua yake ya kujishusha na kutwaa ubinadamu kwaajili ya kuokoa, lakini bado tendo la uumbaji linarejea asili na mamlaka yake kama Muumbaji na si wa ndege tu bali Dunia kwa ujumla (Yohana 1:1-3)
Qur-an inampa cheo gani (Isa) kwa tendo la Kuumba?
Uandishi au kuchapaji mwandishi na mengineyo ya kimsingi.
Qur-an 16:17 …….Ati yeye aliyeumba (naye ni Mwenyezi Mungu) atakuwa sawa na wale wasio umba je hamkumbuki?
Andiko hilo la Qur-an linasema kuwa
– “Ati yeye aliyeumba (Mungu) atakuwa sawa na wasio umba”?
– “Ati yeye aliyeumba (Mungu) atakuwa sawa na wasio umba”?
Jibu :- la” aliyeumba hawezi kuwa sawa wasioumba bali aliye umba anakuwa sawa na aliyeumba hivyo ikiwa Yesu aliumba je yeye ni nani?
Qur-an kamwe haimpi sifa au usawa kiumbe yeyote asiye na sifa inayohusika na Mungu, maana sifa inayomhusu Mungu haswa ile ya kuumba ndiyo humfanya Mungu kuitwa Mungu kamwe hawezi kupewa Mwanadamu.
Pamoja na hayo jambo la kushangaza ni pale Qur-an inapoo nekana kuweka wazi kuwa Nabii “Isa Ibn Mariam” naye alikuwa na sifa hiyo inayo mhusu Mungu maana naye aliweza kuumba
(rejea neno nakuumieni Qur-an 3:49)
(rejea neno nakuumieni Qur-an 3:49)
Na kutokana na kile kichosemwa na aya tuliyoisoma punde Nabii Isa anaonekana kuwa sawa na Mungu au kwa lugha rahisi naya ufupi yeye ni Mungu Muumbaji aliye adhimu kuvaa ubinadamu, lakini ana mamlaka inapita huo ubinadamu (yeye ni neno, muumbaji).
Ndugu msomaji, leo tumejifunza kwa mara nyingine tena kuwa Yesu ni Mungu kwasababu aliumba Quran Sura 16 aya ya 17.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
No comments:
Post a Comment