(SEHEMU YA PILI)
Ndugu msomaji:
Katika ujumbe wa leo, nitawaletea ushahidi mbali mbali unao sema na au mruhumsu Mkristo kusali Jumapili kama ulivyo wekwa na shahidiwa katika Agano Jipya.
Ushahidi wa kubadilika kwa siku ya kusali unaweza kuuona mapema sana katika Agano Jipya. Agano Jipya lina ushahid mwingi sana ambao unasema kuwa SIKU YA SABATO haina nguvu tena na au si Sheria tena kusali Siku ya Saba ya Wiki.
SIKU ZOTE NI ZA BWANA MUNGU
Warumi 14: 5-6 inasema: 5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Ni vyema kuisoma Sura nzima ya Warumi 14, ingawa kuna ushahid mkubwa kuanzia aya ya 1 mpaka ya 12. Hata hivyo, maelekezo hapa ni kwa mtu binafsi kuamua katika akili yake ni siku ipi aitunze na au aitumie kusali na kumwabudu Bwana Mungu. Kwasabau hiyo, basi chaguo ni la Mtu na sio Mungu.
SABATO IMESEMWA NI KIVULI. YESU NDIE SABATO
Wakolosai 2: 16-17 inasema: 16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Angalia kwa makini hapa jinsi siku zilivyo orodheshwa. Sikukuu huwa ni ya Kimwaka, Mwandamo wa Mwezi ni ya Kimwezi, Sabato ni ya Kiwiki. Hakuna mwenye ruhusa ya kuhukumu katika hili. Sabato imesemwa ni KIVULI. Ukweli kamili ni Yesu. Yesu ndie Sabato yetu.
WALIKUTANA SIKU YA KWANZA YA JUMA
Matendo ya Mitume 20 aya 7 Inasema: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Siku ya Kwanza ya Juma ni Jumapili, na hii ni siku ambayo watu walikusanyika na Kumwabudu Bwana Mungu. Hivyo basi, hii aya inaweza kuonyesha kuwa Kanisa lilikutana/kusanyika siku ya Jumapili.
Katika mkusanyiko huu, kuna mambo Mawili Muhimu sana yalifanyika:
1. Walimeka Mkate -Kula Meza ya Bwana. [Communion]
2. Walisoma Neno.
Zaidi ya hapo, Luka hakutumia njia ya Kiyahudi katika kuhesabu siku, yaani kutua kwa jua mpaka kutua kwa jua. Luka alitumia njia ya Kirumi ambayo siku inaanza Saa Sita ya Usiku. [midnight to midnight.] Huu ni ushahidi tosha kuwa Luka hakutumia na au hesabu siku kwa kutumia Njia ya Kiyahudi ya kuhesabu Sabato.
PAULO ANALIAMBIA KANISA LIKUTANE SIKU YA KWANZA YA JUMA
1 Wakorintho 16: 1-2 inasema: 1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
Ona hapa Mtume Paulo analiambia Kanisa likutane siku ya kwanza ya Juma ambayo ni Jumapili na aliwataka waweke akiba katika siku hiyo ya kwanza ya Juma.
Hivyo basi, siku ambayo Kanisa liliambiwa likutane ni Jumapili. Je, hii ni siku ya kisheria ya Mkristo kukutana? Jibu ni lako na uchaguzi ni wako.
YOHANA ALIKUWA KATIKA ROHO SIKU YA BWANA
Ufunuo 1 :10-11 inasema: 10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Katika Kamusi ya Biblia kuhsu "SIKU YA BWANA" katika Ufunuo 1:10. hii ni tukui la kwanza katika maandishi ya Kikristo kuwa watu wakuna siku ya kwanza τῇ κυριακῇ ἡμέρᾳ, "ta kuriaka hamera." Hii ni uthibitisho kuwa, ilikuwa ni desturi ya Wakristo kukutana katika siku hio. Vile vile, ushahid huu uliweza kuoneka katika Karne ya Pili, Soma (Ignatius, Epistle to the Magnesians, 1. 67).
Katika Makanisa mengi sana ya leo" SIKU YA BWANA" inafahamika kuwa ni Jumapili kama ilivyo kuwa tokea Karne ya Pili
Nategemea huu ushahid unatosha kukuambia kuwa Biblia hamlazimishi mtu kusali siku ya Jumamosi. Kma unashida ya aya angalau moja basi Warumi 14 aya ya 1-12 imetupa haki ya kuchagua siku ya kumwabudu Bwana Mungu ambayo inaweza kuwa Jumatau, Jumanne, Tuma Tano, Alahamisi, Ijumaa, Jumamosi au JUMAPILI. Zote hizo ni siku za Bwana.
Na hakuna mwenye haki ya kukuhukumu unapo amua kusali Jumatatu au siku yoyote ile. Soma Warumi 6 aya 14. KUMBUKA TUPO HURU KATIKA KRISTO.
Hivyo basi, leo nimewapa ushahid kadhaa kuhusu siku halali ya kuwambudu Bwana Mungu. SIKU ZOTE NI ZA BWANA.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba
For Max Shimba Ministries Org
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
No comments:
Post a Comment