Ndugu msomaji,
Kama Quran imekamilika kama jinsi Waislam wanavyo dai, kwanini Muhammad alifuta mistari kwenye kitabu cha Allah?
Kama Quran ni maneno ya Allah, je, nani alimpa mamlaka Muhammad kufuta aya za Allah?
Je, hii Quran imekamilka au haijtakamiliak, maana sasa tunafahamu kuwa kuna aya zilifutwa na Muhammad bila ya ruhusa ya Allah.
Huu ni Msiba. Soma ushahid hapa chini.
"Baada ya hapo, Mungu alitufunulia mstari uliokuwa miongoni mwa ile iliyofutwa baadaye." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.416 uk.288.
"Anas bin Malik alisimulia: ... Walifunuliwa wale waliouawa Bi’r-Ma’una, mstari wa Kurani tuliozoea kuukariri, lakini badaye ulifutwa. Mstari wenyewe ulikuwa: ‘Wafahamishe watu wetu kuwa tumekutana na Bwana wetu. Amefurahishwa nasi na ametufurahisha.’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 19 na.69 uk.53. Tazama pia Historia ya al-Tabari juzuu ya 7 uk.156.
Kumbukumbu nyingine za mistari iliyofutwa ni Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 8 na.57 uk.45, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 184 na.299 uk.191, na Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.421 uk.293 zote zinarudia kitu hicho hicho kuhusu mstari huo huo.
Wakati fulani Muhammad aliafikiana na kusema kuwa kuhusiana na mabinti wa Allah kwenye Sura 53:19 "sala ya ya kuombea ilipaswa kutumainiwa." Muhammad alisema tunapaswa kutegemea msaada wa sanamu hizi tatu.
Wafuasi wa Muhammad walishangazwa kuwa amesema hivi. Baadaye, Muhammad alibadilisha msimamo wake na kusema kuwa Shetani alimdanganya. Mistari hii ilibatilishwa au kutolewa. Wanazuoni wa Kiislam wanaiita mistari hii "aya za Shetani." Inafurahisha kusoma maelezo ya Waislam kuhusu namna ambayo nabii wa kweli angeweza kusema hivi.
MASWALI:
1. Kwanini Allah aliruhusu Shetani kumdanganya Nabii wake?
2. Kama Muhammad aliweza kudanganywa na Shetani, je, tutaiamini vipi Quran ambayo imejaa shaka?
3. Je, kuna aya ngapi ambazo ni za Shetani kwenye Quruan, ikiwa sasa tunafahamu kuwa, Shetani na yeye alikuwa anateremsha aya zake kwa kupitia Jibril huyo huyo?
4. Kwanini Waislam wanakataa ukweli wa Mabinti wa Allah ambao Muhammad aliuukubali?
5. Kwanini Muhammad alishindwa kutofautisha maneno ya Allah na Shetani na kudhani ni mtu huyo huyo anasema?
1. Kwanini Allah aliruhusu Shetani kumdanganya Nabii wake?
2. Kama Muhammad aliweza kudanganywa na Shetani, je, tutaiamini vipi Quran ambayo imejaa shaka?
3. Je, kuna aya ngapi ambazo ni za Shetani kwenye Quruan, ikiwa sasa tunafahamu kuwa, Shetani na yeye alikuwa anateremsha aya zake kwa kupitia Jibril huyo huyo?
4. Kwanini Waislam wanakataa ukweli wa Mabinti wa Allah ambao Muhammad aliuukubali?
5. Kwanini Muhammad alishindwa kutofautisha maneno ya Allah na Shetani na kudhani ni mtu huyo huyo anasema?
MABINTI WA ALLAH
Uarabuni kabla ya Muhammad, kabila la Muhammad, Quaraysh, lilimwamini Mungu aitwaye Allah (au Al’Ilah) aliyekuwa na mabinti watatu walioitwa Al-Lat, Al-Uzza, na Manat.
" ‘Urwa alisema, ... kuhusiana na Ansar aliyezoea kumdhania Ihram kuwa anaabudu sanamu anayeitwa ‘Manat’ ambaye walizoea kumwabudu kwenye sehemu iliyoitwa Al-Mushallal..." Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 26 (Hija) sura ya 78 na.706 uk.413.
"Mstari huu ulifunuliwa kwa kuhusiana na Ansar aliyekuwa anamdhania Ihram kuwa sanamu Manat ambaye aliwekwa karibu na sehemu iliyoitwa Qudaid..."Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 27 (‘Hija ya Umra) sura ya 10 na.18 uk.11. Al-Lat, Al-Uzza wameelezewa Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 74 (Kitabu cha Kuomba Ruhusa ya Kuingia) sura ya 52 na.314 uk.209; juzuu ya 5 na.375 uk.259
Hakika Quran sio kitabu cha Mungu na kimejaa shaka kubwa kubwa.
Leo tumejifunza tena kuwa Quran sio kitabu cha Mungu, na zaidi ya hapo, Allah alikuwa na Mabainti watatu.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba
For Max Shimba Ministries
No comments:
Post a Comment