Abuu kwenye ubatizo wa maji mengi chini ya kanisa la EAGT Mito ya Baraka, Dar es Salaam |
1. ABATIZWA NA SASA ANAITWA BOAZ
2. BABA YAKE ANAYEISHI OMAN AKIRI KUWA MUNGU WA "ABUU" HAKIKA NDIE MUNGU MKUU
3. ABUU SASA ANAMTUMIKIA YESU
Ndugu msomaji,
Bwana Yesu apewe sifa,
Haya msomaji wetu karibu katika kipengele chetu maalumu ''USHUHUDA'' ambacho kinakujia kila siku kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutokea lakini yawezekana hauijui pia yawezekana ilitokea ukawa unaijua lakini labda umesaihau.
Abuu Levy au waweza kumuita kwa jina la Boaz kama wengi walivyomzoea, ni jina ambalo amelipata baada ya ubatizo. Historia yake inarejea kwenye Uislamu, ambako ndipo alilpotokea, asili yake akiwa Muarabu. Baba yake mzazi anaishi Oman hadi hivi sasa.
Kwa taarifa yako, licha ya kukulia kwenye famlia ya usilamu, lakini hakuwai si tu kwenda msikitini, bali pia hata mazingira ya ndani ya msikiti anayafahamu yalivyo. Neema imetokana pale alipolelewa na mama yake mkubwa ambaye ni "mlokole".
Alipotimiza umri wa miaka kumi, Abuu alikata shauri na kuokoka. Lakini pamoja na baba yake mzazi kuwa Shekhe wa imani kali ya Kiislam, hakuleta kipingamizi chochote zaidi ya kumsihi tu kuwa asimuache Mungu, yaani Yesu Kristo. Hii ni tofauti na wazazi wengine wa Kiislam ambapo huleta vita kwa mwanao na hata kutishia kifo.
Pamoja na kupewa baraka na baba yake mzazi ambaye ni Muislam mwenye siasa kali, bado hali haikuwa nyepesi kwa baadhi ya ndugu zake, kwani Abuu amepitia magumu mengi, kuotka ndugu zake ambao takribani wote ni Waislam kwa kumtishia maisha yake na kusema maneno makali yenye laana kwasabu ya kubadili dini na kuwa Mkristo. Hata hivyo Abuu alisimama ndani ya Yesu na hakukuwa na kurudi nyuma. Abuu sasa anamtumikia Yesu kwa kuimba Nyimbo za Injili. Tumeweka linkhttps://www.youtube.com/watch?v=sFu6socEVMQ ya nyimbo zake. Tafadhali nunua CD'S/DVDS zake ili kuendelea kuimarisha kazi yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Abuu, mwenye umri wa miaka 24 kwa sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa muda wa miaka nane huku akiwa na album tatu hadi sasa, kati yake mbili zikiwa madukani tayari.
Mungu huandaa na kubadilisha watu wake kwa njia mbalimbali, maana ametujua tangia hatujazaliwa. Naye Abuu yuko kwenye kazi/huduma ya Mungu. Yuko katika utumishi wa Yehova.
Mungu akubariki sana msomaji wetu, tuendelee kuitangaza Injili ya Yesu Kristo kwa Mataifa Yote.
Mungu anawapenda wote na tusikate tamaa hata tunapo kuwa katika magumu, mateso, Yesu bado anatupenda na yupo pamoja nasi kila siku.
Mungu awabariki sana.
By permission
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 1, 2016
April 1, 2016
No comments:
Post a Comment