Ndugu msomaji,
Katika somo hili, nitajibu hoja ya Mashahidi wa Yehova kuhusu kupinga kwao Utatu Mtakatifu wa Mungu.
Taasisi ya Mashahidi wa Yehova wanafundisha kuwa kuna nafsi moja tu katika Uungu naye ni Baba tu. Ikimaanisha kuwa, wanapinga Uungu wa Yesu na wanapinga Uungu wa Roho Mtakatifu.
Mafundisho ya Biblia:
1. Je! Yesu ni yule Mungu mmoja?
Musa alisema: “Sikiliza, Ee Israeli: Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja,” Kumbukumbu ya Torati 6:4
Musa alisema: “Sikiliza, Ee Israeli: Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja,” Kumbukumbu ya Torati 6:4
Lakini katika Injili kutokana na Yohana Yesu anasema yafuatayo: Yesu alisema: “Mimi na Baba tu umoja,” Yohana. 10:30.
Mtume Paula alisema, “Maana katika yeye (Yesu) unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili,” Wakolosai 2:9.
Sasa Mashahidi wa Yehova wanafundisha kuwa kuna nafsi moja na ni Yehova.
Lakini hapa kwenye Wakolasai 2: 9 tumeona nini? Tumeona kwamba wako wawili sasa [kuna Mungu Baba na kuna Yesu ambaye kuna utimilifu wote wa Mungu]. Lakini JE, kuna wawili tu? La hasha! Mafundisho ya Biblia yaliyo wazi sana yanasema.
Soma: 1 Yohana 5:8, “Kwa maana WAKO WATATU washuhudiao mbinguni, BABA, na NENO, na ROHO MTAKATIFU, na watatu hawa ni umoja.”
Tazama, neno la Mungu lasema kuwa WAKO WATATU MBINGUNI, na nafsi hizi tatu hufanya Uungu ule mmoja. Na maana ya kusema hayo ni sawasawa na maana yake aliposema kuwa duniani kuna “Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” mst. 9. Na tunaelewa kwamba roho, maji na damu sio kitu kimoja kiasili. La, bali umoja wao ni ushuhuda wanaotoa kuhusu Yesu. Vivyo hivyo, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu ni nafsi tofauti tatu wanaomshuhudia Yesu kuwa Mwana wa Mungu. Kuna Mungu mmoja tu, walakini ana nafsi zake tatu. Yesu aliposema, “Mimi na Baba tu umoja,” hakuwa na maana kuwa Yeye mwenyewe ndiye Baba.
Tena tuangalie 2 Wakorintho. 13:14, maneno hayo ya Biblia yaonyesha kuwa Uungu ni wa nafsi tatu. Sasa tuchunguze kwenye Biblia maana ya “Umoja” walio nao Baba na Mwana.
Waefeso 5:29-32, “Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitndea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili moja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi na nena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.”
Mst. 30 - “Tu viungo vya mwili wake”.
Mst. 31 - “Hao wawili watakuwa mwili moja.”
Mst. 31 - “Hao wawili watakuwa mwili moja.”
Tazama:
1) Kanisa ni mwili ule mmoja wa Kristo. Sasa maana ya maneno hayo ya Waefeso. 5 ni kwamba kanisa ni mtu mmoja tu. Je, Petro, Paulo, Apollo, Barnaba, Timotheo, Tito na Yohana wote walikuwa mtu mmoja tu? La, mtume mwenyewe alisema kuwa ni Viungo vya mwili ule mmoja. Kanisa ni watu mbalimbali tofauti wanaounganishwa washiriki umoja wa kiroho. Wanashirikiana katika baraka na kazi za Yesu. Vivyo hivyo, Yesu na Baba wa umoja, hata ingawa ni wawili.

