Ndugu msomaji,
Leo nitajibu hii hoja kuitunza siku ya Sabato katika Ufalme
Mpya wa Mungu. Hebu tusome kwanza aya wanazo zitumia kusaidia hoja ya Sabato
katika Ufalme Mpya wa Mungu.
ISAYA 66: 22-24
22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya,
zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu
litakavyokaa.
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Wasabato-SDA wamekuwa wakitumia aya ya 22 na 23 ya Isaya Sura ya 66
kuwa Sabato ni ya milele. NUKUU “22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya,
zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu
litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata
sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.”
Hoja hapa inakuja kwasababu katika
hizi aya pamezungumzia pia Mbingu Mpya na Dunia Mpya, ambazo zimetajwa vile
vile na Yohana katika kitabu cha Ufunuo, kwamba tutakuwa tunatunza Sabato.
Lakini ikumbukwe kuwa katika aya hizi hizi pamesemwa vile vile kuhusu “MWEZI
MPYA” Sasa kifikra lazima tujiulize swali hili: Je, kwanini hatutunzi siku ya
MWEZI MPYA? Je, tutakuwa tunatunza MWEZI MPYA katika Dunia Mpya na Mbingu Mpya?
Swali la Kwanza nimeliweka na
limekuja kwababu ya wazo yakinifu la Mwezi Mpya kuwepo pamoja na Sabato katika
aya ya 23.
Sababu ya Wasabato kutumia hizi aya “22-23”
ni kulinda dai au hoja yao ya kuitunza Sabato sasa na baadae. Hili ni kosa,
kwasababu Isaya 66: 22-23 haizungumzii kuitunza Sabato sasa, LASIVYO, inatubidi
kuitunza na siku ya MWEZI MPYA, sasa. Je, Wasabato wanaitunza siku ya MWEZI
MPYA?
Swali la
pili ni la kushangaza kidogo, na kuna mambo kadhaa ya muhimu lazima tuyawekee
umaanani. KWANZA: Neno ambalo ni tafsir ya “mwezi mpya” katika Kihebrania ni “CHODESH”
likimaanisha MWEZI. Hili neno halikuwa na maana ya watu washerekee MWEZI MPYA.
Kwa mara ya kwanza lilitumika katika Kitabu cha Mwanzo 7 aya ya 11. , likiwa na
tafsir ya “Mwezi”, zamani zaidi kabla ya chodesh kuwa sikukuu ya Wayahudi katika
taifa la Israel.
Zaidi ya
hapo, neno “mbingu mpya” na dunia mpya” linatupa mwanga kuwa mpango wa Mungu ni
kurejesha kila kitu kama ambavyo alitaka kiwe kabla ya dhambi kuingia duniani
kama ilivyo semwa kwenye Sura mbili za kitabu cha Mwanzo. Mfalme mwenye hekima anatuambia kuwa Mhubiri
3: 14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele;
haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili
watu wamche Yeye.
Na katika Sura ya kwanza ya Mhubiri 1: 4 inasema: 4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
Iwapo unaamini kuwa Dunia itakuwa
milele au la, hapa jambo la muhimu ni hili” Mungu atarejesha kila kitu na kuwa
sawa kama pale mwanzo kabla ya dhambi kuingia duniani”
Matendo ya Mitume 3: 20-21 inasema: 20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
Kwa maneno mengine, kila kitu
kitarudishwa na kuwa thabiti kama pale mwanzo. Ushahidi zaidi ni yale maono ya
Yohana ya Mbingu Mpya na Dunia Mpya. UFUNUO 22. Utagundua hata Mti wa Uzima ambao
wakati Fulani ulikuwa katika Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:9), umetajwa hapo.
Ufunuo 22:2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule
mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa
matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Hapo mwanzo tumekutana na mambo
mengi, moja wapo ikiwa ni Siku ya Saba Sabato (Mwanzo 2:1-3). Ndio maana
hatushangai kuwa, Nabii alisema kuhusu Sabato bado ipo hata baada ya dhambi
kuingia, kwa marejesho ya kila kitu ikajumlisha na mwanzo wa Siku ya Saba. Hata
hivyo, tunasoma kuhusu jinsi dunia ya kwanza katika Mwanzo 1 na 2, na hatusomi
kitu chechote kile kuhusu shereza za MWEZI MPYA. Haikutajwa hiyo sherehe
kabisa, je, hii ni kwanini? Jibu lako utalipata katika Ufunuo 22: 2
Ufunuo 22: 2 inasema: katikati ya njia
kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao
matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya
mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Kumbuka kuwa neno la MWEZI MPYA linamaanisha “mwezi” na
tunapo linganisha maneno ya Isaya na ya Yohana, tunajifunza kuwa maneno ya
mwezi mpya kwa mwezi imaanisha ni mkusanyiko wa Watakatifu, mara moja kwa
mwezi, kwasabu ya kula mti wa uzima. Hivyo, jibu kwa swali letu kama Mwezi Mpya
utakuwepo katika dunia mpya, jawabu ni NDIO.
Ingawa sababu ya kukutana katika mwezi mpya ni kula mti wa uzima. Hivyo,
sababu ya kusherekea Sabato itabadilika na sio kusherekea kila wiki kama ilivyo
semwa katika Kutoka 20:11, Hapa
tutasherekea kuumbwa kwa dunia mpya, ndio maana Isaya alisema kuhusu MBINGU
MPYA na DUNIA MPYA –AMBAYO NITAIFANYA
Isaya 66:22.
Isaya aliona mwezi mpya katika maono yake kama
marejesho ya kila kitu katika ukamilifu wake, hususan Yerusalemu, na tunajua
kuwa kutakuwa na Yerusalemu mpya. Kuona kwake kwa mwezi mpya au mwezi, ni
sambamba na Yohana alipo ona kurejeshwa kwa mji (Ufunuo 22:20) hii ndio maona
ambayo Isaya aliyaona katika aya ya 22-23 ya Sabato ya uumbaji, pamoja na
kukutana kwa watakatifu wote, mara moja kwa mwezi, kufurahi na Bwana na kula
Mti wa Uzima.
HOJA:
Sasa tuendelee na aya ya 24 ya Isaya 66 inasema 24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi;
maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni
pa wote wenye mwili.
Hii aya inaweza kujibu zaidi hoja ya SDA, KATIKA AYA YA
15 ya Isaya 16, INATUAMBIA KUWA Bwana Mungu “Maana Bwana atakuja na moto, na
magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake
kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Na katika aya ya 16 anasema Kwa
maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao
watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.
Wakristo wengi wanaamini kuwa hizi aya
zinazungumzia kuja kwa Bwana kwa mara ya pili, au kuja kwa Bwana na watakatifu
wakati wa Milenium.
Je, kwanini hatutunzi siku ya MWEZI
MPYA?
Je, tutakuwa tunatunza MWEZI MPYA katika
Dunia Mpya na Mbingu Mpya?
Je, Adam na Hawa walisherekea Sabato?
Hivyo basi, leo tumejifuza kidogo
kuhusu Isaya 66 aya ya 22 na 23 na kijibu hoja ya Wasabato kuhusu umilele wa
kuitunza Sabato.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba
For Max Shimba Ministries Org.
No comments:
Post a Comment