2) Pia mistari hii inasema mume na mkeo ni mwili mmoja tu! Je, kweli hawa wawili ni mwili mmoja?
Hapana. Lakini wale wawili ni umoja katika kazi na baraka za ndoa? Vivyo hivyo Yesu, Baba na Roho ni mmoja; hata ingawa ni watatu.
Yohana 17:20-21 “Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako: hao nao wawe ndani yetu.”
Je, umoja ambao Yesu alituombea ni kwamba Wakristo wote wawe mtu mmoja tu? Si anaongea habari ya umoja wa matendo, imani, na maneno yetu? Kama vile Yesu na Baba wanao umoja katika kutuumba na kutuletea wokovu, vivyo hivyo Wakristo wawe na lengo moja na juhudi moja. Tuone mfano mwengine wa umoja katika Biblia. 2 Samweli 7:23, “Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israeli...?”
Waisraeli walikuwa watu wengi na makabila mengi lakini wanaitwa kuwa ni taifa moja tu! Vivyo hivyo, Uungu ni mmoja, lakini una nafsi tatu.
2. Matatizo ya kusema kuna nafsi moja tu.
Yohana 17:1-5, Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza dunia, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa nifanye. Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.”

Sasa kama Mungu ni nafsi moja tu, na Mungu alikuja ulimwenguni katika mwili na aliitwa Yesu. Sasa huyo Yesu (Kama nafsi pekee) alikuwa ana ongea na nani hapa? Mbona alisema, Wakujue wewe, Mungu wa pekee, na Yesu Kristo uliyemtuma. Akiwa yeye (Yesu) alikuwa nafsi pekee sasa nani alitumwa huyu?
Kwa hiyo tumeona Baba na Mwana ni nafsi mbili tofauti. Na wana umoja katika kazi zao na asili yao ya Uungu.
Soma Yohana 14:9-10, “Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.”
Sasa wakati Yesu alisema “Siyasemi kwa shauri langu”. Sasa ameyasema kwa shauri la nani? Akiwa ninafsi pekee, ni nani aliyempa maneno ayaseme? Yesu tena alisema, “Mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu.” Sasa hakusema Yeye ni Baba! Lakini alisema Baba yu ndani yake! Kwa hiyo 1 + 1=2!
Kumbe!
Yohana 14:26, “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”
Tazama 1+1+1=3. Wako Watatu! Roho Mtakatifu atakayepelekwa na Baba kwa jina
la Yesu! Pia angalia mistari hii:

1 Wakorinth 11:3; 1 Wakorintho 15:24-28; 1 Timotheo 2:5; Marko 13:32; Mathayo 27:46; Luka 23:46-47.
HIVYOBASI, TUMEJIFUNZA kuwa kumbe wako Watatu, tena hao watatu wapo Mbinguni: 1 Yohana 5:8, “Kwa maana WAKO WATATU washuhudiao mbinguni, BABA, na NENO, na ROHO MTAKATIFU, na watatu hawa ni umoja.”
Baada ya kusoma huu ujumbe, sasa jiulize maswali yafuatayo:
MASWALI YAKINIFU:
Je, Yesu na Baba ni UMOJA – Yohana Mlango wa 10 aya ya 30?
Je, UMOJA maana yake ni MMOJA?
Je, Yesu ni UKAMILIFU WA KIMWILI WA MUNGU – Wakolosai 2”9?
Je, UNAKUBALINA NA: 1 Yohana 5:8, “Kwa maana WAKO WATATU washuhudiao mbinguni, BABA, na NENO, na ROHO MTAKATIFU, na watatu hawa ni umoja.”?

Namaliza kwa kusema kuwa, hoja ya Mashahid wa Yehova kupinga UTATU MTAKATIFU wa Mungu ni dhaifu, maana 1 Yohana 5:8, “Kwa maana WAKO WATATU washuhudiao mbinguni, BABA, na NENO, na ROHO MTAKATIFU, na watatu hawa ni umoja
Ni maombi yangu Mungu ayafungue macho ya Mashahidi wa Yehova kwa ukweli wa injili na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
No comments:
Post a Comment